KERO Mgogoro wa Ardhi Lindi: Wananchi Muhimbili Juu tunadhulumiwa maeneo yetu bila kupata msaada wowote

KERO Mgogoro wa Ardhi Lindi: Wananchi Muhimbili Juu tunadhulumiwa maeneo yetu bila kupata msaada wowote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Wananchi wa Mtaa wa Muhimbili Juu, Kata ya Rasibula, Manispaa ya Lindi, tunataka kunyang’anywa ardhi yetu katika mgogoro ambao umedumu tangu mwaka 2022.

Mtu anayejulikana kwa jina la Kahawa kavamia maeneo yetu. Katika utatuzi wa awali, ilipendekezwa kuwa atufidie wananchi au atuhamishie eneo lingine. Hata hivyo, tulikataa pendekezo hilo na kusisitiza kutaka kubaki katika maeneo yetu. Baada ya muda, maafisa wa ardhi walifika na kupiga picha za eneo hilo bila kutujulisha wananchi wala Mwenyekiti wa Mtaa kuhusu zoezi hilo.

Mgogoro huo umeibuka upya mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu baada ya wananchi kwenda kuomba maeneo yao yapimwe ili waweze kupata huduma za kijamii, hususan maji na umeme. Hata hivyo, waliambiwa kwanza watatue mgogoro uliopo na mtu huyo anayeitwa Kahawa.

Wananchi tunalalamika kuzungushwa na watendaji wa mtaa husika pamoja na maafisa wa ardhi. Pia, Kahawa amewalipa fedha baadhi ya viongozi wa mtaa ili wamuwezeshe kupata eneo hilo kinyume na utaratibu.

Kutokana na hali hiyo, wananchi tunaomba suala hilo lifichuliwe ili tupate haki yetu, maeneo yetu yapimwe na umiliki wake urasimishwe, pamoja na kuwezeshwa kupata huduma muhimu za kijamii.
 
Back
Top Bottom