Mgawo wa Umeme wasitishwa, utafiti mpya umeona hauhitajiki kama awali

Kwahiyo Rais akisema usiwepo basi hautakuwepo
 
Tanesko kuna siku tanesko tutawapeleka mahakamani kwa kukatakata na kuwasha, hii inaonyesha wazi kuna kamchezo kanafanywa na manegiment ya tanesko, tafuteni njia mbadala ya kunusuru tatizo lenu la Zima na kuwasha huu michezo muuache mnakela mno.
 
Safi Mama Samia...Tanesco wasimamiwe vizuri.
Safi ya nini sasa wewe bendera fuata upepo. Haingii akilini wanatengeneza tatizo halafu wanalitatua wenyewe ili wananchi waone kuwa viongozi wana huruma na wanyonge kumbe ni 0.
 
Kwa hiyo Maharage, Makamba na bodi yao ya akina Gachuma walikurupuka kuanzisha mgao mkali wa umeme nchi nzima kwa sababu mitambo mingi ya kufua umeme ni mibovu, chakavu na ni ya mingi? Kwamba mitambo hii inatakiwa kuwa replaced na mipya. Na kwamba hata huko Songosongo mitambo ya kufua gesi ya kampuni binafsi ya Songas nguvu yake haikidhi mahitaji na inatakiwa kufungwa mingine kuiongeza nguvu. Na kwamba kutakuwa na upungufu wa 350 MW kwenye grid ya taifa.

Mama katuma makachero wake na kugundua kuwa si kweli na kuwaagiza hataki kusikia mchezo huo la sivyo atawatumbua. Ndiyo sasa wanatuambia kwamba kamati yao ya watalaam wamefanya utafiti na kubaini kwamba hakutakuwa na upungufu wa maana wa umeme wakati wa zoezi hili la normal maintanance ya mitambo. Upungufu kidogo usiozidi 100 MW utaweza kuwa absolved kirahisi na mfumo. Hivyo hakutakuwa na mgawo.

Sasa kwa situation kama hii kwa nini Maharage, Makamba na bodi yake wasiachie ngazi for gross incompetency? Yaani hadi Maharage anasema kwamba masuala haya ni ya sayansi na engineering. Yaani kwake engineering siyo sayansi. Engineering is separate from science! Huu ni Uswahili mtupu.
 
Hamna cha makachero. Wakina Makamba walikuwa sahihi. Hapa ama tunarudi kule ambako neno mgao liliacha kutumika wakati umeme ulikuwa unakatwa. Au tatizo limesogezwa mbele lakini bado limebakia kuwa tatizo. Gharama ya kufanya hivi tutaijua huko mbeleni.

Amandla..
 
Huyo mama na makachero wapi na wapi? Wameona mitandao watu wanavyolalamika basi wakashituka! Huyo mama kama angekuwa mfatiliaji wa mambo tokea makamba aingie kashafanya ujinga mwingi wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na mikataba ya ovyo ovyo!
Kwa hiyo Maharage, Makamba na bodi yao ya akina Gachuma walikurupuka kuanzisha mgao mkali wa umeme nchi nzima kwa sababu mitambo mingi ya kufua umeme ni mibovu, chakavu na ni ya mingi?...
 
Mambo ya kurekebisha mitambo ni kuwaona watz wote wajinga.shida ni kina cha maji kilikuwa chini.baada ya mvua ya juzi kina kimeongezeka.sijui sababu gani wanasiasa hawapendi kuongea ukweli
 
Mbona kuna jamaa huko analoloma na koroboi yake toka sa sita.mpk 12
 
Sasa unaelewa kwa nini mitambo haifanyiwi service au maintenance? Political expediency kwa kwenda mbele.

Amandla...
Ifanyiwe maintenance au isifanyiwe, hiyo siyo sababu ya kusababisha migao.

Ndo maana nimeshahoji kuwa, huko kwingine mitambo yao huwa haifanyiwi maintenance?

Maana katu sijawahi sikia hata kwa lisaa limoja tu kuwa kutakuwepo na mgao wa umeme wa siku 10 kwa sababu mitambo inafanyiwa maintenance.

Hawa Tanesco wetu hawana uwezo wa kufanya maintenance kwenye mitambo yao bila kusitisha huduma? Haiwezekani kabisa kufanya hivyo?
 
Huyo mama na makachero wapi na wapi? Wameona mitandao watu wanavyolalamika basi wakashituka! Huyo mama kama angekuwa mfatiliaji wa mambo tokea makamba aingie kashafanya ujinga mwingi wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na mikataba ya ovyo ovyo!
[Color= red]✓Hatashituka ikifika mwaka 2025

Sent from my Nokia 1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kwa sababu Kalemani alilimaliza kabisa tatizo la mgao wa umeme naamini January Makamba baada ya haya matengenezo anayoyafanya kwa siku 10 siyo tu mgai utakuwa historia bali hata kiwango cha umeme unaozalishwa kitaongezeka.

Kadhalika kwa sababu sasa umeme utakuwa haupotei baada ya miundombinu kukarabatiwa ni wazi bei ya umeme mitashuka.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!
 
CCM ni kansa
 
Back
Top Bottom