Mgahawa wangu mambo yalikuwa mazuri, ghafla imedoda, nifanye nini biashara irejee kwenye mstari?

Binafsi sehemu ninayoenda kula chakula napita migahawa karibu 6 ambayo Iko jirani yangu kabisa.
 
Kosa kubwa ulilofanya ni kufunga biashara, cha kufanya ungepunguza kiwango cha kupika kama ulikua unapika kilo 5 ungeshusha mpaka kilo 2 ukunikiendelea kushughulikia hiyo changamoto la tatizo la watejakupungua
 
Nataka nikuombee kazi hapo ukamsaidie kuuza chakula umwage tabasamu uwe mfano Kwa wengine
kama analipa vizuri,, mimi ni nani nikatae kazi jamani😇😇 hapo kwenye kuchekea wateja ndo penyewe kabisa,,, yaaan mpka wataanza kuhisi nawataka kumbe ni customer care yangu👌
 
kama analipa vizuri,, mimi ni nani nikatae kazi jamani😇😇 hapo kwenye kuchekea wateja ndo penyewe kabisa,,, yaaan mpka wataanza kuhisi nawataka kumbe ni customer care yangu👌
Basi nikuombee kazi Emirates airlines 🤣 siyo Kwa tabasamu Hilo 🤣
 
muhimu kwa sisi 'maafisa shibe' ni USAFI. hakuna atakayevumilia uchafu wa vyombo, mabaki, mhudumu na vyombo. pia joto la chakula. wali mwingi katika migahawa utadhani kiporo cha siku 2.

mwisho; sehemu nyingi biashara zimedoda, sio tu chakula. jipe moyo
 
Kabla ya kufikiria kwamba Kuna watu/ mtu kakuloga chunguza kwanza huduma yako hasa mapishi,usafi namna ya kukaribisha wateja(kauri) nk.

Biashara ya chakula inahitaji umakini wa Hali ya juu. Pia angalia mgahawa wako umeuweka mazingira Gani, mfano mgahawa umezungukwa na mafundi ujenzi na wabeba zege, hao usiwawekee chakula kama unavyopakulia watu wa maofsini kesho hutopata mtu.

Kama mgahawa umeuweka mazingira ya watu wanaojielewa hakikisha usafi na ubora wa chakula ni wa Hali ya juu sana tofauti na hapo utashika sana watu uchawi. Yani mshua anashuka kwenye gari yake kuja kula wali unampakulia wali wa chenga chenga? Vinyama mchizi umejitenga na mafuta??........!

Mwisho: wateja uliowapata siku ya kwanza walikuja kuona kama unakitu Cha tofauti, wamegundua huna maajabu. Jichunguze then lekebisha utakuja kunishukru
 
bado unafanya hii biashara ili nikupe wazo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…