Mfungwa wa tukio la Ugaidi Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya, Rashid Mberesero adaiwa kujinyonga Gerezani Kamiti

Mfungwa wa tukio la Ugaidi Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya, Rashid Mberesero adaiwa kujinyonga Gerezani Kamiti

Shuleni alipewa Suspension kwa kosa la kuvaa barakashia parade,maana aliambiwa avue akagoma, Mkuu wa shule akamwambia aende nyumbani akijua ya kwamba jamaa ataogopa na kuomba msamaha lakini jamaa alibeba vitu vyake akasepa asubui mapema na hapo shule tukijua ya kwamba Jamaa kaenda kwao
dah...hawa ndo wale imani kali kabisa dini imeingia mpaka kwenye mifupa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu kijana kwa kumuangalia tu anaonekana ana tatizo la msongo wa kimawazo au ugonjwa wa schizophrenia angepimwa akili kwanza na kuchunguza historia ya familia yao kiakili si ajabu alikuwa innocent suala la kusema alikuwa anafanya nini juu ya dari sio kigezo cha kumuhukumu.
Kwani mtu ukipita mahali ukakuta watu wanamimina risasi ukaingia nyumbani kwa mtu darini kusetiri maisha yako ukija kamatwa utahusishwa na kosa?
Wakati mwingine kuna watu hawajui kujieleza angepewa mwanasheria ingejulikana mbichi na mbivu.
Simtetei wala sitetei ugaidi ila je Kenya walichunguza mambo yote haya?
Nimefuatilia sana mkasa wa huyu jamaa toka siku anakamatwa baada ya tukio, nilimsikia mama yake mzazi akihojiwa na BBC nakusema kijana wake alikuwa mtu wa swala tano, mkimyaa, asiyependa kujichanganya na vijana wenzake, alichaguliwa kujiunga na Bihawana High school 2014 lkn alivyokuwa shuleni walimu walikuwa wakimkataza kuvaa kibaraghashia darasani lkn alikua hasikii hivyo mara nyingi kuingia mgogoro na walimu, siku anakamatwa huko Gharisa walimu walikuwa hawana taarifa zozote kama hayuko shuleni, ila wanafunzi waliokuwa wakisoma naye mchepuo mmoja walikuwa hawamuoni darasani wala shuleni na wenyewe walizani walimu wana taarifa zake kwanini hayupo shule.

Mama yake mzazi akihojiwa mapema mwaka huu alikuwa akisikitika kuwa toka kukamatwa kwa mwanaye hajawahi kuwasiliana naye wala kumuona, na alikuwa hana uwezo wa kuhudhuria mahakamani jijini Nairobi ili kusikiliza kesi ya mtoto wake, na vilevile alisema kwasasa ni mgonjwa wa pressure ya kupanda na kushuka toka alipopata taarifa za mtoto wake kuhusika kwenye ugaidi, Baba mzazi wa marehemu Mberesero alishafariki kwahiyo alikuwa akielelewa na baba wa kufikia.
 
NAONA WATU WENGI WANAKENGEUKA.

Ni mshukiwa wa ugaidi na bado mahakama haijathibitisha.
 
kwa jinsi ninavyowajua polisi wa kenye huyo watakua wamemnyonga tu
 
Jamaa alitoroka shulen kwao akamfata Demu wake kwenye hicho chuo likapigwa tukio na yeye akashikwa kwnye eneo la tukio wakamuunganisha kwenye hiyo kes hakua gaid chalii hajui hata kupakia risas kwenye magazine
Hujui unachoongea, huyo Bihawana secondary walikuwa wanamjua mzee wa itikadi Kali, iweje awe na demu huku mzee swala tano Tena itikadi Kali?

Dogo alijiunga Al shabab kupitia shehe Ilunga branch ya Abdul Rongo Kenya, na akapewa mafunzo!

Kwenye chuo kile alienda akiwa master plan wa tukio maana alikuwa kijana sawa na wanachuo hivyo vigumu kushtukiwa!!

Ndomana Al shabab walivyokuja under his instructions hawakuweza kumdhuru maana Ni mwenzao!
 
