Mfungwa wa tukio la Ugaidi Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya, Rashid Mberesero adaiwa kujinyonga Gerezani Kamiti

dah...hawa ndo wale imani kali kabisa dini imeingia mpaka kwenye mifupa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefuatilia sana mkasa wa huyu jamaa toka siku anakamatwa baada ya tukio, nilimsikia mama yake mzazi akihojiwa na BBC nakusema kijana wake alikuwa mtu wa swala tano, mkimyaa, asiyependa kujichanganya na vijana wenzake, alichaguliwa kujiunga na Bihawana High school 2014 lkn alivyokuwa shuleni walimu walikuwa wakimkataza kuvaa kibaraghashia darasani lkn alikua hasikii hivyo mara nyingi kuingia mgogoro na walimu, siku anakamatwa huko Gharisa walimu walikuwa hawana taarifa zozote kama hayuko shuleni, ila wanafunzi waliokuwa wakisoma naye mchepuo mmoja walikuwa hawamuoni darasani wala shuleni na wenyewe walizani walimu wana taarifa zake kwanini hayupo shule.

Mama yake mzazi akihojiwa mapema mwaka huu alikuwa akisikitika kuwa toka kukamatwa kwa mwanaye hajawahi kuwasiliana naye wala kumuona, na alikuwa hana uwezo wa kuhudhuria mahakamani jijini Nairobi ili kusikiliza kesi ya mtoto wake, na vilevile alisema kwasasa ni mgonjwa wa pressure ya kupanda na kushuka toka alipopata taarifa za mtoto wake kuhusika kwenye ugaidi, Baba mzazi wa marehemu Mberesero alishafariki kwahiyo alikuwa akielelewa na baba wa kufikia.
 
NAONA WATU WENGI WANAKENGEUKA.

Ni mshukiwa wa ugaidi na bado mahakama haijathibitisha.
 
kwa jinsi ninavyowajua polisi wa kenye huyo watakua wamemnyonga tu
 
Jamaa alitoroka shulen kwao akamfata Demu wake kwenye hicho chuo likapigwa tukio na yeye akashikwa kwnye eneo la tukio wakamuunganisha kwenye hiyo kes hakua gaid chalii hajui hata kupakia risas kwenye magazine
Hujui unachoongea, huyo Bihawana secondary walikuwa wanamjua mzee wa itikadi Kali, iweje awe na demu huku mzee swala tano Tena itikadi Kali?

Dogo alijiunga Al shabab kupitia shehe Ilunga branch ya Abdul Rongo Kenya, na akapewa mafunzo!

Kwenye chuo kile alienda akiwa master plan wa tukio maana alikuwa kijana sawa na wanachuo hivyo vigumu kushtukiwa!!

Ndomana Al shabab walivyokuja under his instructions hawakuweza kumdhuru maana Ni mwenzao!
 
Kwamba siku hizi shule za sekondari zinatoa ruhusa kwa wanafunzi wa kiume kufuta mademu zao vyuoni?
Unapokuwa unaingia kwenye shida lazima useme ukweli!alivyoomba ruhusa angesema hivyo hivyo, haiwezekani demu asiwaambie wenzake ana jamaa yake anakuja kumtembelea, lazima ingejulikana.
 
kwa jinsi ninavyowajua polisi wa kenye huyo watakua wamemnyonga tu
Hakuna ushahidi wa jamaa kuhusika na ugaidi, halafu sijui kama wachunguzi kutoka Tanzania walihusishwa, hii ki diplomasia sijui imekaa je

Mda mwingine namwelewa sana Magufuli maana hawa wakenya wana mambo ya kijinga kweli
 
Hakuna ushahidi wa jamaa kuhusika na ugaidi, halafu sijui kama wachunguzi kutoka Tanzania walihusishwa, hii ki diplomasia sijui imekaa je

Mda mwingine namwelewa sana Magufuli maana hawa wakenya wana mambo ya kijinga kweli

Nini kazi ya polisi na mahakama. Ujui majukumu yao
 
Huyo gaidi akatwekatwe vipande vipande then akatupwe chooni.
 
Amekata tamaa mapema sana, bado alikuwa ana nafasi ya kutoka gerezani.
Nani angemtoa? Maana sidhani kama hata kuna mtu alikwenda kumuona au kutaka kujua ukweli kutoka kwake zaidi ya polisi na mahakama ya Kenya
 
Si alikuwa mwanafunzi hapo chuoni.
Hapana mkuu huyu alikuwa mwanafunzi mkoani Dodoma (Bihawana kama sikosei) na tukio lilipotokea alitakiwa awe shule alianza kubadilika taratibu kiimani baadae akatoweka shuleni hata wazazi walijua yupo shuleni si Kenya, na yeye alipokamatwa alisema alikwenda kumsalimia rafiki yake, hizi ni taarifa za Mwanzo tu alipomakatwa baada ya hapo sikufuatilia tena habari zake
 
We jamaa bana hivi upo serious? Huyu alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tano bihawana secondary huko dodoma. Na aliondoka hapo shuleni bila taarifa, ndio hadi anakuja kukutwa kwenye hilo tukio huko kenya.

Wazazi wake walijua yupo shule.
Hii habari nilipata vizuri kwa mwanafunzi mwenzie wa darasa moja ambaye amemaliza chuo huu
 
UPARENI kuna siasa kali sana, serikali ianzishe kanda maalum, pale KIRINJIKO, HEDARU, MAKANYA NA SAME SI SALAMA kivile hasa kwa hawa vijana.
Huyu Gaidi aliyeua watu 146 ni familia ya kina Mberesero wenye Ksmpuni za Mabasi , sitaji majina ila mnayajua wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…