saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
12 Septemba 2021 ni siku ambayo Tanzania iliingia kwenye mgogoro mkubwa wa kiuchumi baada ya kuteuliwa Januari Makamba(MNEC) kuwa Waziri wa Nishati.
Mwaka 2022 unaelekea kufikia mwisho ni mwaka ambao watanzania wengi wa hali ya chini wamefilisika na wengine biashara zao nyingi zimekufa na kupoteza wateja hasa zile biashara zilizokuwa zinategemea uwepo wa nishati ya umeme karibu kipindi chote cha mwaka 2022.
Watu wa biashara za saluni za kike na za kiume, biashara za stationary, biashara za uchomeleaji vyuma, biashara za kufyatua matofali, biashara za kuuza nyimbo kwenye flash, biashara za studio za muziki, biashara za bucha za samaki na nyama, wauza juice.
Wengine waliolia kilio kikubwa ni watengenezaji wa barafu, wauzaji wa ice cream, biashara za visima vya maji na biashara mbalimbali zinazotegemea umeme hawatausahau mwaka 2022 jinsi walivyopoteza mapato mengi kutokana na kadhia ya kukosekana kwa umeme kwa sababu ya Januari Makamba(MNEC)
Wenye viwanda nao hawatausahau mwaka 2022 kwa jinsi walivyolazimika kupunguza shift za uzalishaji kutokana na mgao wa umeme.
Na sisi wananchi wa mwisho hatutasahau jinsi bidhaa zilivyopanda bei mara dufu vikiwemo vifaa vya ujenzi kama mabati, saruji, nondo, vigae na bidhaa mbalimbali za viwandani kutokana upatikanaji mdogo wa bidhaa kutokana na uzalishaji mdogo viwandani uliosababishwa na tatizo la umeme.
Pamoja na matatizo makubwa hayo ya kiuchumi yako mengi mazuri yamefanywa na Serikali ikiwemo ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari.
Tunaweza kuyakumbuka matatizo mengine makubwa yaliyotuathiri kama taifa kwa mwaka 2022 kutokana na usimamizi mbovu wa mawaziri wetu waliopewa dhamana.