Mgodi wa North Mara imeleta maafa Ziwa Victoria tena, Serikali inajiuma uma tu kwa kamati feki

Mgodi wa North Mara imeleta maafa Ziwa Victoria tena, Serikali inajiuma uma tu kwa kamati feki

Haijawahi kutokea eti kinyesi na mkojo wa ng'ombe kwenye maji yanayotembea unasababisha sumu ya kuua viumbe walioko majini?

Nilikuwa JKT kwa mwaka mzima, kipindi tunapata mafunzo ya porini tulikuwa tunapitishwa kwenye malambo ya maji ambamo mifugo inakunywa na kujisaidia lakini mpaka tuna maliza mafunzo hakuna hata mmoja aliyeugua typhoid nk iweje sasa eti kwenye mto Mara mifugo imechangia uwepo wa sumu iliyoathiri uhai wa samaki kwenye maji yanayotembea?

Mwenyekiti wa kamati hiyo amefanya uchunguzi kwa faida ya aliyemtukama sio uhalisia na matokeo yakinifu ya kitaalamu-apewe pole kwa kupotosha umma na kama nafsi inamsuta anatakiwa aombe radhi kwa kuwa osio yeye pekee mwenye uwezo wa kuchunguza kisababibisha cha madhara kwa samaki ndani ya maji yanayotembea
You are correct Braza! Mtu kama huyu kujiita Profesa, ameongeza idadi ya wale wa aina ya Lipumba. Sidhani kama aliheshimu sheria za uandishi ili angalau pitio la maandishi ya wengine limpe support kwamba kinyesi cha ng'ombe ni sumu. He is just a hopeless lame scholar. Unfortunately aliwahi kuwa mkemia mkuu wa serikali bila credentials, Nimeona mtu akieleza kumbe alipewa kikabila na PM aliyepita.
 
Hili siyo tatizo jipya! Linathibitisha uzembe wa serikali ya CCM.

Wakati mh. Sitta akiwa Spika na mama Makinda naibu wake, uchunguzi wa aina hii ulifanyika, lakini ajabu kabisa hata Sitta alikuwa analazimiasha ionekane hakuna tatizo la mgodi.

Ni wazi kwamba North Mara Gold mine ltd wanatumia pesa kuficha ukweli na kuumiza wananchi na mazingira.

Kwa ujumla wananchi wote wa TZ tunaumizwa maana tunakula samaki wa ziwa nchi nzima.

Hii kamati ya sasa imeundwa na waziri Jaffo.

Naiona ni kama uchafu tu! Uchafuzi wa kemikali ulihitaji watu makini zaidi.

Siwaoni hapo! Naweza kusema hii imeundwa kutuliza vumbi.

Waziri kisha ramba kiasi chake anachoweza na kazi iendelee.

Haya ndo mawazo ya wakulima mitaani:

View attachment 2159656
Mtakwisha kwa Kansa huko Kanda ya Ziwa .
 
Ukiwa huna Utu hata baba yako utamuuwa kwa thamani ndogo

Sio eti ndio tumefika huku hapana ni tabia na hulka ya mswahili
 
Sasa naanza kuelewa kwa nini kanda ya ziwa inaongoza kwenye ugonjwa wa saratani Tanzania.

Ni muhimu uchunguzi wa kina ufanyike....kwenye hii migodi yote Geita, North Mara, Stamigold, Bulyanhulu na Buzwagi sijui wameshafunga na ile ya zamani Buhemba.

Na baadhi zinazoibuka...
Mlisema huko lake zone ni sehemu sahihi ya kuishi mbona mnaanza kuulizana?

Na bado,mgodi mpya unafunguliwa sengerema tena mkubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom