Mgao wa Umeme Tanzania Nzima, Kisa cha Engine ya Dizeli na Mradi Wa Stigler's HEP, matrilioni yetu Tumepigwa tena?

Siwezi kukubishia mkuu, maana sijui unalizungumzia katika engo gani. Lakini ukisema vinalingana, lazima mtu akukodolee mijicho kwa mshangao.
Elimu iko mkononi bwashee ndio sababu Mbowe na Sugu Wana maarifa kupita Lipumba japo waliishia form four πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ”₯
 
Hii nchi wapumbavu ni wengi sana. Lakini tusishangae, hawa viongozi tumesoma nao na kufanya nao kazi tunazijua akili zao. Miaka mitano, sita ... tu iliyopita tulikuwa tumesahau kukatika katika umeme lakini sasa imebaki kawaida.
 
Tatizo mindset ya Watanzania.

Hata wewe mwenyewe badala ya kutafuta ufumbuzi endelevu wa tatizo, umetafuta shortcut ya kumpachika mtu mmoja atutatulie tatizo.

Huyo mtu mmoja akifa je, utafanya nini?
 
Wazo langu ni kwamba badala ya kuhangaika na njia ndefu ya kumtafuta mwekezaji, halafu tupambane kuwaondoa mchwa ili tummilikishe yeye, kwa nini tusipambane tu kuwaondoa mchwa hao kisha tukajimilikisha wenyewe nchi yetu?
Tukodishe nchi?πŸ˜πŸ˜†
 
Tatizo mindset ya Watanzania.

Hata wewe mwenyewe badala ya kutafuta ufumbuzi endelevu wa tatizo, umetafuta shortcut ya kumpachika mtu mmoja atutatulie tatizo.

Huyo mtu mmoja akifa je, utafanya nini?
There is always some one to lead, mkuu hata kwa wezi kuna mwizi mkuu ambaye ana authority ya kuamua waibe wapi kwa nani. Hata kama wanaiba wote
 
Kuweni na uzaendo kwa nchi yenu. Mambo kama hayo siyo kuyaanika mitandaoni kwani nchi jirani zikiona zitatudharau. Mambo kama haya tuwe tunalalamika kwa kupigiana simu au kwenye magrupu ya kitanzania au kuwatumia ujumbe wakuu wa wilaya na mikoa

Waambie wale wanaokula kwa urefu wa Kamba zao wawe Wazalendo .... Haya makelele yote wala hutayasikia.
 
There is always some one to lead, mkuu hata kwa wezi kuna mwizi mkuu ambaye ana authority ya kuamua waibe wapi kwa nani. Hata kama wanaiba wote
Hata hawa viongozi wa sasa walikoanzia ni kuaminiwa na wananchi waongoze.

Huyo Tundu Lissu uliyemtaja, siku moja nilikuwa naongea naye.

Nikamuuliza swali.

Nikamwambia, nilikuwa nasoma kitabu cha maisha ya Mario Vargas Llosa, muandishi mshindi wa nishani ya Nobel ya Literature ya 1990, kutoka Peru, ambaye alienda kuingia kwenye siasa za nchini kwake Peru. Kitabu kinaitwa "A Fish Out of Water".

Katika kitabu cha maisha yake Mario Vargas Llosa, ambaye kimsingi alikuwa muandishi na si mwanasiasa, ila aliingizwa tu katika kinyang'anyiro cha kugombea urais kutokana na umaarufu wake kama muandishi, aliandika kuwa, wanasiasa wana maneno mengi sana, watakuambia wanavyotaka kukomboa wananchi na wanavyotaka haki za binadamu na kupandisha uchumi na mambo kedekede, lakini, siasa unayoisoma kwenye magazeti na kuisikia redioni na kuisikia kwenye mijadala ni tofauti sana na realpolitik, siasa yenyewe inayoendelea ndani ya vyumba vilivyofungwa milango huko.

Huko nyuma ya pazia, walioshika madaraka wana nia moja tu, kuendelea kushika madaraka, na wanaotafuta madaraka wana nia moja tu, kupata madaraka, habari nyingine zote ni geresha tu.

Baada ya kumpa nukuu hiyo Tundu Lissu, nikamuuliza, sasa, kwa kuzingatia alichosema Mario Vargas Llosa, tunaelewa CHADEMA na wewe hususan umefanya kazi kubwa sana na nzuri, tukikupa madaraka, tutahakikishaje kuwa hutaenda kutugeuka baada ya kupata madaraka?

Tundu Lissu alijibu kwa kusisitiza wananchi kujikita katika mabadiliko ya kimfumo na kuacha kuangalia watu, mabadiliko ya kimfumo ambayo yatamlazimisha kiongozi yeyote afanye mambo wanavyotaka wananchi, apende asipende. Na zaidi, alisistiza kuwa suala la kuongoza nchi ni suala shirikishi, wasiachiwe viongozi tu, viongozi wanahitaji kupewa feedback na hata kuwa ctiticized.

Nachelea tunawa lionize sana viongozi na kuwaachia wao ndio watuletee maendeleo.

Hili ni tatizo ambalo limetengeneza uongozi mbovu tulionao sasa.

Tunatakiwa kulirekebisha.
 
Nikirusi kipo katika mfumo kuanzia juu hadi chini! Hii nchi ni katiba na kwambia mafisadi watanyoka!
 
Toa habari inayoeleweka. Sio kila mtu anajua unachowaza akilini
 
Bwawa la Nyerere linatoa suluhisho la mahitaji yetu ya umeme kwa sasa. Hakuna excuse. Maji yalijaa mpaka kumwagika, ili waongo wajitenge na wakweli.
Nina mashaka kama tumeandaa miundombinu sahihi ya kuutoa huo umeme na kuunganisha kwenye grid ya Taifa. Maana hata hatuelewi nini kinaendelea
 
Huko nyuma ya oazia, walioshika madaraka wana nia moja tu, kuendelea kushika madaraka, na wanaitafuta madaraka wanannia moja tu, kupata madaraka, habari nyingine zote ni geresha tu.
Hapa umenipa ukweli umeniuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…