Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
Je unaweza kushiriki chakula cha jioni ukiwa mtupu bila nguo na watu 40 usiowafahamu?
•
Huko nchini Marekani upo mgahawa unaowapokea wateja wanaopenda kupata mlo wakiwa watupu.
•
"The Füde Breathwork Experience" mjini New York City ni hafla ya chakula cha jioni ambapo washiriki hula chakula huku wakiwa hawajavaa nguo.
•
Gharama ya kiingilio ni kuanzia dola 44 hadi dola 88, ambazo zitakuwezesha kushiriki pia mazoezi ya kupumua na hatimaye kula mlo usiokuwa na nyama yaani chakula kitokanacho na mimea.
•
Wateja kwenye mgahawa huo, mara nyingi huwa ni watu ambao hawafahamiani, lakini hukaa pamoja na kula chakula.
•
Lengo la hafla ya Füde ni kuwasaidia watu kuunganisha 'nafsi zao na uhalisia wao halisi'.
•
Chanzo: BBC SWAHILI