Konny Joseph
Senior Member
- Aug 28, 2016
- 118
- 199
Nimejaribu kufuatilia michakato ya usajili na uajiri wa vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama.
Kikubwa nilichokigundua ni kwamba mfumo wa uajiri wa JWTZ bado ni wa kizamani sana, jambo ambalo linaweza kusababisha kuwepo kwa mianya ya rushwa.
Mpaka leo kwa taasisi kubwa kama JWTZ kuendelea kutumia mifumo ya kizamani ya kuandika barua kwa mkono na kutuma kwa sanduku la posta ni wazi kwamba mifumo ya taasisi bado ni ya kizamani na haiendi na wakati.
Sababu ya usiri haina uzito kwa kuwa sio kila kitu kinachohusu jeshi huwa ni siri.
Kama Polisi na Magereza wamefikia kuwa na mifumo ya kisasa ya uajiri na usajili kwa nini ishindikane JWTZ?