Mgahawa wangu mambo yalikuwa mazuri, ghafla imedoda, nifanye nini biashara irejee kwenye mstari?

Mgahawa wangu mambo yalikuwa mazuri, ghafla imedoda, nifanye nini biashara irejee kwenye mstari?

Pole sana
Sina uzoefu na biashara ya chakula lakini nikuulize jambo
Je hukufungua kipindi hichi cha mfungo?
Je hapo ulipo hamna migahawa mingine?
Je una wapishi wazuri??
Bei zako vipi?

Ndugu yangu kama ulifungua kipindi cha ramadhani unaweza kukutana na changamoto sana
Lakin umesema siku za mwanzo wateja walijaa
So inawezekana ni wamekuja kutest ladha ya msosi kisha wakaukuta mbaya au bei zako zipo juu
Hivi unajua kuna watu wanawasha gari wanaenda kufata msosi mbali sana
Mimi ki ukweli nikija kwako kwa mara ya kwanza msosi ukawa mbaya hata kama unauza rahisi vip sirudi tena

Sehemu za vyakula mpishi anatakiwa kuzingatiwa sana wakati unafungua biashara ya msosi

Alafu pia LOCATION yako ipoje??
Mazingira yanaruhusu watu kuwa wengi kila siku??

Hilo la migahawa kuwa mingi inachangia sawa wateja kuwa na option za kutosha

Pia varieties za vyakula

Cha mwisho kabisa ambacho naweza nikakushauri japo post yako haijaeleza mambo mengi ili upate kushauriwa
Wakati unaenda kufata mahitaji yako sokoni omba MUNGU na ombea vile vitu
Kisha ombea hapo kazini ...ombea na vitendea kazi
Waweke na hao wafanyakazi mikononi kwa Mungu
Alafu pia asubuh sana wakati mnafungua hapo mwaga chumvi ya mawe nje na ndani
Na pia weka station ya mahubiri..yale maombi ya usiku kuamkia asubuh
Mpaka mkishafungua kila kitu kipo tayari ndo unazima redio/youtube
La mwisho consider delivery
Anza kupost msosi unaoutengeneza na ku offer delivery service
USIFUNGE BIASHARA
PIKA HATA KILO MOJA YA NCHELE ,kilo ya unga na mboga zingine kidogo kidogo
Ongeza na udambwi udambwi wa juyce,mtindi

Weka kila kitu kidogo kidogo
Option ya kufunga iwe ya mwisho
ALL THE BEST DEAR
Binafsi sehemu ninayoenda kula chakula napita migahawa karibu 6 ambayo Iko jirani yangu kabisa.
 
Kosa kubwa ulilofanya ni kufunga biashara, cha kufanya ungepunguza kiwango cha kupika kama ulikua unapika kilo 5 ungeshusha mpaka kilo 2 ukunikiendelea kushughulikia hiyo changamoto la tatizo la watejakupungua
 
Nataka nikuombee kazi hapo ukamsaidie kuuza chakula umwage tabasamu uwe mfano Kwa wengine
kama analipa vizuri,, mimi ni nani nikatae kazi jamani😇😇 hapo kwenye kuchekea wateja ndo penyewe kabisa,,, yaaan mpka wataanza kuhisi nawataka kumbe ni customer care yangu👌
 
kama analipa vizuri,, mimi ni nani nikatae kazi jamani😇😇 hapo kwenye kuchekea wateja ndo penyewe kabisa,,, yaaan mpka wataanza kuhisi nawataka kumbe ni customer care yangu👌
Basi nikuombee kazi Emirates airlines 🤣 siyo Kwa tabasamu Hilo 🤣
 
Kama wateja walikuwa wanakuja kwa siku 2 mfululizo kuna jambo hapo halipo sawa labda walikuwa wanajaribu kuona utofaut wa chakula chakona wengine na baadae wakaona n cha kawaida hvyo wameamua kurud walikokuwa wanakula mwanzo

Pili vipi kauli zako na za wafanyakaz wako inawezakana kipengele hicho hakipo sawa jichunguZe

Tatu washindan wako ambao walikuwa wanauza kabla yako nao wamejiongeza Zaid kwa kutoa discount au kuongeza kipimo na bonus mbalimbal

