Mfumo wa Sheria wa Tanzania unabagua Wahalifu kulingana na uwezo wa uchumi au cheo?

Mfumo wa Sheria wa Tanzania unabagua Wahalifu kulingana na uwezo wa uchumi au cheo?

roadmaster

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2023
Posts
1,609
Reaction score
2,751
Kweli, hili linaniogofya sana! Kuna hali isiyo ya kawaida katika utoaji wa haki hapa Tanzania. Hili linajitokeza hasa miaka ya sasa. Nimegundua wenye uwezo wa kiuchumi na vyeo serikalini huwa wanabebwa na kutoadhibiwa pindi wanapofanya makosa, tofauti na miaka ya nyuma.

Kuna mifano hai inayothibitisha ninachosema.

Kuna gari la mbunge limekamatwa na wahamiaji haramu, mpaka leo polisi wamekausha na hakuna kinachoendelea. Sijui ingekuwaje kwa mlalahoi angekuwa amefanya kosa kama hili.

Kuna huyu mkuu wa mkoa wa Simiyu, amemlawiti mwanafunzi. Mpaka sasa kimya, wakati ushahidi upo wazi. Sijui ingekuwaje kama angelawiti mlalahoi.

Kuna kiongozi aliendesha gari akagonga na kuua watu wawili kwenye bajaji maeneo ya Masaki. Kesi ilipigwa danadana ikapotea.

Kuna kiongozi aliua dereva wa daladala kwa kumpiga risasi kichwani. Hakuna kilichoendelea mpaka muuaji alipofariki. Sijui ingekuwaje kama muuwaji angekuwa raia wa kawaida.

Matukio ni mengi sana. Sijajua kama mfumo wa sheria unatetea viongozi au vipi.

Nikiwa mdogo, nilisoma kwenye gazeti pendwa la Mfanyakazi kwamba kuna mbunge wa Songea alifungwa miaka mingi kwa kusafirisha meno ya tembo. Kama sikosei, alikua anaitwa Abdurabi. Alikwenda jela miaka ya kutosha. Nadhani wakati ule mfumo wa sheria ulikuwa tofauti na sasa.
 
Ndugu umesahau na mafisadi,wao wanakiri kosa halafu wanaingia makubaliano na DCI mwishowe kesi inaondolewa mahakamani!!!
 
Back
Top Bottom