Mfumo wa USA Dollar ulivyoanza kutumika Duniani, na Kupelekea Dunia Kuchezeshwa DECI (Ponzi Scheme)

Kumbuka nchi karibia zote duniani zinadaiwa na WB ama IMF...in terms of dolar.kwamba madeni yalipwe kwa dola. Una epuka vp huo mtego?

Unakumbuka vita vya Ukraine vilivyopoanza walimuwekea vikwazo Urusi na wakamwambia alipe madeni yake kwa USD. Russia akakataa. Aliwaambia wanunuzi kutoka Ulaya wote walipie gesi na mafuta walipie kwa Ruble.

Nafikiri ukiwa na uchumi mkubwa na uwezo wa kufanya biashara na washirika wengine unaweza kutoboa.
 

Gaddafi wa Libya alitaka kuanzisha huu mfumo wa pesa ya Afrika ilkiwa backed na Gold pamoja na mfumo mpya kabisa wa Benki ya Afrika, system za ku-settle transactions ya pesa tofauti za nchi tofauti za Afrika na Mifumo kama ya Swift na bank of Settlement.

Kikwazo kikubwa ni USA, watajaribu kila njia kuwaondoa wanaojaribu kuleta another altenative.

Ila kama majority ya nchi nyingi zenye nguvu wakikubaliana USA hataweza kufanikiwa kuwasambaratisha.

Nina uhakika, ni inevitable ndani ya miaka 50 ijao dunia itakuwa na mfumo mwingine.

Ukiangalia trends za uchumi, population, elimu, military power, technology kusambaa, nchi kujitambua nk.
 
BRICS naona kama wamepandikiziwa kirusi,mwendelezo unaanza kuwashinda.
 
Haya sasa ndio mambo ya msingi ambayo ubongo wangu unayahitaji, sio siasa.
 
BRICS wanapanga kuja na utaratibu mwingine usiotumia dollar. Vipi maoni yako? watafanikiwa?
Wabunge Congress USA walikaa Kikao mwaka jana mwezi wa Sita kuangalia hii issue ambao kwao walisema ni Tishio..., Pamoja na kuwa na egos za ajabu ajabu lakini baadi walielezea hatari kwa uchumi wao
Maneno ya wabunge
....................................................................................​
Luetkemeyer boasted of the many “economic advantages” that dollar hegemony gives to the United States:


Beatty’s rhetoric was less aggressive than that of Luetkemeyer, but she essentially echoed the same talking points, stating:

Marshall Billingslea, the Treasury’s assistant secretary for terrorist financing under Trump, who also previously worked in the Pentagon, expressed concern that the central banks of China and Russia have been de-dollarizing their foreign-exchange reserves and instead buying other assets, such as gold, which cannot be easily sanctioned:

Kim singled out the currency swap-line agreements that the People’s Bank of China has signed with the central banks of other countries, such as Argentina, which is a way for Beijing to give liquidity or credit in yuan, bypassing Washington-dominated financial institutions like the SWIFT inter-bank messaging system:

Also present in the hearing was Daniel McDowell, an associate professor in the political science department at Syracuse University in New York, and author of the book “Bucking the Buck: US Financial Sanctions and the International Backlash Against the Dollar”.

McDowell argued that, by imposing more and more sanctions on countries around the world, Washington is actually weakening the dominance of the dollar.

The US has sanctions on nations that represent more than one-third of the global population and 29% of the world’s GDP.

McDowell explained:

 
Nilivyo kuelewa mimi.
Batter trade ndio mfumo halisi usio na dhulma. Unanipa mbuzi nakupa mahindi
Badala kunipa makaratasi uliochapa.
Batter teade iliondolewa na wahuni kudhulumu wengine. Hayo manhunu ya ulaya wanamiliki makaratasi.
Wizi mwingine unafanyika kwenye silaha. Kila mwaka unauziwa masilaha ambayo hujawahi yatumia na inawezekana usiyatumie, kazi yako inayobaki ni kutunza hayo masilaha kununua vipuri na kulipia gharama za wataalamu wa kutunza hayo masilaha ambayo ni kiini macho.
Baada ya miaka wanaunda masilaha mengine yale yanapitwa na wakati inabidi ununue mengine upeleke na wataalamu wa kuyatumia wawafundishe.
Badala ya kununua mashine za kulimia unanunua machuma ya kuweka bohari na wala vita haitokei na ikitokea ni hao hao wenye silaha ndio chanzo.
Kitu kingine wameweka class ya vitu na kuuza kwa bei kubwa mfano magari. Utasikia hayo magari ni ya kitajiri ila cha ajabu gari ya kitajiri imeundwa na chuma kilekille, plastiki zile zile, ngozi zile zile, vitambaa vile vile, rangi zile sile. Hi tujiulize kuna malighafi za tofauti zinazozalisha gari za kitajiri ? Jibu ni hamna huo ni utapeli wa kimagharibi kuibia mazwazwa hasa weusi na warabu.
Unauziwa majina ya magari. Bahati mbaya sana watetezi wa wazungu ni mtu mweusi. Mtu mweusi ni kiumbe cha ajabu sana.
 
Nadhani cha maana kama nchi tuache kutegemea hizi pesa za kigeni kama ndio kila kitu na kuweza kufanya hivyo inabidi kuwa na uwezo wa anagalau kujitegemea na sio kila unachotaka lazima ukitoe nje.
Uko sahihi ila wazungu wanatamka wazi hawawezi kuruhusu Afrika ijitegemee. Wanadai walifanya kosa kwa nchi za Asia sasa ikitokea Afrika wao watashindwa kuishi maana hawatauza bidhaa zao ukizingatia wao sio wengi na baina ya nchi zao wanaunda vitu vinavyo fanana mfano magari viwanda.
Kwa hio wanatumia kila hila kuzuia sisi kujitegemea na kudhibiti viongozi wetu.
 
Nilivyo kuelewa mimi.
Batter trade ndio mfumo halisi usio na dhulma. Unanipa mbuzi nakupa mahindi
Badala kunipa makaratasi uliochapa.
Barter trade ni ngumu kuanza kunipa mimi mahindi ili nikupe mbuzi inawezekana trade ikachukua muda mrefu zaidi kwahio kuna kipindi watu walitumia sarafu hizo hizo, gold au silver na wafua vyuma goldsmiths sababu walikuwa na masefu ya kuweka hizo gold na sarafu kwao ilikuwa rahisi sana kutoa risiti kwamba bwana fulani ana gold kiasi fulani hivyo apate huduma kwa kiasi fulani cha gold.., hawa blacksmiths wakagundua kwamba huenda kwa wakati husika ni vigumu sana kila mtu kuja kuchukua gold zake..., hivyo wakaanza kutoa makaratasi zaidi hata ya uwezo wa gold uliopo na hii ndio mbinu inayotumiwa na mabenki mpaka leo hii ni kwamba kila mtu akishituka labda nchi inafirisika ni kwamba pesa iliyopo Benki na Watu wanayodai haitoshi...

Theoretically huu mfumo huenda ukawa mzuri iwapo pesa ya kwenye mzunguko ikiwe inatengenezwa kwa njia ya mikopo..., yaani wewe ukienda kuomba mkopo wa bilioni moja (benki hawana bilioni moja) ila wanakukopesha hio bilioni moja plus commission; sasa ukienda kuzalisha hio bilioni moja kitaa ni kwamba kwa nguvu zako wewe utakuwa umeongeza bilioni moja kwenye mzungoko na kuwapa benki faida yao (commission)...

Ingawa kinachotokea USA sio hivyo Serikali inakopa haizalishi bali kuwalipa waliokopa juzi na nyingine kuzitumia (Ponzi Scheme)
Batter teade iliondolewa na wahuni kudhulumu wengine. Hayo manhunu ya ulaya wanamiliki makaratasi.
Huu mfumo ulivyoanza ni kwamba ulikuwa umewekwa kwamba pesa zifuate dollar na dollar ifuate gold; hivyo hata USA asingeweza kuprint pesa nyingi kuliko deposit yake aliyonayo (Ila USA kwa ujanja akawa anaprint pesa kuliko deposit yake) alifanya Utapeli; watu kushituka na kuanza kutumia gold kama exchange na sio dollar (1971) Nixon akaondoa utegemezi kwenye dollar sababu dollar zilikuwepo nyingi kitaa kuliko uwezo wake wa gold...

