The Eye
JF-Expert Member
- Oct 29, 2020
- 278
- 393
Hapa umeandika bila uhalisia....bali ni chuki binafsi kwa Hayati.Kivuli cha JPM ndio kipimo cha urais wa Samia. Marehemu aliwazoeza watu vibaya kwa kuwahakikishia ufanisi unaotokana na upendo hata kama ni kwa gharama za kutokuwa mkweli.
Wake ukawa ni uongozi unaofanana na mshumaa, unawawakia watu kwa gharama ya wenyewe kuteketea. JPM alikuwa ni POPULIST LEADER, Alisikiliza shida za wengi na akataka aonekane anao uwezo wa kutatua kila tatizo, kumbe utatuzi mwingine ukiambatana na ukweli ni bora zaidi kwa serikali yake na kwa mwananchi.
Tatizo hapa ni sababu za mgao wa umeme....
Mara ya kwanza ilikuwa ni ukame...
Sasa hivi ni matengenezo.
Cha ajabu huo mgao wenyewe unaweza usionekane kwasababu umeme unakatwa kila siku karibu mara 10....
Ni jambo la ajabu sana nchi yenye miaka sitini ya uhuru kuwa na mgao wa umeme....
Shida zingine ni za muhimu sana....umeme matumizi yake ni makubwa mno hasa kwa nchi zinazotaka kuendelea...
Kwenye serikali hii ya SAMIA inakosa mtu mwenye huruma na wananchi....