Nyoka kibisa
JF-Expert Member
- Nov 30, 2014
- 568
- 1,507
Wadau mwaka jana mwanajf Suley2019 alileta habari hapa jf kuhusu mgogoro wa ardhi katika kijiji cha nyambogo wilaya ya rorya iliyopelekea mwili wa marehemu kutozikwa zaidi ya miezi 8.
- Rorya, Mara: Mgogoro wa ardhi wasababisha marehemu kutozikwa tangu Januari 20, 2021 mpaka leo
Naam kuna kihoja tena katika kijiji hicho hicho cha nyambogo ambapo kuna mgogoro kati ya mama moja na familia ya kwao na adodo. Ambapo kwa madai ni kwamba mzee wake adodo alimkaribisha huyo mama kwa kumpatia eneo la makazi miaka zaidi ya 20 iliyopita na ni eneo la senta baada ya mji kukua na hawa vijana akina adodo na nduguze kugundua eneo alolopatiwa huyo mama ni sehemu ya kibiashara zaidi ikabidi wafungue kesi.
Lakini walishindwa kesi na huyu mama kwa kila hatua waliyoenda.
Sasa cha kufurahisha na kusikitisha ni kwamba miaka miwili baadae hawa vijana wakaja kujenga makaburi mawili uwanjani kwa huyu mama wakidai hapo ndipo wazazi wao walipo zikwa na mara baada ya makaburi kujengwa makaburi yalivunjwa vunjwa na mtu asiyejulikana
Mkuu wa wilaya alifika eneo la tukio ambapo makaburi yalijengwa na baada ya kupatiwa nyaraka za eneo alisema huyo mama ana haki zote.
Lakini maneno ya mkuu wa wilaya hayajasaidia kitu kwani inavyosemekana hawa vijana wameapa kumchinja au hata kumchoma huyo mama moto ndani ya nyumba ili warejeshe eneo lao hali iliopelekea huyo mama kulala kwa majirani akihofia maisha yake.
Lakini inavyosemekana ni kwamba baraza la ardhi la kata ndio limeoza na kutawaliwa na rushwa na wanafanya kazi kwa mihemko.
Pia soma