La mwisho ushirikina upo wala usisite lakn hil liwe la mwisho baada ya kujiridhisha hayo mambo matatu juu
muhimu kwa sisi 'maafisa shibe' ni USAFI. hakuna atakayevumilia uchafu wa vyombo, mabaki, mhudumu na vyombo. pia joto la chakula. wali mwingi katika migahawa utadhani kiporo cha siku 2.

mwisho; sehemu nyingi biashara zimedoda, sio tu chakula. jipe moyo
 
Jamani Wana JamiiForums nilitengeneza mgahawa wangu mzuri na Classic maeneo flani kwa ajili ya mapishi ya Supu, chapati, ugali, na wali.

Nikawa nauza vizuri tu siku ya kwanza hamna hata Chakula kimoja kilichobaki, yaani Saa 5 hamna supu Wala chapati mchana hivyohivyo.

Ila siku zilivyoenda kama wiki ya pili mambo yakabadilika, yaani kuanzia asubuhi mpaka jioni wanakuja watu wanne tu, hali ambayo sio ya kawaida hata kidogo mpaka nikafunga.

Nikaona ule ni Uchawi Live na wengine wakaniambia wanataka uhame uwaachie site😣, wengine wananiambia niendelee kumwaga mazagazaga ya kuvutia zaidi dah😓

Jamani kwa wazoefu sehemu zinazokuwa na mambo ya kishirikina kama hizi wenzetu mnafanyeje? Nisaidieni nirudi kwenye ofisi yangu.

Nilikuwa naitegemea, sina maisha bila pale na niliwekeza nguvu zangu zote nikiamini natoboa. Please msaada kwa mliowahi kumbana na watu wanaologa biashara zenu zife au kutaka kuwahamisha mni save niokoe ugali wangu🙏🙏
Kabla ya kufikiria kwamba Kuna watu/ mtu kakuloga chunguza kwanza huduma yako hasa mapishi,usafi namna ya kukaribisha wateja(kauri) nk.

Biashara ya chakula inahitaji umakini wa Hali ya juu. Pia angalia mgahawa wako umeuweka mazingira Gani, mfano mgahawa umezungukwa na mafundi ujenzi na wabeba zege, hao usiwawekee chakula kama unavyopakulia watu wa maofsini kesho hutopata mtu.

Kama mgahawa umeuweka mazingira ya watu wanaojielewa hakikisha usafi na ubora wa chakula ni wa Hali ya juu sana tofauti na hapo utashika sana watu uchawi. Yani mshua anashuka kwenye gari yake kuja kula wali unampakulia wali wa chenga chenga? Vinyama mchizi umejitenga na mafuta??........!

Mwisho: wateja uliowapata siku ya kwanza walikuja kuona kama unakitu Cha tofauti, wamegundua huna maajabu. Jichunguze then lekebisha utakuja kunishukru
 
Naona wengi wanakupa ushauri wa ki-chatGPT wakati hawajawahi kufanya biashara ya mgahawa. Wengine wanasema eti umefungua wakati wa mfungo hivyo hakuna biashara... hakuna wanalojua. Kwenye mfungo huwa kuna hela tamu sana kwa kuuza futari na daku.

Binafsi nimefanya biashara ya mgahawa jijini Dar tena pembeni ya barabara maarufu sio ndanindani. Hiyo hali iliyokutokea hata mimi ilinitokea. Mimi nilikaza nikafunga baada ya mwaka na nusu.

Siri kuu ya hiyo biashara ni kwa wewe mwenyewe mhusika kuwepo hapo tangu alfajiri hadi kufunga. Yaani unasimamia kinoko kila kitu. Mimi nilikuwa na biashara zingine hivyo nikawa sikai sana ndo ikawa changamoto. Kusimamia inamaanisha unahakikisha kuanzia usafi, ladha ya chakula na huduma kwa wateja ni ya hali ya juu. Usivumilie upuuzi wa mpishi au mtu mwingine yeyote.

Kuhusu uchawi fanya tu kama unaamini. Mimi sikufanya uchawi ila kwenye hiyo biashara kumejaa uchawi. Tafuta mganga konki.
bado unafanya hii biashara ili nikupe wazo ?
 
Back
Top Bottom