JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) kati ya USM Alger ya Algeria dhidi ya RS Berkane ya Morocco umeshindikana kufanyika baada ya wageni RS Berkane kuzikataa jezi walizozikuta kwenye vyumba vya uwanjani wakidai sio zao.
Awali, RS Berkane walidai jezi zao zilizuiwa Uwanja wa Ndege walipowasili Algeria, wakawaambia hawataruhusiwa kuzitumia kwa kuwa zina Bendera ya Morocco, jambo ambalo lilipingwa na RS Berkane na kusisitiza wanataka kuzitumia jezi hizo la sivyo hawataingia uwanjani.
RS Berkane ilipofika katika vyumba vya uwanja, ikakuta jezi ambazo hazina bendera ya Morocco, ikagoma kuingia uwanjani na baada ya majadiliano marefu wameondoka uwanjani.
Wadau wanasubiri maamuzi kutoka kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Nusu Fainali nyingine ya kombe hilo Zamalek (Misri) 0-0 Dreams FC (Ghana).