Mtindo huu utaitafuna sana CCM na kuna baadhi ya mambo wanayajutia kuyakubali kwa upambe lakini ndiyo hali waliyo iruhusu wenyewe
CCM ya sasa ukiweza ku mobulise wajumbe kwa namna yeyote ya kuwafurahisha basi unaweza kuwa rais hii ni hatari sana kwa usalama wa nchi
CCM ilishakufa ndio maana wanahangaika kuiua CHADEMA kwa gharama kubwa sana . Chama hai hakiwezi kuhangaikia uchaguzi wa chama kingine eti kipate mgombea dhaifu.
Kujenga upinzani dhaifu ni kujenga taifa dhaifu na siku moja kuwa na wawakilishi dhaifu na hata viongozi dhaifu.
Tanzania tumejikuta kwenye nchi iliyogeuza ufisadi kuwa ni sifa na ushujaa .
Wadogo ndio wanaobanwa na kushughulikiwa kisawasawa .
Leo Lisu akitaja mafisadi na kuyakemea anaonekana anaropoka lakini Trafiki akipewa pongezi na kondakta anaonekana anachafua jeshi la polisi na serikali . Anayesambaza picha za buku moja wanazopewa trafiki ili wanywe maji kutokana na jua la Dar hatuoni akikemewa lakini anayesema kuna mamilioni ya dola yanatumika kuhonga wapinzani anakamatwa na kuwekwa ndani eti analeta taharuki.
Hivi hii nchi nani amewaloga hawa wakuu wa vyombo vya dola na serikali ya CCM . Hivi taharuki kubwa ni ipi watu kukosa imani na polisi au wanachama wa CHADEMA kukosa imani na Mbowe.
Polisi wanadhalilishwa kwenye mitandao kwa kutegeshewa kamera kisha kurushwa mpaka Kwenye vyombo vikubwa vya habari ili tu wananchi wakose imani na Jeshi lao kwa pesa ambazo hatukuona wakiomba kama rushwa zaidi ya kua kama Kibati tu cha trafiki na madereva .
Watu wanaiba mabilioni huko TANESCO haziingii serikalini japo watu nananunua Luku bei juu. Pesa za bandari zinakwapuliwa zinahalishiwa Dubai . Utalii hauna tija inayolingana na utalii na mapato yanayongia nchini . Pesa zinaishia mifukoni mwa wasanii wachache . Pesa za mauzo ya wanyama hai hazijulikani zinakwenda tangu Mwaka 1991 mpaka leo kule dunia wamejaa wanayama wengi wanakaribia na Serengeti . Lakini nchi bado inashindwa kujanga miundo mbinu ya kuhakikisha trafiki hawasimamii kwenye vumbi na moshi wa magari barabarani .
Hata mfumo tu wa faini wameshinda kuiboresha uwe unaingia kwenye mifumo mingine ya kifedha na kulipa pesa za serikali bila kukamatana na kudaiana madeni huko njiani .
Treni ya mwendo kasi leo hii akipewa mtu binafsi ataheuka kuwa bilionea kama Bakheressa alivyopewa shirika la la kusindika chakula na mitambo yake ,leo hii ni bilionea .
Kila kitu seikali imeshindwa kukisimamia lakini wakiambiwa wanasema ni taharuki . Hivi ni taharuki gani inayosemwa wakati Magufuli aliendesha nchi mwenzi mzima bila Waziri hata mmoja wala naibu waziri. Je, unaweza ukaendesha nchi mwezi mzima bila polisi au trafiki kwa mkoa kama DSM ?
CCM ukitafakari na ijitofautishe na vyombo vya dola . CCM ni chama tu kama kilivyo chama cha mpira TFF na UDP , Chauma ,DP ,CHADEMA .n.k. Wasijione eti bila CCM nchi itayumba. Wao ndio watayumba kwenye mifuko yao lakini sio Taifa . Zaidi watu watapata mabadiliko na kuondokana na unyonyaji wa matajiri wanaoifadhili CCM pamoja na ugaidi maana wafadhili wengi wa CCM ndio pia wanaofadhili ugaidi. Akiwemo gaidi Mbowe.