Mgogoro wa Ardhi Katoro: Mwenye hati ni CCM, sisi ni watoto wa CCM; tutashauri chama, mwekezaji anamuharibia Rais wetu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mwalimu Jumanne Misungwi, ametaka hekima na busara zitumike katika utatuzi wa mgogoro wa eneo linalodaiwa kuwa mali ya Serikali, akisisitiza umuhimu wa kufanya vikao vya ndani ili kupata suluhisho la kudumu.

Misungwi ametoa kauli hiyo kufuatia sintofahamu iliyoibuka na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonyesha mwekezaji mmoja akirushiana maneno na Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Musukuma, kuhusiana na umiliki wa eneo hilo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo akiwa na Kamati ya Fedha ya Halmashauri, Misungwi alisema kuna madai kuwa mwekezaji huyo alivamia na kubomoa majengo ya Halmashauri bila kupata ridhaa rasmi kutoka kwenye mamlaka husika.

Ameeleza kuwa Halmashauri inaendelea kukusanya taarifa na vielelezo ili kubaini ukweli wa madai hayo, huku akisisitiza kuwa hakuna mtu au taasisi inayopaswa kuchukua hatua nje ya utaratibu wa kisheria.

Mwenyekiti huyo alihitimisha kwa kusema kuwa masuala ya ardhi yanahitaji utatuzi wa amani, kwa kufuata sheria na kwa kushirikisha wadau wote muhimu ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.

Majizi yanaparurana
 
Back
Top Bottom