Mfungwa aliyeachiwa kwa msamaha wa Rais akamatwa kwa wizi

Maisha ya uraiani kwa mtu aliyekaa ndani ni magumu ku adjust, lazima uwekwe sawa kisaikolojia kabla ya kurudishwa mtaani.
 
Twende kisomi jamani. Ulipomsikia huyo mmoja kati ya wafungwa 5000 (1/5000), kitakwimu unaona hilo ni tatizo?
Mkuu,hiyo ni sehemu tu ya changamoto za hawa watu wakirudi uraiani. Jana kuna ule uzi wa yule jamaa aliyekataa kutoka jela baada ya msaada, kuna baadhi ya wachangiaji walo-raise concern kuhusu maana halisi ya kumfunga mtu baada ya kupatikana na hatia.

Magereza kama kule Zanzibar wanavoita inapaswa kuwa chuo cha mafunzo,yaani mfungwa akitoka jela awe mtu bora kuliko alivoingia kitabia.

Nadhani ndio hapo kwenye tatizo,magereza yetu yanarundika tu watu bila kuwabadili tabia na mitazamo yao warudipo uraiani.
Na watu wameshauri sana pia kuhusu namna ya kuwajengea uwezo wa kujipatia riziki warudipo uraiani japo kwa kuwapa skills mbalimbali km za uashi,useremala,mekaniksi,kilimo,ufugaji nk na hata kuwaajiri kwenye baadhi ya miradi inayotekelezwa na magereza kwa fani husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
moja ya makosa makubwa wanayofanya magereza ni kutowaandaa wafungwa kuishi maisha mengine baada ya kutoka jela kama kuwapatia elimu au ujuzi wanaoweza kuutumia kama maisha mbadala ya uhalifu ingawa wengine watasema mbona kuna watu walifaulu kupitia chuo kikuu huria wale walifaulu kwa juhudi zao binafsi sanasana magereza walitoa sapoti kwa sababu hakukuwa na njia mbadala ys kumzuia.
Kama ingefanyika study ingeonyesha wafungwa wengi ni watu wanaorudia kufanya makosa badla ya wale ambao wanafanya makosa na kutorudia hii inatokana na kutokuwa na njia mbadala ya kuishi ndio maana kibaka akitoka anakuja kuwa jambazi sugu lakini utaratibu wetu wa msamaha pia una matatizo ilitakiwa bodi ya parole ndio iwe ama inatoa au kupendekeza msamaha kwa wafungwa baada ya kufatilia na kujihakikishia tabia zao kuwa zimebadirika lakini wengi wanaoachiwa ni wahalifu waliokubuhu
 
Mkuu umekoment kikike kike haswa hapa....hujui mishe za jela wewe ukienda kule ukirudi mtaani unaanza zero kabisa yan back to square 1....kapewa heka 1 atapambana kuuza hata nusu iliyobaki anaanzia maisha yanasonga.

Halafu katika maisha kuna opportunity nyingine zinatokea na kuanza baada ya kumess up kumbuka hao walipokuwa jela walikuwa wanapata ujuzi wa kilimo.

Endelea kudoea pizza ya dada akiletewa na shemeji.
 
Umepata wivu wafungwa kuachiwa?

Haya kafungwe wewe sasa ufurahi

Upinzani kwa wivu hamjambo

God first
Akili ya tope wewe, sijaona sehemu yeyote ambapo mleta mada ameonesha wivu kwa wafungwa walioachiwa na Meko ili kutafuta kiki.
 
Siku za hivi karibuni rais amekuwa akiwapigia kelele Jeshi la Magereza na Wizara nzima kwa kutowatumia ktk kazi. Wanatakiwa watumike ili hatima ya kifungo chao itoe matokeo ya uzoefu wa jambo fulani, badala ya kulima tuuu! Akiachiwa anapewa tena shamba wakati anafahamu kilimo ni adhabu.
 
Hao wafungwa bado ni vijana sana lazima watarudia uhalifu. Wangebaki tu jela kwa maoni yangu!!!
 
another abject dunderhead

ex-criminal hatakiwi kuwa rewarded just because he came out of jail...

hana pa kuanzia? nani anacho?

hana pa kuanzia, kwani kabla ya jela hakuwa uraiani?

Watanzania wanakodi ardhi, wana renti farm equipment, watengeneza kahela waishi, yeye anapewa ardhi ya bure, ye nani, what is so special about an ex convict, ye naniii????

mbumbumbu popoma mkubwa
 
Yupo polisi na tulipomhoji alisema tamaa zimemshika na akafanya hayo. Tunawataka wasirudie vitendo vya uhalifu watarudi jela. Maisha yake ameamua kuwa gerezani na atarudi gerezani,” amesema Issa.

Labda alikuwa anatafuta zawadi ya kupeleka nyumbani kwaajili ya sikukuu
 
Angalau Ali test hewa ya uraiani
 
Ni tabia iliyo ndani ya damu na nafsi yake kuacha sio rahisi hata kama anakipato kukubwa kama ni tabia hataiacha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…