Mfungwa aliyeachiwa kwa msamaha wa Rais akamatwa kwa wizi

Mfungwa aliyeachiwa kwa msamaha wa Rais akamatwa kwa wizi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
MFUNGWA ALIYEACHIWA KWA MSAMAHA WA RAIS MAGUFULI AKAMATWA NA POLISI

Mmoja wa wafungwa walioachiwa kwa msamaha wa rais mkoani Njombe anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa kosa la kuvunja nyumba ya kulala wageni ya Nang'ano mjini Makambako ili kuiba fedha.

Mussa Msolwa maarufu Hitler amedai alikwenda hapo kulala lakini tamaa ilimshika baada ya kuona fedha hizo.

1576070147105.jpeg
*****

Jumatatu Desemba 9, 2019 Rais wa Tanzania John Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 5,533 lakini mmoja wa wafungwa hao, Mussa Msola maarufu Hitler amekamatwa na polisi mkoani Njombe kwa tuhuma za kuvunja nyumba ya kulala wageni iliyopo mjini Makambako.

Msola ambaye kabla ya kuondoka katika gereza la Njombe aliomba msamaha mbele ya viongozi wa Serikali na maofisa usalama huku akiwasihi wenzake kuwa wema waendapo uraiani, aliachiwa huru jana Jumanne Desemba 10, 2019 saa 8 mchana.

Lakini saa nane baadaye alikamatwa na wananchi akiwa katika nyumba hiyo ya wageni ya Nang’ano iliyopo mtaa wa Mwembetogwa mjini Makambako akifanya uhalifu.

Rais Magufuli alitoa msamaha huo katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumatano Desemba 11, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issa amesema, “ninaweza kusema msemo wa Kiswahili kuwa sikio la kufa halisikii dawa umetia leo Njombe baada ya mtuhumiwa mmoja Mussa Msola maarufu Hitler.”

“Aliyepewa msamaha (na Rais) na kuondoka Njombe kuja Makambako jana mchana lakini baada ya saa nane tangu atoke gerezani alishawishika na kufanya tukio la uvunjaji na wa nyumba ya kulala wageni ya Nang’ano.”

Issa amesema mtuhumiwa huyo ambaye kabla ya kutoa gerezani aliwasihi wenzake kuwa wema na kuomba msamaha kwa viongozi waliofika gerezani kushuhudia wafungwa wakiachiwa, alikamatwa na wananchi na kufikishwa kituo cha polisi.

“Yupo polisi na tulipomhoji alisema tamaa zimemshika na akafanya hayo. Tunawataka wasirudie vitendo vya uhalifu watarudi jela. Maisha yake ameamua kuwa gerezani na atarudi gerezani,” amesema Issa.
 
Niccampoops... tuna mashudu vichwani

Mkuu wa Mkoa wa Njombe awapa ekari moja moja wafungwa waliosamehewa

Unam reward criminal, eti afanye kazi asirudi jela, sisi wa nje nani anatupa ardhi bure tuitumie tusende jela ???

Akili ya mtu mweusi mbolea tupu...
 
Ni kama kafanya makusudi anataka kurudi jela.
Ukiona hivyo hao ndio wenye biashara zao huko jela kama kuingiza na kuuza sigara, bhangi na ulanguzi wa bidhaa zingine za kawaida.
Sio ajabu kukuta ana mke au mume huko jela.
 
Niccampoops... tuna mashudu vichwani

Mkuu wa Mkoa wa Njombe awapa ekari moja moja wafungwa waliosamehewa

Unam reward criminal, eti afanye kazi asirudi jela, sisi wa nje nani anatupa ardhi bure tuitumie tusende jela ???

Akili ya mtu mweusi mbolea tupu...
Umenikumbusha Prof Muhongo na cheti chake!
 
Niccampoops... tuna mashudu vichwani

Mkuu wa Mkoa wa Njombe awapa ekari moja moja wafungwa waliosamehewa

Unam reward criminal, eti afanye kazi asirudi jela, sisi wa nje nani anatupa ardhi bure tuitumie tusende jela ???

Akili ya mtu mweusi mbolea tupu...
Mkuu wewe ndio utakua mbolea..

Unashindwa kuona kama hao waliopewa hizo ekari wana tatizo na wanahitaji msaada?umesahau wametoka jela hawana pakuanzia?Ama unafurahishwa warejee kwenye uwalifu tena?Ama unawaonea gere?Fanya uhalifu na wewe ukafungwe ukitoka tutakupa.

Jinga
 
MFUNGWA ALIYEACHIWA KWA MSAMAHA WA RAIS MAGUFULI AKAMATWA NA POLISI

Mmoja wa wafungwa walioachiwa kwa msamaha wa rais mkoani Njombe anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa kosa la kuvunja nyumba ya kulala wageni ya Nang'ano mjini Makambako ili kuiba fedha.

Mussa Msolwa maarufu Hitler amedai alikwenda hapo kulala lakini tamaa ilimshika baada ya kuona fedha hizo.

View attachment 1288690
Hizo fedha zilikuwa wapi?
 
Twende kisomi jamani. Ulipomsikia huyo mmoja kati ya wafungwa 5000 (1/5000), kitakwimu unaona hilo ni tatizo?
Ni tatizo sana tu, yaani kaiacha ekari yake moja aliepewa bure na kaamua kutaka kuiba tena? Huyu mtu hata elimu alioipata akiwa gerezani kaamua aiache, na tusitegemee huyo tu watajitokeza wengine!
 
huyo alikuwa ni wakupiga kiberiti tuu, mambo mengine ni kupoteza muda tuu
 
Back
Top Bottom