Mgao ujao wa umeme…

Mgao ujao wa umeme…

Inadaiwa mgao wa umeme unakuja. Inadaiwa unaanza tarehe 1 mwezi ujao wa Februari.

Sababu ya huo mgao eti ni matengenezo ya mitambo yao ya wapi wapi huko sijui…

Sasa kwa akili zangu hizi za kidato cha nne, ni kama vile sielewi elewi.

Mbona nchi zingine huwa hakuna migao inayosababishwa na matengenezo ya mitambo ya umeme?

Au zipo? Kama zipo, basi sawa. Ila kwa nchi nizijuazo mimi, kamwe hata mara moja sijawahi sikia eti kutakuwepo na mgao au migao ya umeme kwa sababu mitambo ya kuzalisha au kusambaza umeme inafanyiwa ukarabati.

Hao wenzetu wao mitambo yao huwa haihitaji ukarabati? Kama huwa inahitaji ukarabati, wanawezaje kuepuka migao ya umeme?

Kwa nini sisi kila mitambo inapohitaji ukarabati [ kama ni kweli inahitaji huo ukarabati] basi kunakuwepo na mgao?

Manake hili si jambo geni. Limekuwepo siku zote. Sasa miaka yote hii hawa watu hawajaweza tu kubuni namna ya kuikarabati hiyo mitambo bila kuleta usumbufu wa migao?

Tanesco….and whoever else involved….seriously????

NB: Halafu nani anaamini huu mgao utakuwa ni wa siku 10 tu????? Mimi siamini….
Hama Nchi Kama vipi, unataka TANESCO wasifanye maintenance ya mitambo ya umeme? Hata hiyo gari Kuna muda unaisimamisha kazi unaifanyia service!
Nyie wasukuma vipi,mmerogwa au
 
Hiyo mitambo haikufanyiwa marekebisho kwa muda mrefu sababu wahusika waliogopa kutumbuliwa (hili waziri alishasema)

Sababu za mgao ni kufanya ukarabati na bila kufanya huo ukarabati kipindi hiki huenda hata huo umeme wa mgao usiwepo.....hivyo Watanzania ondoeni wasiwasi kwani hayo matengenezo ni muhimu kipindi hiki.
sawa
 
Nafikiri kwa muda mrefu Tanesco wamekuwa wakiendesha hiyo mitambo bila periodic maintenance kwa kuhofia kuonekana saboteurs baada ya serikali kuahidi hamna mgao. Now the chickens have come home to roost maana wakizidi kuiendesha ita collapse kabisa. Hawana jinsi bali wafanye the long over due maintenance.

Amandla...
mmmh kwahiyo nchi zingine huwa wao wajinga wapokuwaga na backup wakati wa matengenezo?
 
Nipo hoves sana jmn na suala la Umeme,na waziri wake ... hii inji hiii
 
Ilikuwepo japo na watumiaji walikuwa wachache..
Watumiaji wakiwa wachache na Tanesco inapata mapato kidogo, lakini watumiaji wakiongezeka wakawa wengi na Tanesco wanapata mapato makubwa zaidi na zaidi !! Kwahiyo hiyo kuongezeka kwa watumiaji sio justification ya umeme kuzidiwa Bali ni kutowajibika kwa wanaohusika kwa sababu wanazozijua wao !! Labda mifuko ya sandarusi !!"
 
Hajui afanye nini!
Wacha kumsingizia, kama alikuwa anahamahama utotoni na kusoma shule kumi kwa miaka 7 unategemea nini? Yupo njiani kuwa raisi wa nchi nyingine ya kusadikika wakati wowote.
 
