Mgao wa umeme unaivua nguo Serikali

Mgao wa umeme unaivua nguo Serikali

Mvua zilinyesha chini ya kiwango mtela bwawa halikujaa ipasavyo hata aje nani kama mabwawa maji hayatoshi mgao utazidi kuwepo tu



Mbona Magufuli kuna namna alifanya tukaendelea kupata huduma ya umeme na maji?

Rais anatakiwa limkoseshe usingizi mpaka ufumbuzi upatikane wa haraka.

Anatakiwa aende huko maporomoko, Akutane na hiyo team ya jopo la Umeme na maji

Waje na suluhisho mbadala haraka.
 
Hakuna haja ya salamu.

Unajua kuna vitu unaweza kupiga siasa, ukapiga porojo, ukatia nakshi nakshi, ukatetea nk na watu wakakuelewa. Ila inapokuja kwenye vitu ambavyo vinaonekana wazi na vinaathiri maisha ya watu MOJA KWA MOJA kunakua hakuna kiasi cha porojo, siasa, mbwembwe wala maneno matamu yanayosaidia!

Hivi ina maana nchi nzima hii ya Tanzania yenye Rais, Makamu wa rais wawili, Waziri mkuu, mawaziri, wabunge, maprofesa, mainjinia, wataalam, vyanzo vya maji vya kila aina, upepo, jua, gesi, nk yaani imeshindikana kabisa kwa miaka 60 sasa kuwa na umeme wa uhakika?

Hivi tuna kipi cha kujitetea, tuna maneno gani ya kuongea, tuna porojo zipi za kupiga kuonyesha ni sababu gani imepelekea mpaka leo hii nchi inaingia gizani? Na bila AIBU tanesco inatoa ratiba ya mgao wa umeme, as if ni kitu cha kawaida tu wala hakuna tatizo lolote.
Bado natafuta mwalimu wa kufundisha courses za computer kama vile word excel PowerPoint publisher adobe acrobat chatgpt windows operating system etc.kama una hiyo skillset usisite kunicheki pm.
 
Biashara ya majenereta, Sola panels, battery etc.

Lazima mgao uwepo ili biashara za wakubwa zifanyike. Kusipokuwepo mgao wa Umeme: majenereta, Sola panels na battery watamuuzia Nani? [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Tatizo la Mgao wa umeme Tanzania ni lakutengenezwa. Namsifu sana MH Magufuli kwenye Utawala wake Aliwadhibiti sana Watengeneza Mgao wa Umeme.

Nakumbuka Alisema Kulikua na watu wanafungua maji kwenye bwawa la Mtera ili maji yapungue wapate Uhalai wa kusema maji yamepungua kwenye mabwawa ya kuzalisha Umeme ili wauze Majenereta yao.

Na ukweli kuna watu walifukuzwa pale tanesko na wote ni mashahidi kwa miaka 6 Ya utawala wake hakukuwa na Mgao wa Umeme.

Sasa Mama yetu Anawaamini sana wataalam wa tanesko bila kuwa na Uchunguzi wa Menejimenti nzima ya Tanesco.
Mkuu ubora wa utendaji huanzia juu..chini ni mapokeo tu..juu kukiwa ziro chini haiwezi kuwa tano.

Hata siku moja tanzania usitegemee perfomance kutokea chini kama juu kumeoza.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
E bana ee... kwahiyo upungufu wa maji unapelekea tatizo la umeme na upungufu wa umeme unapelekea tatizo la maji..! Hii nchi hii..🙆‍♀️
Bado safari ni ndefu.
 
Back
Top Bottom