Mganda kinara mgomo UDSM ni wa UVCCM

Mganda kinara mgomo UDSM ni wa UVCCM

Uliangalia kipima joto cha jana itv yule mzee aliwahimiza wanafunzi wagome nchi nzima kwa masilahi ya vizazi vijavyo wagome hata miaka 100 ili mradi maslahi yao yasikilizwe na yafanyiwe kazi
 
Hii serikali iache kukurupuka,mbona hoja itabadilika very soon na kumtaka JK na seriklai yake waachie mamlaka? Nikitaka kwenda kuhamasisha saa hizi nani wa kunizuia?
 
huyu mganda ni scapegoat,kikwete be a man,go in person to the campus and face these students.surely,surely this is where we miss kambarage
 
Hivi ukiwa Foreigner huruhusiwi kujiunga na chama cha siasa nchini?..
I mean kujiunga kama mwanachama na sio kiongozi.
 
Fidel88 huitaji kuwa mwana ccm kuwa na kadi ya CCM au jumuiya yake. Unaweza kupata popte kwa muda wowote. Kwa hiyo idea yako kuwa wangemkuta na kadi ya CHADEMA sijui ingekuwaje, haina maana hapa. Wangeweza kumchomekea pia. Nashangaa Mzee Mwanajiji unamshangaa shy kwa kusema hivyo. Nina wasi wasi na reasoning yako zaidi!

Muhimu hii kitu irudishwe kwao immediately. Inawavuruga vijaba wetu ambao wengi hawajui kwanini waligoma. Suala la mikopo ni issue ambayo si rahisi kama wanavyoona wengi kwenye hii post. Kuna mtu anasema Rais angekuja kuhutubia!? Strange ehh! Rais has a lot of things to handle bwana! Unataka kusema Rais akisikia Mgomo tu ajitoke kufafanunua? Kuna wastaafu na waalimu. Wanafunzi hawakuwa na sababu ya mgomo. Uelewa mdogo sana. Hii itathibitishwa very soon. Wataitwa kwa mafungu kukubali au kukaa udhamini wa serikali. Tuone atayekataa nani!

La msingi ni kujua kuwa ile Wizara sasa hivi na watu makini sana sana. Waziri na manaibu wake wawili. Isitoshe katibu mkuu ni bonge la mtendaji kuwahi kupatikana nchini. Tatizo students always ni toto tundu...

Nakumbuka enzi hizo, FOEs wakiamua mgomo, basi nyie huku wote kwanza mnaitwa NGWINI, then lazima mkubaliane! Jaribu kukataa uone! Then in three weeks or one month, wote mnaitwa chuo. Injinias wa kwanza kuingia kwa kunyata kama panya.......
 
•
Odong Odwar awagawa Chuo Kikuu

Similar Stories
• Moto wazua tafrani Chuo Kikuu Muhimbili 21.11.2008 [More]
• Makerere kufukuza wahadhiri wanaogoma 14.02.2008 [More]
• Wanafunzi Chuo Kikuu wagoma 18.02.2008 [More]

Na Said Mwishehe

SIKU moja baada ya Serikali kumfukuza nchini mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam raia wa
Uganda Odong Odwar, wanafunzi wa chuo hicho wamegawanyika huku wengi wao wakipinga hatua hiyo na
kumwita shujaa na mtetezi wao.

Wakizungumza na gazeti hili leo asubuhi kwa njia ya simu baadhi wanafunzi wa chuo hicho ambao
kwa sasa wametimuliwa na baadhi wakikutana katika vikao mitaani kujadili hatma yao na kitendo
cha kufukuzwa Odwar ambapo amedai alikuwa mwanafunzi halali na hatua iliyochukuliwa dhidi yake
ni kumwonea kutokana na msimamo wake kupinga uonevu na sera potofu.

Waldai serikali ina ajenda binafsi ndio maana imeamua kumfukuza Odwar na kusisitiza wao
wataendelea kupinga kufukuzwa kwa mwanafunzi huyo hasa katika kipindi hiki cha kushunikiza
mabadiliko katika Sera ya uchangiaji elimu ya juu.

Mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazeti
alisema Odwar ni mwanafunzi kama wengine wa vyuo vikuu hivyo alikuwa na haki ya kushiriki katika

mgomo ili kupigania haki za wanafunzi wenzake hata kama yeye si Mtanzania.

"Serikali haikuanza kumfuatilia Odwar katika suala la mgomo tu bali imekuwa ikimwandama kitambo

sasa wameona njia pekee ya kumkomoa ni kumrudisha kwao Uganda kwa madai ya kuishi nchini

isivyo halali, hii imechangiwa na msimamo wake wa kuonekana kinara wa migomo.Kwetu Odwar ni

shujaa na mtetezi ambaye amekuwa akitusaidia kama mwenzetu kupigania haki zetu.

