Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Leo jioni nimepokea mgeni adhim kupita kiasi niliyekutananae akiwa mtoto mdogo akisoma shule ya msingi.
Mtoto huyubalikuja nyumbani kwangu kaletwa na baba yake.
Ilikuwa asubuhi moja mwaka wa 2018.
Mtoto huyu baba yake ambae hatukuwa tunafahamiana aliniambia kuwa mwanae alikuwa amesoma kitabu cha Abdul Sykes na kimemuathiri sana kiasi alimuomba ampeleke kwa mwandishi wa kitabu hicho.
Hivi ndivyo nilivyokutana na kijana huyu kwenye picha hiyo hapo chini.
Jina la mtoto huyu ni Abdulrahman Yahya Ahmed.
Mtoto huyu alinionyesha maajabu.
Alikuwa kahifadhi sehemu za kitabu cha Abdul Sykes ghibu na akawa ananisomea.
Ukimsikiliza utadhani anasoma Barzanji.
Mashaallah.
Nilishangaa pakubwa.
Miaka sita imepita.
Mtoto huyu ambae sasa ni kijana kama anavyoonekana hapo chini picha ya kwanza leo kaja nyumbani kwangu kunisalimu.
Hivi sasa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu na alikuwa nje ya Tanzania akisoma.
Amekuja kuniona na kaniletea zawadi ya vitabu kwa ajili ya Maktaba.
Furaha yangu kwa hakika haisemeki wala haielezeki.
Mwangalie hapo chini Abdulrahman alivyokuwa mwaka wa 2018 akinisomea kitabu cha Abdul Sykes ghibu yaani anasoma kutoka kichwani.
Baba yake ni huyo aliyekaa mkono wa kushoto.
Picha hii niliipiga tarehe 4 August 2018 saa 3:38 asubuhi.
Abdulrahman 2024
Abdulrahman 2018