Madibira 1
JF-Expert Member
- Jan 6, 2023
- 358
- 831
Mfumo wa utoaji na usahihishaji Mtihani wa darasa la Saba ubadirishwe
Ndugu Wanabodi, nimeangalia na kusikia kuhusu kiongozi alietangaza kusitishwa masomo Ili kupisha KKK. Mwalimu ameshaandaa mpango kazi, scheme of work, lesson notes n.k anaambiwa asitishe. Mimi mwalimu wa sekondari nahusikaje na KKK?
Alichokisema waziri naungana nacho Kwa asilimia 75 kutokana na kilichopo mashuleni. Mwezi march mwanzoni kulikua na zoezi la upimaji wa watoto kusoma, kuandika na kujitambulisha Kwa kiingereza japo kwa sentensi tano na kuendelea. Lakini kwenye kituo nilichokuwepo hapa shinyanga Hali si Hali yaani kwenye kuandika 80% walifanya vibaya Sana, kwenye kujieleza waliishia salamu tu, kwenye kusoma ndio kabisaa hakuna kitu. Nafikiri atakua ameangalia aina ya taifa tunalolizalisha Kwa siku za mbeleni.
Lakini Nini kinafanyika
Mtoto anaanza darasa la kwanza mpaka la Saba kimazabe na mwisho anakuja kupimwa Kwa kusiliba! Hata Kama hajui kusoma na kuandika kusiliba ataweza tu, maana namba ya mtahiniwa wanabandikiwa kwahiyo anakopi vizuri tu.
Najua lengo la kusema watoto wasilibe ilikua ni kuokoa bajeti wakati wa kusahihisha lakini matokeo yake ndio haya. Katika mtihani wa maswali 45 ni maswali matano tu yenye jumla ya alama kumi tu ndio yakuandika au kukokotoa. Hapa mtoto mwenye uwezo mkubwa wa kudanganya au kutazamia Kwa mwenye uwezo anatoboa vizuri tu na kuingia sekondari.
Nini kifanyike
Ningependa ule mfumo wa zamani ambao ulituzalisha sisi akina senior jobless na mpwayungu village miaka ya 2007 kurudi nyuma kutumika. Yaani kwenye hesabu hakuna swali la kuchagua na masomo mengine kuchagua ni sehemu (section) A tu. Piga ua galagaza mtoto asiejua kusoma Kwa mfumo ule ilikua ni ngumu kutoboa na sekondari tulienda wachache Sana.
Pia serikali iache kuingilia taaluma za watu na kuwapangia Nini Cha kufanya. Kiongozi ambae anajua kabisa shule Haina walimu wa kutosha madarasa machache na wanafunzi ni wengi anaamuru mwalimu kuhamishwa iwapo hatafaulisha watoto wengi! Matokeo yake mwalimu anajiongeza hata Kwa kurubuni wasimamizi kukaa nje Kwa muda Ili wenye uwezo wawasilibie wasio na uwezo Ili mwalimu atetee kibarua chake. Serikali ingeacha asili iamue hatima ya mtoto yaani mwenye uwezo na asie na uwezo watenganishwe na akili zao na sio viongozi wa kisiasa. Ikumbukwe watoto Hawa ndio kundi la kwanza la elimu Bure ya Rais Magufuli ambao wamesoma kwa walimu wao wakipewa vitisho na amri za kisiasa jambo lililopelekea walimu kupika matokeo Ili kuwafurahisha viongozi.
Ushauri Kwa naibu waziri
Mheshimiwa waziri nikuombe usitishe mpango wako na uache walimu waendelee na program zao. Watoto Hawa ambao unawasitishia masomo Ili wasome KKK walishaandaliwa mfumo wao ndani ya siku za masomo 192 na walimu walishaweka taratibu zao. Vile vile watoto Hawa mwakani wanamtihani wa taifa je nao utasogezwa mbele Ili kufidia muda huu? Au utatoa tamko walimu wakimbizane na watoto kadili ya matamko yenu. Niombe serikali ikae pembeni katika hili kwakua wao ndio wazarishaji wa hili labda tuchuje watoto Kwenye mtihani wa mwisho wa kidato Cha kwanza na watakao chemka watafutiwe utaratibu mwingine.