Mfumuko wa bei huku mtaani unashamiri, kuna nini kinaendelea?

Mfumuko wa bei huku mtaani unashamiri, kuna nini kinaendelea?

FUTURE HUNTER

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
2,050
Reaction score
2,651
Salaamu watoto wa Jamhuri ya Muungano!

Kiukweli huku MTAANI vitu vinazidi kupanda bei siku Hadi siku.Nyama saizi 8000 Toka 7000. Juzi nimeenda dukani kununua Colgate naambiwa Sasa ni 5000/= ikiwa hapo awali nilikuwa nanuna 3500/.

Kwa ujumla vitu vingi bei vimepanda na sijaona tamko lolote kutoka mamlaka za serikali kuhusu hili. Je, Kuna inflation inapiga raia kimya kimya na serikali haitaki tamka rasmi?

Wataalamu naombeni uchambuzi ni ni kimesababisha Hali hii ghafla hivi.
 
Magufuli alidhibiti mazao na mifugo visiuzwe nje ya nchi kwa kufunga mipaka maana mazao yangeadimika, fikiria maisha yangekuwaje?

Japokuwa mkulima alikuwa hanufaiki lakini faida ni kubwa kuliko hasara, maana mahindi mchele mifugo n.k walahi tungetafutana
 
Hujaeleweka so unakubali sera zipi za Magu ama!!?
 
Magufuli alidhibiti mazao na mifugo visiuzwe nje ya nchi kwa kufunga mipaka maana mazao yangeadimika, fikiria maisha yangekuwaje?

Japokuwa mkulima alikuwa hanufaiki lakini faida ni kubwa kuliko hasara, maana mahindi mchele mifugo n.k walahi tungetafutana
fikiri kama mtu mwenye elimu hata unaweza hata kutumia internet. Sera hiyo ilikuwa ya hovyo sana na ilidumaza maisha ya wakulima ambao ni zaidi ya 70% ya watanzania wote. Ilikuwa sera ya hovyo iliyoasisiwa pasipo kufanyiwa utafiti
 
Kwa hiyo ni sababu ya ile TSH 100 kwenye Kila Lita ya mafuta?
usiione ndogo mkuu. maisha hayaonwi kwa issue moja.....hiyo sh 100 ina mlolongo wa athari nyingi kuanzia athari yake kwenye pembejeo mpaka usafirisha na uuzaji....ni mnyororo. Ndiyo sababu watunga sera na watoa maamuzi wanapaswa kuwa makini sana
 
Hayo ndo madhara ya rais kufariki akiwa madarakani, nchi inakosa uthibiti kabisa.......tunaposema mchakato wa katiba mpya uanze ni pamoja a kuweka sawa mambo kama haya ya succession plan.

Haiingii akilini mtu ambaye hachaguliwa kwa kura kwenye nafasi kubwa kama ya rais asimikwe kwenye nafasi hiyo kwa miaka zaidi ya minne.

Kwa uelewa wangu madaraka ya rais hayawezi kukaimiwa kwa zadi ya miezi sita kabla ya kufanya uchaguzi upya.
 
Back
Top Bottom