Alisema hata wakati wa kuchagua viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es

Salaam(DARUSO) Odwar alionekana kipenzi cha wengi na angeshinda kwa kishindo nafasi ya urais

lakini aliwekewa zengwe na alishindwa kugombea.


Mwanafunzi mwingine aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina pia, alisema

wanachotaka ni kuona mwanafunzi huyo anarudi nchini kuendelea na masomo yake hasa katika kipindi

hiki ambacho nchi za Afrika Mashariki zipo katika harakati za kuleta ushirikiano katika mambo

mbalimbali.

"Tunachotaka sisi Odwar arudi chuo hakuna sababu kumfukuza ni mwanafunzi halali chuoni hapo na

kama kugoma hakuwa peke yake.Kwa sasa kitu ambacho kinaonekana hapa ni kwamba serikali imeamua

kumtoa kafara kwa kuwa si Mtanzania,"alisema.

Naibu Kamishina wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Peter Kivuyo alikaririwa akisema taarifa

walizotapa ni kwamba mwanafunzi huyo amekataliwa nchini kwao Uganda kutokana na sababu

mbalimbali ikiwemo ya kutakiwa kuonesha kibali cha kosa alilofanya hadi akatimuliwa chuoni.

Tangu kuanza kwa mgomo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kufuatiwa na vyuo vikuu vingine nchini

serikali imekuwa ikifanya uchunguzi kubaini vinara wa migomo hiyo.

Wakati huo huo serikali imetoa masharti magumu kwa wanafunzi ambao wapo tayari kurudi chuoni

ambapo sharti kubwa ni kwamba atakayekubali kurudi chuoni lazima akubaliane na sera ya sasa ya

uchangiaji wa elimu ya juu.

%%%%%%%%%%%%%%%%%
 
Jamani nauliza tena ni kosa kuwa mwanachama wa chama cha siasa ukiwa sio raia?.. Mbona huko nje wanakofungua matawi ya chama wengi wanachama wao ni raia wa nchi hizo!
 
mwanjelwa,mayb reasoning should also start at home!! ishu sio Kikwete kwenda kuwaona vijana kila siku,but kama una uelewa maana ya state university,ungeona umuhimu wa kumshauri rais aende kuongea na vijana at least mara moja kwa mwaka...
 
Jamani nauliza tena ni kosa kuwa mwanachama wa chama cha siasa ukiwa sio raia?.. Mbona huko nje wanakofungua matawi ya chama wengi wanachama wao ni raia wa nchi hizo!

Principally, and possibly legally, huruhusiwi. Katika nchi nyingi wakazi ambao sio raia, japokuwa wanaweza kuruhusiwa kupiga kura, hawaruhusiwe kisheria kuwa wanachama wa vyama vya siasa katika nchi hiyo.
 
Mimi na shindwa kuelewa kabisa...hii migomo imeanza lini na huyu mganda amekuja lini hapa tz? nimechoka kwa kweli!
 
Kitla Mkubwo,
Basi ajabu kubwa hapa kwetu mkazi anaweza kuwa mwanachama wa chochote chama cha siasa lakini haruhusiwi kupiga kura.. Ni raia pekee anayeruhusiwa kupiga kura ama kugombea kiti cha uongozi..
 
Ebwana Mwanjelwa, mimi natofautiana na wewe kabisa kutokana na sababu zifuatazo:-
a) kitendo cha kugoma vyuo vikuu vyote si jambo dogo, hivyo Rais anaweza kuingilia kati inawaje si kwa kutoa hotuba tu bali kutoa maagizo gazi husika.

b) kwamba wanafunzi wanagoma bila kujua sababu sikubaliani nawe. Naona umeamua kuwashusha sana. Hata sisi enzi zetu tulisoma hapo na tuligoma mara nyingi tu na tulipo fukuzwa tulienda kuwaeleza wazazi sababu zetu za kugoma. Wanafunzi wa vyuo vikuu sii mambumbu, ni cream ya taifa tena ni chini ya 1% ya wale waliomaliza darasa la saba katika mwaka wao. Na kama kweli hawajui sababu za kugoma na wanagoma basi hakuna sababu ya kuwapa degree.

c) Ninashaka hujasoma ripoti ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ya Juu Sanyansi
na Teknolojia juu ya migomo na vurugu vyuoni ya mwaka 2004.(Mwanakijiji ameiambatanisha kwenye thread hii.

d) Pia kama umezingatia taarifa ya naibu Waziri wa Elimu amekiri upungufu au au makosa yanayofanywa na bodi ya mikopo katika zoezi zima la means testing. Jamaa wapo pale kukadiria tu bila kuwa na formula zinaoeleweka.

