Mgao ujao wa umeme…

Hapa umeandika bila uhalisia....bali ni chuki binafsi kwa Hayati.

Tatizo hapa ni sababu za mgao wa umeme....

Mara ya kwanza ilikuwa ni ukame...

Sasa hivi ni matengenezo.


Cha ajabu huo mgao wenyewe unaweza usionekane kwasababu umeme unakatwa kila siku karibu mara 10....

Ni jambo la ajabu sana nchi yenye miaka sitini ya uhuru kuwa na mgao wa umeme....

Shida zingine ni za muhimu sana....umeme matumizi yake ni makubwa mno hasa kwa nchi zinazotaka kuendelea...

Kwenye serikali hii ya SAMIA inakosa mtu mwenye huruma na wananchi....
 
Sina chuki kwa JPM, alipokuwa hai nilikuwa ni mmoja wa waliomuunga mkono kwa dhati kabisa. Alipofariki nikajifunza mengi kuhusiana na aina ya watu wake wa karibu na mienendo yao, ninapotoa maoni kumhusu ninajitahidi sana nimtendee haki.

Umeme wa Tanzania umeingizwa na siasa ukizingatia nishati hii ni pesa tupu. Hivyo wapigaji wakubwa wanaingiza mikono yao katika masuala yanayogusa maisha ya nchi.

Mama kazunguka kuitangaza nchi kimataifa hivyo alipaswa kufahamu muunganiko unaokuwepo kati ya uwekezaji mpana na uwepo wa nishati ya uhakika. Ni wizara nyeti sana lakini makundi ndani ya CCM yanaifanya ionekane kama vile ni wizara isiyoweza kuongozwa ikaongozeka.
 
Wenye Tanzania na CCM walisharudi; wewe ulikuwa hujui hilo? Siku hizi nchi inakwenda kwa maneno na ahadi lukuki huku matendo yakiwa zero.
 
Imebaki siku moja!

Ila baadhi ya watu wanadai tayari mgao ushaanza na wengine wanasema kuwa mgao umekuwepo kwa muda sasa!

🖕
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…