Kwamba siku hizi shule za sekondari zinatoa ruhusa kwa wanafunzi wa kiume kufuta mademu zao vyuoni?
Unapokuwa unaingia kwenye shida lazima useme ukweli!alivyoomba ruhusa angesema hivyo hivyo, haiwezekani demu asiwaambie wenzake ana jamaa yake anakuja kumtembelea, lazima ingejulikana.
 
kwa jinsi ninavyowajua polisi wa kenye huyo watakua wamemnyonga tu
Hakuna ushahidi wa jamaa kuhusika na ugaidi, halafu sijui kama wachunguzi kutoka Tanzania walihusishwa, hii ki diplomasia sijui imekaa je

Mda mwingine namwelewa sana Magufuli maana hawa wakenya wana mambo ya kijinga kweli
 
Hakuna ushahidi wa jamaa kuhusika na ugaidi, halafu sijui kama wachunguzi kutoka Tanzania walihusishwa, hii ki diplomasia sijui imekaa je

Mda mwingine namwelewa sana Magufuli maana hawa wakenya wana mambo ya kijinga kweli

Nini kazi ya polisi na mahakama. Ujui majukumu yao
 
Huyo gaidi akatwekatwe vipande vipande then akatupwe chooni.
 
Amekata tamaa mapema sana, bado alikuwa ana nafasi ya kutoka gerezani.
Nani angemtoa? Maana sidhani kama hata kuna mtu alikwenda kumuona au kutaka kujua ukweli kutoka kwake zaidi ya polisi na mahakama ya Kenya
 
Si alikuwa mwanafunzi hapo chuoni.
Hapana mkuu huyu alikuwa mwanafunzi mkoani Dodoma (Bihawana kama sikosei) na tukio lilipotokea alitakiwa awe shule alianza kubadilika taratibu kiimani baadae akatoweka shuleni hata wazazi walijua yupo shuleni si Kenya, na yeye alipokamatwa alisema alikwenda kumsalimia rafiki yake, hizi ni taarifa za Mwanzo tu alipomakatwa baada ya hapo sikufuatilia tena habari zake
 
We jamaa bana hivi upo serious? Huyu alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tano bihawana secondary huko dodoma. Na aliondoka hapo shuleni bila taarifa, ndio hadi anakuja kukutwa kwenye hilo tukio huko kenya.

Wazazi wake walijua yupo shule.
Hii habari nilipata vizuri kwa mwanafunzi mwenzie wa darasa moja ambaye amemaliza chuo huu
 
Wakuu mnamkumbuka bwana mdogo Rashid Charles Mberesero, Mpare, aliyekuwa moja wa masterminder wa shambulio la Garisa University na kuua 148, amejinyonga Gerezani leo

Mapambano mema na kaburi na
Je, Sheria inasemaje? Atarudishwa Upareni na Seriakli ya Kenya?


---
One of the three people who were convicted of planning the Garissa University attack five years ago where 156 people were killed has been found dead.

Rashid Charles Mberesero was found dead in his cell at the Kamiti Maximum Prison where he was serving a life sentence.

“He committed suicide on Friday at 1520hours inside his cell using a blanket that he used to hang himself with from the grills. He was alone but the matter is under investigation. The body has been taken to the City Mortuary awaiting autopsy,” Prisons Spokesman Kennedy Aluda said.

Speaking to Citizen Digital on Sunday, Mr. Aluda noted that the matter will be handled by the embassy since the deceased was a Tanzanian national.

The deceased was among three persons who were convicted over the Garissa University terror attack which occurred in April 2, 2015.

Mberesero, Mohammed Abdi Abdikar and Hassan Edin Hassan were convicted for being members of al Shabaab, committing a terrorist act and conspiracy to commit terrorism.

“Prosecution has proved its case beyond any reasonable doubt,” ruled Trial Magistrate Francis Andayi, adding that the three were in communication with the attackers and knew of the plot.

The magistrate noted that the attack was carried out as an attempt to coerce the government into removing the Kenya Defense Forces (KDF) from Somalia.

According to the court, Mberesero led the attackers to the institution since he never explained the reasons as to why he was on scene when people were being asked to leave.

“He remained in the hostel when everyone had left and could not satisfactorily explain why he was there,” the court noted.

Over 22 witnesses testified in the case among them students and experts.
UPARENI kuna siasa kali sana, serikali ianzishe kanda maalum, pale KIRINJIKO, HEDARU, MAKANYA NA SAME SI SALAMA kivile hasa kwa hawa vijana.
Huyu Gaidi aliyeua watu 146 ni familia ya kina Mberesero wenye Ksmpuni za Mabasi , sitaji majina ila mnayajua wenyewe
 
Back
Top Bottom