Mgawanyiko wa vyama vya siasa

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Wataalamu wanasema ukichukuwa idadi ya wanachama wenye usajili ukazidisha mara mbili ndiyo nguvu ya wafuasi wao. Tujue kuna watoto ambao ni wapambe wa wanachama walezi wao kwenye mahesabu haya

kwa hivyo CCM ina wanachama 17M na wafuasi kwa ujuma 34M, Chadema wanachama 7M na wafuasi 14M wengine wote ni vyama vingine. Hivyo Kwa idadi ya 60M kwa Watanzania wote CCM 56%, Chadema 23% na wengine wote 21%.

Tatizo ni viongozi wengi serikalini kujiaminisha wapo 100% hivyo migogoro itatokea tu mpaka pale watakapo jua wana 56% tu na inapingua kila kukicha. Nchi yetu haitaweza kuendelea mpaka pale kuwe na maelewano ya hivi vyama
 
Ccm hata 30% hawana nitakupa hoja ni vile watu hawatoki kupiga kura wakitoka ccm akijitaidi sana atapata 30%

Halafu acha uongo wanachama wa ccm hawafiki hata milion6 wapo kwenye million 5 na kitu kwa mujibu wa kadi za uwanachama.
 
Watu wazima wanaoweza kujiunga na vyama vyao siasa nchini Tanzania ni chini ya ya 34m.
Watu 60m ni pamoja na watoto wachanga.
 
Ndugu Kamuundu takwimu hizo ni zile za kupikwa au ni zile zitokanazo na Sheria ile ya takwimu ya mswaada wa hati ya dharura wa awamu tangulizi?
 
Kweli ccm wangekuwa na wafuasi wengi hivyo wasingekuwa na sababu ya kuiba kura au kuhujumu uchaguzi. Kimsingi wangekuwa wa kwanza kukubali tume huru ya uchaguzi.

Lakini kwa kuwa hawana namba hizo watakuwa watu wa kuhangaika siku zote kuwa refa katika mechi wanayocheza ili kuepuka kufutika katika uwanja wa siasa nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…