Mgogoro wa Ethiopia unadhihirisha umadhubuti wa mfumo wetu wa mikoa dhidi ya ule mfumo wa majimbo

U
Unaingiza dini ili ulete taharuki...nimeshakujibu katika comment nyingine angalia hapo chini......

Zanzibar na Tanganyika ni nchi moja.....nguvu ya KUYALINDA MAPINDUZI matukufu hutoka pande zote na ndio maana kufikia leo HAYAJANAJISIWA......
Tanzania ni nchi moja iliyoundwa kwa muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar. Kwa hiyo Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili na sio moja. Acha porojo za kiccm za kudai 9 desemba ni uhuru wa Tanzania Bara.
 
Kuhusu sttatement yako ya mwisho, Labda nikuulize dhuluma za uchaguzi zinazofanywa na chama chenye dola huwa ni kwa maslahi ya nani !? Maslahi ya wananchi au wenye chama!? Kama ni ya wananchi, je kwa nini maamuzi ya wenye nchi yasiheshimiwe!? Au wenye chama ndiyo wamiliki wa nchi!? Au wale wasio chama dola nao waingie msituni kama alivyowahi kushauri Museveni maana naye aliingia msituni? Ila hapa nchini maslahi ya ccm ni makubwa kuliko ya nchi na ndio maana wako tayari kuiba fedha BoT ili kugharamia uchaguzi.
 
U

Tanzania ni nchi moja iliyoundwa kwa muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar. Kwa hiyo Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili na sio moja. Acha porojo za kiccm za kudai 9 desemba ni uhuru wa Tanzania Bara.
Kama ni nchi mbili mbona Zanzibar haina kiti cha kudumu umoja wa mataifa?!!!
 
Hili ndio tatizo kuu la Ethiopia yaani ukabila, hayo ya majimbo sio kweli.

Upo sahihi kabisa, mazingira yetu ya kisiasa ni tofauti kabisa na Ethiopia hivyo serikali ya majimbo haiwezi kutuigawa au kuivunja nchi hao wanaotumia Ethiopia kupinga huo mfumo huenda wanapotosha tu makusudi au hawaijui historia ya Ethiopia.
 
Kama ni nchi mbili mbona Zanzibar haina kiti cha kudumu umoja wa mataifa?!!!
Je, Tanganyika ina kiti huko!? Naona unajaribu kutonielewa. Wewe umeandika "Zanzibar na Tanganyika ni nchi moja" . Na mimi niamendika Tanzania ni nchi moja iliyoundwa kwa muungano wa nchi mbili Zanzibar na Tanganyika" Kwa hiyo kuandika kuwa Zanzibar na Tanganyika ni nchi moja huo ni uongo.
 
Chukua K-Vant kubwa 3 nitalipa.
 
Unatumia kinywaji gani kaka?
 
Bro hebu Google zaidi juu ya armed forces za ndani ya majimbo ya America
Marekani wana federal army halafu majimbo pia yana forces zake mzee.
Ndio maana enzi za ubaguzi, kulikuwa na utata ambapo jimbo la Arkansas na gavana wake na jeshi lake la ndani walizuia black students kusoma katika shule ya little Rock high school,
Ikabidi rais wa enzi hizo atume federal army kupambana na gavana na wafuasi wake na hiyo armed forces yake, ilibidi a tumie federal army kulazimisha serikali na viongozi wa jimbo na askari wao wa ndani waruhusu watoto weusi waingie shule.

Kwa hivyo mifano ipo ya majimbo kufika huko kwenye kutumia army kupingana na serikali ya kitaifa
Na si hivyo tu mifano iko mingi huko marekani ya majimbo kugombana, kama vile, mgogoro wa maji ya mto Colorado, mto una pita katika majimbo makame na ni chanzo cha maji cha majiji kama Los Angeles , kuna utata mkubwa wa matumizi ya rasilimali hiyo, kila jimbo linaona linaonewa na California inayotumia maji kupita majimbo mezake

Pia kumbuka Civil War huko USA umajimbo ulinogesha ile vita vilivyo
 
Mkuu wa wa Army, Navy, Marines, Air Force, Space Force na National Guard ni Rais wa Marekani na mkuu wa hayo majeshi yote ni Rais wa Marekani. Hakuna majeshi ya majimbo Marekani.
 
Mkuu wa wa Army, Navy, Marines, Air Force, Space Force na National Guard ni Rais wa Marekani na mkuu wa hayo majeshi yote ni Rais wa Marekani. Hakuna majeshi ya majimbo Marekani.
Ndugu ushahidi huu ka google
Marekani wana kitu kinaitwa state de fence forces, ambazo zipo chini ya Magavana wa majimbo
 

..mbona Tz kuna mikoa iko nyuma kimaendeleo utadhani si sehemu ya Tz?

..hata mfumo centralized wa mikoa bado ubaguzi upo na mfano mzuri ni kilichokuwa kikiendelea awamu ya 5 kwa upendeleo wa wazi kwa eneo fulani.
 
Sasa pata picha, Eti na sisi tungekuwa na vijeshi uchwara huko arusha sijui moro sijui mbeya,
Huo umajimbo hauna maana
 
Kwani kimeondoshwa?au ulikivunja wewe miguu kikatupwa?
Nakusubiri unijibu maswali yangu usikimbie
Shangaa na Scotland ,Wales na Ireland kutokuwa na kiti hapo umoja wa mataifa.......
 
TANGANYIKA ilikuwa na kiti kabla ya Muungano.....leo ni kimoja tu kwa ajili ya URT........

Mbona Scotland ,Wales na Ireland hawana viti huko UN?!!!
 
Hayo sio majeshi, ni kama walivyo mgambo.
Labda hujui kiingereza nikusaidie,
Mgambo kwa kingereza huitwa militia na sio forces,
Forces kwa kiswahili ni majeshi
Na hayo majeshi ya ndani ya majimbo ya America ya naitwa, 'state defence forces', yani in swahili tunatafsiri, 'majeshi ya ulinzi ya majimbo'

Mzee baba ni majeshi ya ulinzi na sio Mgambo wa ulinzi, wangeita 'state defence militia' kama ingekuwa ni mgambo tu
Hebu ongeza ilmu hapo kati
 
Shangaa na Scotland ,Wales na Ireland kutokuwa na kiti hapo umoja wa mataifa.......
Mimi sijakuuliza Scotland wala Wales , nakuuliza unao ushahidi kiti cha Zanzibar kimeondoshwa? Au ulikiondosha wewe baada kukivunja miguu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…