Mganga wa kienyeji atapeliwa Mbeya, aenda kulalamika kwa mkuu wa mkoa

Mganga wa kienyeji atapeliwa Mbeya, aenda kulalamika kwa mkuu wa mkoa

Katika hali isiyo ya kawaida Mganga wa kienyeji Edward Mwansasu mkazi wa Kijiji Cha Ndubi Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya, amefika mbele ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya kulalamika juu ya kutapeliwa na mteje wake aliye mhudumia kwa kumpa dawa za biashara.

Mganga huyo amefika mbele ya mkuu wa Mkoa wakati akisikiliza kero za wananchi Wilayani humo akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali na kusikiliza kero za wananchi ambapo mbali na hilo amelalamikia hatua ya wazee na walemavu katika Kijiji cha Ndubi kutopata misaada inayo tolewa na serikali ikiwemo vyerehani na fedha za tasaf.

Akijibu malalamiko hayo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera ameelekeza wataalamu kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, kufika katika Kijiji hicho Ili kuangalia namna ya kuwawezesha walemavu na wazee.

#WasafiDigital
Mshana Jr hii imekaaje mkuu
 
Mshana Jr hii imekaaje mkuu
Baadhi ya matapeli na waganga wa jadi ni watu wenye IQ ya hali ya juu sana.. Wakishausoma mchezo mzima ni rahisi kumpanga mtu akapangika
Kwa mfano kama jamaa alitaka kumtapeli mganga milion 5 alihakikisha anatumia laki 5 mpaka milion kumuweka sawa mganga
Nitaendelea

Kwahiyo jamaa atajifanya ana matatizo sana na anamwamini sana mganga.. Hivyo atatibiwa kwa siku kadhaa na kila akienda kupata tiba atjifanya anapona kwa haraka na anapokea siku za madili makubwa makubwa .. Na mwisho wa matibabu anampa mganga kifurushi cha mazagazaga ya zawadi na shekeli

Baada ya siku mbili tatu anarudi kumshawishi mganga ajiunge kwenye dili ya pesa ndefu anajifanya kawekeza pesa yenye faida ya maana na kumshawishi mganga naye afanye hivyo

Mganga akiwa tayari keshajenga imani kubwa kwa mteja wake anakabidhi fungu na huo ndio unakuwa mwisho wa story[emoji1787]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom