Mgogoro NCCR Mageuzi: Timu Mbatia wachukua ofisi, wasema umefanyika uhaini ndani ya chama, Mbatia bado ni mwenyekiti

Watakuja kupigana risasi wasipokuwa makini.
 
Poor NCCR MAGEUZI😡
 
Wenyeviti wa hizi SACCOS kutoka Kaskazini wameona kama uenyekiti ni haki zao,Mbatia pamoja na Mbowe ni wenyeviti kwa muda mrefu hawana tofauti na raisi wa Uganda M7,
Huyo Anton Komu anayetajwa kama kaimu katibu mkuu alitoka nccr akaenda chadema; kumbe alirudi tena nccr.

Wao kila wanapokwenda ni kutafuta ukubwa kwa njia za kihuni na kusababisha migogoro.
 
Vita vya Madaraka.

Selasini hawezi kubali kuwa sio kiongozi popote alipo
Hivi kuwavua wadhamini wa chama ni rahisi hivyo.
Kama kuna makosa ya Mbatia nadhani hawa wadhamini ndio walitakiwa wawe mstari wa mbele.Uhuni juu ya uhuni.
 
Hiyo ni ccm na serikali yake isiyo na ridhaa ya watanzania ndio wanafanya huo uhuni kisa ni Mbatia kukataa kushiriki kwenye ule mkutano feki ulioandaliwa na serikali.

Tena ni serikali ndiyo imetoa hata pesa za kugharamia huo mkutano na kumpatia Selasini na ndio maana hata msajili alikuwepo kwenye huo mkutano.

Serikali ya ccm siku zote inachokifanya ni kupambana na upinzani na kwa kuwa mshika mbili moja humponyoka ndio maana nchi haiwezi kuendelea kwa sababu serikali nguvu kubwa wanapeleka kwenye kupambana na upinzani.

Hiyo ndiyo ajenda kubwa ya ccm na haijalishi nani yuko madarakani hata hatoke huyu mama aingie mwingine sera ni hiyo hiyo na kama tutaendelea kuwa na hii katiba yao mwisho hii nchi itakuwa takataka kabisa.
 
Vita ya pazi vuraha kwa kunguru .Hapo lazima kuna watu wanakitaka kiti cha uwenjekiti kwa kutumia usnitch
 
Kabla ya chadema alikuwa wapi?!

Mtu yoyote mwenye umri zaidi ya miaka 50 lazima alikuwa CCM hata kama alikuwa hataki. Zamani hizo kila mtu mwenye umri wa miaka 18+ alikuwa na kadi ya CCM kwa lazima, wakati wengi hawakuwa na vitambulisho.
 
Huyu selAsini ni chawa na funza hatakiwi kwenye chama, ikiwezekana chama kimtimue kama chadema ilivyomtimua
 
System ipo kazini kumzima Mbatia kwasababu ya msimamo wake anaouonesha siku hizi kuhusu hali ya kidemokrasia nchini, wale kina Selasini ni wasaliti ndani ya NCCR.
 

Ila CHADEMA imetapakaa Sana. Huyu Simbeye alikuwa CHADEMA miaka ya nyuma hapo. Kweli CHADEMA ni kiwanda Cha kutengeneza wanasiasa. Mpaka CCM walienda kununua huko baada ya kuona kwao ni magalasa. Keep it up CHADEMA.
 

Unaziita SACCOS Halafu unataka zifanye demokrasia. Acha dharau na kiburi. Zingekuwa SACCOS mngefanya uchafuzi wa 2019 na 2020. Mngewaingilia CHADEMA kwenye viti maalum?. Acheni dharau wakati mkizidiwa mnawamiminia Risasi na kuwabambikizia kesi za ugaidi. Acha dharau maana Rais wa nchi ana jua thamani ya hivi vyama ndio maana anaongea nao ikulu.
 
Unashangaa hayo tu!hushangai mtu ni Rais na bado ni mwenyekiti wa chama,wakati huo huo wenzie anawaambia lazima mchague kimoja!! Na siku ya uchaguzi inaandaliwa fomu ya mgombea mmoja tu kwenye nafasi ya mwenyekiti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…