Kwahio kuanzia hapo ni kwamba anaprint madollar anavyotaka (kila mwaka matumizi yake yanazipo mapato); na dunia nzima ndio inayomkopesha (kwa kuwauzia government bonds) hivyo mikopo yake ni ya bei nafuu sana na siku dollar ikifa nchi nyingi zitaingia kwenye shida sababu savings za nchi nyingi zipo kwenye hizi Bonds

Ingawa huenda ameanza kujifunga mwenyewe kwa kuanza kutumia sana dollar kama silaha (kuwawekea vikwazo nchi kama Urusi na kuchukua pesa zako zilizopo USA) kumefanya watu kuwa waoga sababu siku ukikosana na USA pesa zako zitashikiliwa... Kwahio watu wameendelea kuwaza Dedolarization...
Naam hii wametumia sana hata UK kwa kuwauzia waarabu huko Middle East kwa kuwaonga viongozi wao.., BAE walitaka kumpa issue Regan ya ma bilioni ya pesa kuwauzia silaha Regan akaona noma sababu washikaji zao Israel hawatapenda..., Regan akampa pande Margaret Thatcher na hio tender iliwafaidisha sana UK na pamoja na BAE kutoa Hongo za kufa mtu kwa Prince Banda yaani walitoa Hongo ya Poundi Bilioni Moja, sasa imagine hio tenda ilikuwa ni ya kiasi gani;
Ingawa kwa hili siwalaumu wao bali watu wetu ambao wamekuwa walafi kuwaza kupata vijisenti badala ya ustawi wa jamii ya leo na kesho...

Hata sisi tulitaka kununua Radar huko ila hata baadhi ya watu wa huko wakatushangaa (Yaani wao wana uchungu kuliko hata sisi

 
ivyo wakaanza kutoa makaratasi zaidi hata ya uwezo wa gold uliopo na hii ndio mbinu inayotumiwa na mabenki mpaka leo hii ni kwamba kila mtu akishituka labda nchi inafirisika ni kwamba pesa iliyopo Benki na Watu wanayodai haitoshi...
Seriksli ina print pesa kwa kuthamanisha na nini ? Kama sio ule ule wizi wa kuchapa dollar.
 
Seriksli ina print pesa kwa kuthamanisha na nini ? Kama sio ule ule wizi wa kuchapa dollar.
Naam huu ndio mfumo wa kisasa unaotumiwa na Dunia (FIAT Money) ambao kweli ni Desi ila huku angalau kwenye mfumo halisi (best case scenario) ni kwamba Mabenki ndio yanatengeneza pesa; Na sio Serikali kutumia pesa zaidi ya makusanyo na kuchapisha kila wanavyojisikia na kutengeneza Bonds...,

Na huo mfumo ni kwamba ukienda Benki pesa unazopewa sio kwamba benki anazo ila ukianza kulipa ndio wewe unaziongeza kwenye mzunguko... (Huo bado ni wizi ila bora huu wizi kuliko wizi wa USA, wa kufanya dunia nzima wacheze Desi yao na kujipatia mikopo ya Bei rahisi kuliko wengine) wakati sisi tunakopeshwa na kina IMF na wajukuu mpaka wajukuu wanalipa..., USA wao wanachapisha kwa kutoa Government Bonds ambazo marejesho yake ni madogo na wanarejesha kwa kuprint madollar mengine... (Yaani matumizi yao ukilinganisha na mapato ni mara mbili kuliko nchi nyingine yoyote)
 
Kikawaramba
 
Hahaa US katufanya dunia nzima matahira kumbe
 
Huu uzi una madini kinoma lakini nashangaa hadi leo haujaenda sana.

Wale Pro-US siwaoni kabisa humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…