Mgogoro iliozusha Marekani si kati yake na China, bali ni kati ya ubinadamu na umwamba

Mgogoro iliozusha Marekani si kati yake na China, bali ni kati ya ubinadamu na umwamba

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111338516390.jpg


Hivi karibuni, maandamano ya kupinga serikali yalitokea nchini Cuba. Wakati jamii ya kimataifa ilipotia wasiwasi na kuwa tayari kutoa msaada, Marekani nayo ilitumia maandamano hayo kama ni fursa. Rais Joe Biden alisema, “Marekani iko pamoja na watu wa Cuba”, na kutangaza vikwazo vipya dhidi ya nchi hiyo.

Ukweli ni kuwa Marekani haiko pamoja na watu wa Cuba, bali inatembea migongoni mwao. Je, kwa nini Marekani haiwezi kuvumilia uwepo wa nchi ndogo ya kijamaa kusini mwake na kuendelea kuiwekea vikwazo vya kijeshi, kisiasa na kiuchumi bila kujali kura za hapana zinazopigwa miaka mingi na nchi mbalimbali katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, huku ikikaa nyuma ya wafarakanishaji na kuwaunga mkono kupindua serikali ya Cuba.

Ni wazi kuwa janga la virusi vya Corona limeanika matatizo yaliyopo katika mfumo wa jamii ya Marekani. Watu zaidi ya laki 6.3 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa COVID-19, lakini serikali ya Biden inazingatia tu jinsi ya kulinda itikadi ya ubepari na hadhi ya umwamba chini ya mfumo wa ubeberu, hili ni jambo linalotia aibu. Wakati nchi mbalimbali duniani zinapojitahidi kupambana na virusi, sera ya Marekani ya kuzingatia itikadi peke yake sio tu imenyima haki za kimsingi za watu wake, bali pia imezidisha mgogoro kati yake na nchi zenye mifumo tofauti ya kisiasa, na kuzipa taabu kubwa zaidi nchi hizi katika kukabiliana na janga hilo.

Cuba, nchi maskini zaidi duniani, inaweza kutokomeza haraka njaa na tatizo la kutojua kuandika wala kusoma, lakini Marekani nchi tajiri zaidi duniani bado inakabiliwa na matatizo hayo. Hii ina maana kuwa kiini cha mfumo wa ujamaa ni ubinadamu, yaani kuweka kipaumbele maslahi ya umma kuliko faida za kiuchumi, jambo ambalo halitakubaliwa kamwe na watu mashuhuri wa Marekani. Mfumo wa ubepari ni hodari katika kuzalisha bidhaa nyingi, kama vile huduma za matibabu zenye bei kubwa, lakini haupendi kutoa mfumo bora wa afya ya umma, ambao hauna faida yoyote ya kiuchumi. Nchini Marekani, kuchuma pesa ni jambo zuri na sahihi, lakini kwa sababu ya ukosefu mkubwa wa usawa katika jamii, watu wengi wanashindwa kumudu huduma bora za matibabu.

Tofauti na Marekani, jinsi China inavyokabiliana na janga hilo imeonesha mtazamo wake wa kuweka kipaumbele maslahi ya watu na nguvu bora ya mfumo wa kisiasa, na pia inalingana na ushauri uliotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO, yaani kuheshimu sayansi na ubinadamu na kupambana na janga hilo kwa ushirikiano. Wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC wako katika mstari wa mbele kuwatibu wagonjwa, na serikali imetumia mfuko wa hazina ya taifa kuunga mkono mapambano haya. Hapa kuna tofauti kubwa na jinsi nchi nyingi za magharibi zinavyodharau sayansi, ubinadamu na kutetea sera mbaya ya utaifa. Kwa mfano, ni kwa sababu kushindwa kukabiliana na janga hilo, rais aliyepita wa Marekani Donald Trump aliitupia lawama China, badala ya kutathmini ipasavyo mchango uliotolewa na CPC na serikali ya China kwa dunia.

Nchi za magharibi zinaogopa kuinuka kwa nchi kama China. Kwa mfano katika miaka hii 50, nchi za magharibi ziliongoza kabisa katika sekta ya sayansi duniani, na kujipatia faida nyingi kwa kurefusha muda wa hakimiliki za ubunifu. Maendeleo ya China yamechukuliwa kama ni tishio kubwa kwa hadhi ya uongozi ya nchi hizo katika mawasiliano ya simu, roboti, reli ya mwendo kasi na sekta nyingi za sayansi. Ni kwa sababu ya kuogopa kupoteza hadhi yao ya uongozi, Marekani ilizusha “vita baridi mpya” na China, na kuchukua hatua nne zifuatazo:

Kwanza, kuanzisha vita ya kibiashara na China ili kulinda umwamba wake kiuchumi na kiteknolojia; pili, kuwashinikiza washirika wake kupambana na China, ili China itengwe duniani; tatu, kuwaunga mkono watu wanaofarakanisha China kwa jina la “haki za binadamu” na kuchafua sura ya China kimataifa; nne ni uchokozi wa kijeshi, haswa kwa kupitia eti muungano wa nchi nne, yaani Australia, India, Japan na Marekani. Lakini kinachochekesha ni kuwa “kundi hili jipya” limefanya juu chini kuzishinikiza China na nchi nyingine, jambo ambalo haliendani na Mkataba wa Umoja wa Mataifa ulioanzishwa na nchi za mashariki na magharibi kwa pamoja zikiwemo nchi hizi nne. Hii ndio sababu nchi 17 zikiwemo China na Russia zimeanzisha kundi la kirafiki la kutetea Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Hii ni hatua muhimu, kwani kwa upande mmoja inatoa heshima kwa Mkataba huo, na kwa upande mwingine kupinga matumizi ya demokrasia kwa jina tu.

Mwezi Septemba mwaka huu, harakati ya kutofungamana na upande wowote itatimiza miaka 60. Nchi nyingi zinazoendelea bado zinatetea kithabiti harakati hiyo, kwani hazipendi kuchagua upande katika “vita baridi mpya” iliyoanzishwa na Marekani. Hili sio mgogoro kati ya China na Marekani, bali ni kati ya ubinadamu na umwamba.
 
Haya mambo yanafikirisha sana, hapo ndio unaelewa usemi "Dunia Uwanja wa fujo"
 
Haya mambo yanafikirisha sana, hapo ndio unaelewa usemi "Dunia Uwanja wa fujo"
E F Kezilahabi ha ha haaa aliandika vema Dunia Ni uwanja wa fujo...

Malizia hii ..Usiku utakapokwisha.!!
 
Back
Top Bottom