e) Wanafunzi wametoa takwimu kwamba toka ianze sera ya uchangiaji, matokeo ya mitihani yamekuwa mabaya kuliko hapo awali. Sasa kama hiyo sera inapunguza ubora wa elimu kwanini wasigome? Kwa mfano Chuo Kikuu cha Dar es salaam inawezekana kikawa ndo chuo pekee mwanafunzi anapata degree bila kununua kitabu hata kimoja.

f) Kwa mujibu wa baadhi ya wanafunzi na wahadhiri, kuna idadi kubwa ya wanafunzi wa UDSM na ARU hawajapata matokeo ya mwaka wa masomo uliopita kwa kukosa kulipa ada. Pia wanafunzi wa mwaka wa kwanza wengi bado hawajasajiliwa (12,000 kati 18,000) kwa kukosa ada. wapo chuoni kwasababu ya admission tu.

sasa ni nani ambaye haoni kwamba haya ni matatizo? Wale wanaoendeleza hoja kwamba wanafunzi hawajui sababu ya kugoma wanasimamia wapi?
 
Hapo ndo unaona udhaifu wa serikali yetu,siku zote tunajidanganya tunatibu ugonjwa wakati hata chanzo chake hatujui! Ati last mgonjwa wa kansa tunampa panadol! Toka migomo imeanza wanachoweza kutueleza ni kumrudisha huyp mganda kwao! Na mbona kwenye vyuo vingine hawatuambii nini kinaendelea wamebaki pale Mlimani tuu! Au ni chambo ili serikali ionekane inawajibika?
 
Na je baada ya kumkamata kinara wa migomo ndo kusema migomo imekwisha/itakwisha?
 
Na je baada ya kumkamata kinara wa migomo ndo kusema migomo imekwisha/itakwisha?

Mkuu Calnde
Migomo haiwezi kwisha. Mgomo ni mfumo wa maisha ya watu wanaouhitaji ili kupinga mfumo fulani kwa kusimamamisha kutoa nguvukazi yao...

Ila sijui ingekuwaje kama Odwar angekuwa Mtanzania na amefanya haya tunayoripotiwa kuyafanya pale Makerere, mzee wa pama angemfanya nini? Bado najaribu kupata picha
 
Mkuu Calnde
Migomo haiwezi kwisha. Mgomo ni mfumo wa maisha ya watu wanaouhitaji ili kupinga mfumo fulani kwa kusimamamisha kutoa nguvukazi yao...

Ila sijui ingekuwaje kama Odwar angekuwa Mtanzania na amefanya haya tunayoripotiwa kuyafanya pale Makerere, mzee wa pama angemfanya nini? Bado najaribu kupata picha

Kama si suluhisho then waache kupayuka payuka ovyo. they have to come up with good conclusion!

Kuna tetesi kuwa hata kwao hapatani na mkuu wa kaya yao!Wanadai kuna uwezekano jamaa akawa anahusiana na LRA. Wenye details zaidi wanaweza kutupa!
 
Yote hayo pia hutegemea upeo wa raisi na watu wake wa karibu katika mambo hayo raisi mwenyewe alikuwa ni waziri wa mambo ya nje karibu maisha yake yote unategemea leo hii aje kufanya mapinduzi ??
 
sioni shida kuwa na kadi ya CCM hata kama wewe ni mgeni, katiba ya UVCCM inasema lazima mwanachama wake awe raia wa TZ? Matawi yanayofunguliwa London na sehemu zingine duniani yamejaza watu wasio raia wa TZ kwani walishaukana uraia siku nyingi hata passport zao walishachana. Sasa shida ipo wapi kuwa Mshabiki wa Manchester United wakati unaishi Dar? na kuwa Mshabiki wa Democrat na Obama wakati Upo Nakuru, au kuwa mwanachama wa CCM wakati Upo SINZA, sioni utofauti. Kijana wa watu ameonewa!!!
 
Imagine situation ambayo, wanafunzi wataweza kuwashawishi walimu kuunganisha ajenda, na baadaye kundi hili liombe kanyongeza ka waastafu wa africa mashariki kwa ajili ya strategy, na baadaye waamue kuwashawishi watanzania wote waliopo kwenye Public sector kugoma kazi kwa siku tatu mfululizo (serikali haita-react of course) Then waitishe mgomo Mkubwa zaidi utakaowajumuisha wakulima, sasa wakasema tunaandama kwa sababu hatuna Imani na serikali. (FFU na JWTZ Tafadhari msiwe kimbele mbele). hapo ni diplomacy tu,

Nashangaa hawa Viongozi wetu wamewashindwa hata Mr. Ziro alipokuwa waziri mkuu mwaka 2000 aliweza kuzungumza na wanafunzi na kufikia muafaka, upo wapi uzeofu wa Pinda mzee wa usalama mika kibao? amekulia Ikulu Pinda walisema toka enzi za mwalimu, anajua serikali zote, Upo wapi ukijana wa Ngereja? Upo wapi utoto wa mjini wa Makamba? wote wamefeli???
 
Back
Top Bottom