Mr-Njombe
Member
- Aug 29, 2022
- 64
- 122
Mwanzoni viongozi waandamizi wa chadema hususani ngazi ya taifa walikua wakijipiga kifua sana hadaharani kwamba hakuna mgawanyiko wala mpasuko wowote ndani ya chadema, ispokua kilichokua kinajitokeza ni uhuru wa viongozi na wanachama wa chadema kutoa maoni na mitazamo yao dhidi ya waliyo kua wakiyaona ndani ya chama chao.
Lakini kwasasa, ni wazi waliokua wanakana kutofautiani ndio hao hao wanalumbana waziwazi na kupambana kugombania nafasi na fursa za uongozi wa ngazi za juu chadema.
Unafiki wao wa kiwango cha juu, wanaupambanua wenyewe bila kificho kwasasa, kwa kutuhumiana masuala ya rushwa, kudanganya umma au kusema uongo.
Ni mategemeo ya wengi kwamba unafiki zaidi miongoni mwa viongozi waandamizi wa chadema, unatarajiwa kuibuka na kujidhihirisha bayana kadiri siku za uchaguzi zinavyokaribia.
Vita ya maneno ni kali mno, na kuna mashaka na hofu kubwa sana katika kila upande, na ni kwamba vita hii isipodhibitiwa kisaisa mapema inaweza kuleta madhara ya kijamii na kisiasa miongoni mwa wahusika na chadema wakapata hasara na huzuni.
Una maoni gani?