Mfumuko wa bei ni 3.1% Tanzania

Daaaah shopper market huku kwetu hakuna mzee.

Afu niliambiwa ata huko supermarkets mwisho kilo tatu
Huo ni uongo bei niliyokuambia ni uhakika hata ukienda kesho mkuu!
 
Mbona chama cha kijani kilituambia mfumuko wa bei umeshushwa na mzee baba mpaka 0% ??
 
Inaelekea mwaka wa tano sasa wakaazi walioko mkoani Kagera cement imekuwa ikiuzwa shilingi 21,500/= sasa sijui miaka yote hicho kiwanda kilikuwa kwenye matengenezo au la!
 
Huu ni uongo wa dhahiri huyo mama wamchukulie hatua,mfumuko kwa sasa ni 0% kuelekea Negative(-) inshort hakuna mfumuko wa bei kabisa.

Mitano tenaaaaaaaaaaaa.
 
Hiyo ni Dar nenda Shoppers Supermarket Mbezi Beach nanunulia hapo kila mara mkuu!
Kwa hiyo atoke temeke afuate sukari mbezi beach? Ukiongeza nauli na muda inakuwa bei gani?

Kwa nini isipatikane maeneo yote kwa bei hiyo? Nini maana ya kusogeza huduma kwa walaji?
 
Kwa hiyo atoke temeke afuate sukari mbezi beach? Ukiongeza nauli na muda inakuwa bei gani?

Kwa nini isipatikane maeneo yote kwa bei hiyo? Nini maana ya kusogeza huduma kwa walaji?
Mimi nilitaka kumwonyesha kuwa anachosema ni uongo bei ya sukali siyo bei kama alivyodai kuwa ni shs 5,000!!
 
Mbona kabla hata ya kujengwa kiwanda cha Dangote cement haikuwahi kufika huko, iweje matengenezo tu cement imefika huko? Halafu acha uongo, jana nimeona taarifa ya habari mkuu wa mkoa kaendakiwandani anawamaindi kuwa kwanini hawakuwa wametoa report kwenye vyombo vya habari kuhusu kusimamakwa uzalishaji kwa ajili ya matengenezo.
Hivyo usiwambie watu eti hawasikilizi walakusoma taarifa za nchi, maana hata hao dangote hawakuwa wametoa taarifajuu ya hili.
 
Mimi nilitaka kumwonyesha kuwa anachosema ni uongo bei ya sukali siyo bei kama alivyodai kuwa ni shs 5,000!!
Kumwonesha[emoji3582]
Kumuonesha[emoji3581]

Sukali[emoji3582]
Sukari[emoji3581]


Sijui hata shule kama mmewahi kupita nyie misukule!
 
2500 kutoka 1800


Ulizia Bei ya sukari Zanzibar
Sasa wewe ulitaka tuendelee kuwa hapo hapo? Maendeleo ni pamoja na bei kupanda na wananchi kuwa na uwezo wa kulipa. Yaani kipato kimepanda pia. Hivyo watz kwa sasa wanauwezo wa kulipa 2500 kwa kuwa kipato chao kimepanda ndiyo maana tuko kwenye nchi ya kipato cha kati!
 
Kumwonesha[emoji3582]
Kumuonesha[emoji3581]

Sukali[emoji3582]
Sukari[emoji3581]


Sijui hata shule kama mmewahi kupita nyie misukule!
Kwani tuko kwenye mtihani wa kiswahili mkuu? Hope umeelewa nilikuwa na maana gani.
 
Kreti ya bia ni Bei rahisi kuliko mfuko wa saruji a.k.a cement
Kwahiyo tunywe bia? Basi wacha watu wanywe bia!! [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
 
Nitafurahi sana siku wabunge wetu watakapokua wanachangia suala la mfumu
Kumwonesha[emoji3582]
Kumuonesha[emoji3581]

Sukali[emoji3582]
Sukari[emoji3581]


Sijui hata shule kama mmewahi kupita nyie misukule!
Eti ananunulia SUKALI shoppers. Kuna shule ya ujinga wanayosomea wapiga makofi.
 
Tra kutaka kuweka rekodi ya makusanyo wanapandisha kodi, muuzaji nae anapandisha bei ya bidhaa ili apate faida- maumivu kwa mlaji wa mwisho (wanannchi wa tanzania)
Kwa wale wa mipakani wanapata ahueni kwa kupenyeza magendo ndani ya nchi.
Wafanyabiashara wetu wanakosa wateja na hatimae wanafunga biashara zao.
Tra wanakosa makusanyo wanayotarajia ,,wanaona solution ni kupandisha kodi tena.

Hii cycle starling mchekeshaji anajijua [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hahahaha daah Kuna watu mnasikitisha Sana haki ya mungu.


Yani mwananchi afurahie kulipa Bei kubwa hivi hivyo vichwa vimejaa makamasi au mate.
 
Kwani tuko kwenye mtihani wa kiswahili mkuu? Hope umeelewa nilikuwa na maana gani.
Siwezi kuwa mkuu kwa mtu mpuuzi kama wewe. Usijiweke kwenye cycle yangu bora nimuweke mbwa kwemye cycle yangu kuliko "Jitu" puuzi kama wewe.
 
Ogopa mfumuko wa bei unaotokea kwenye Sukari, Cement au Petrol. Kwa sababu athari zake zinagusa kila eneo la kimaisha kwa wananchi wote.

Serikali inapaswa kuja na maelezo sahihi na uhakika kwa nini hili linatokea, tena linatokea sasa. Kusema ni kwa sababu Dangote kasimamisha uzalishaji, huko ni kujifariji kwa uongo, maana viwanda vya Saruji hapa Tanzania vipo vingi, tena mikoa tofauti tofauti (hata kabla na baada ya Dangote kuanza kuzalisha cement) na vimekuwa vikishindana kufanya biashara kiasi hata cha kuuza Cement nje ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…