Kitu chochote ili kimudu kinahitaji regular service/maintenance. Na unatakiwa uwe na source nyingine ya umeme. Kwa wenzetu wanafanya service inspotakiwa, na wakati mitambo inapofanyiwa service wananunua mahitaji yao kwa wenye surplus. Tungekuwa tumeunganisha na wa msumbiji au Zambia au Kenya wakati huu ndio tungenunua kutoka kwao.
Mimi siwaelewi watu wanaoshangaa. Mara ngapi tunaambiwa kuns sehemu hazitapata maji wiki nzima kwa sababu tunafanya service mitambo ya Ruvu Juu au Chini! Huko ulikoishi uliwahi kusikia metropolis kama Dar ina kosa maji wiki nzima kwa sababu yeyote?
Hatupaki majumba yetu, tunashindwa kufanyiq service vyo vya maofisini, madirisha yakivunjika hatuweki maji, paa zinavuja, mitaro hatuzibui mpaka mvua ifike, magari ya serikali yanashindwa kubadilisha matairi , barabara kila kukicha tunajenga upya kwa sababu tulishindwa kuziba potholes, halafu tunajifanya kushangaa kwamba Tanesco walikuwa wanaburuza mitambo bila kuifanyia service! Sisi kweli watu wa ajabu.

Amandla....
Kufanyia ukarabati mitambo au sijui mabomba ya gesi or whatever, bila kuleta mgao, inawezekana kabisa.

Ni upumbavu wetu tu.
 
We are stupid.

Kufanyia ukarabati mitambo au sijui mabomba ya gesi or whatever, bila kuleta mgao, inawezekana kabisa.

Ni upumbavu wetu tu.
Kwanza hata kabla tu yakutangaza kutakuwa na mgawo umeme ulikuwa unakatika na hapo kumbuka wametoka kufanya wanayoita matengenezo na hapo tunajiuliza hayo matengenezo waliofanya ni yapi ikiwa still umeme unakatika Mara Jana wanatoa taarifa yakutangaza kutakuwa na mgawo kwasababu ile ile waliohitaja wananchi Wana doubt hata wakifanya hayo matengenezo kuna uhakika gani umeme hautakatika? Ikiwa mwanzo pia walisema hivyo hivyo na umeme ukawa unakatika Hili ndio swali walitakiwa watujibu
 
Na kwanini hilo zoezi liwe la nchi nzima?
Hata sielewi maana kabla ya hapo hili zoezi lilikuwa limekwishaanza kuna maeneo umeme ulikuwa ukikatika na jibu likawa ni kwa sababu ya matengenezo.
 
Inadaiwa mgao wa umeme unakuja. Inadaiwa unaanza tarehe 1 mwezi ujao wa Februari.

Sababu ya huo mgao eti ni matengenezo ya mitambo yao ya wapi wapi huko sijui…

Sasa kwa akili zangu hizi za kidato cha nne, ni kama vile sielewi elewi.

Mbona nchi zingine huwa hakuna migao inayosababishwa na matengenezo ya mitambo ya umeme?

Au zipo? Kama zipo, basi sawa. Ila kwa nchi nizijuazo mimi, kamwe hata mara moja sijawahi sikia eti kutakuwepo na mgao au migao ya umeme kwa sababu mitambo ya kuzalisha au kusambaza umeme inafanyiwa ukarabati.

Hao wenzetu wao mitambo yao huwa haihitaji ukarabati? Kama huwa inahitaji ukarabati, wanawezaje kuepuka migao ya umeme?

Kwa nini sisi kila mitambo inapohitaji ukarabati [ kama ni kweli inahitaji huo ukarabati] basi kunakuwepo na mgao?

Manake hili si jambo geni. Limekuwepo siku zote. Sasa miaka yote hii hawa watu hawajaweza tu kubuni namna ya kuikarabati hiyo mitambo bila kuleta usumbufu wa migao?

Tanesco….and whoever else involved….seriously????

NB: Halafu nani anaamini huu mgao utakuwa ni wa siku 10 tu????? Mimi siamini….
Wanatengeneza mazingira ya kupiga hela maana walianz na sababu za ukame tukawa na mgao na ss wamekuja na sababu zingine CCm ni janga la kitaifa
 
Back
Top Bottom