Mganga wa kienyeji ahukumiwa miaka 20 jela na viboko 12 kwa kosa la kufuga fisi.

Mganga wa kienyeji ahukumiwa miaka 20 jela na viboko 12 kwa kosa la kufuga fisi.

Hapo sio kwamba wamejisumbua tu😁
Watakuwa wanashinda na kulala na limnyama gerezani.
 
Kama ukoo tupo kujiandaa kukata rufaa
mjomba wangu haiwezekani aende jela kwa kosa dogo kama hilo
Ntunzu huku tunajipanga kwa mashambulizi kwa hakim na mahakama kwa ujumla!
 
Kama ukoo tupo kujiandaa kukata rufaa
mjomba wangu haiwezekani aende jela kwa kosa dogo kama hilo
Ntunzu huku tunajipanga kwa mashambulizi kwa hakim na mahakama kwa ujumla!
Nguvu yenu lazima waitambue, nyie ba kokaya fanyeni jambo nchi nzima itetemeke 😂 😂
 
Mnafunga mganga wa kienyeji jela, akienda kugeuka kinyamkera huko jela si atawawasumbua askari jela na wafungwa, nani atamgusa mchawi huyo?
Ngoja tuone itakavyokua, ila serikali haiamini kwenye uchawi 🫠
 
Hivi kwa nini sheria za Tanzania ni za uonevu sana. Yaani kufuga fisi miaka ishirini jela?

Hizi sheria lengo lake ni kufundisha au kukomoana?
Ni kwa sababu tulirithi mfumo wa haki jinai wa kikoloni, ambao ulilenga kuwakomoa watawaliwa. Tulipopata uhuru watawala wapya wakafanya mageuzi kwenye mambo mengine yaliyowapa faida wao kiutawala, yale mabaya ya kikoloni yaliyosaidia kutawala kwa urahisi kama sheria mbovu na matumizi mabaya ya vyombo vya dola hayakupewa kipaumbele kufanyiwa mageuzi
 
Nani anaikumbuka hii kesi ya yule mganga wa kienyeji aliyekamatwa na fisi? amehukumiwa leo.

View attachment 3267716

Mahakama ya Wilaya Bariadi mkoani Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela pamoja na kuchapwa viboko 12 Emmanuel John (31), maarufu kama Chief wa Kilulu, kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali aina ya fisi akiwa hai na akiishi naye nyumbani kwake.

Mshtakiwa huyo, ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kilulu kilichopo kata ya Bunhamala, wilayani Bariadi, na mganga wa kienyeji, alipewa adhabu hiyo katika kesi namba 2458/2025 iliyokuwa ikimkabili kwenye mahakama hiyo.

Awali, akisoma kosa la mshtakiwa, Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mashtaka Mkoa, Lupiana Mahenge, alieleza mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa na nyara ya serikali, fisi akiwa hai, akimfuga nyumbani kwake kinyume cha sheria.

Mtuhumiwa aliishi na fisi huyo kama mnyama wa kufuga kinyume na kifungu cha 86 (1) na kifungu kidogo cha (2)(C)(III) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori sura ya 283, kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliomba mahakama imsamehe kwa kuwa anategemewa na familia ya watoto wanne, wakiwemo mapacha, ndipo hakimu akatoa adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela na viboko 12 ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine.
Mbona kuna chama cha siasa pia kinafuga fisi

1741781337438.png
 
Back
Top Bottom