figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Salaam Wakuu,
Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais Yoon Suk Yeol wa Jamhuri ya Korea walishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ushirikiano wa Uchumi (EPA).
Mkataba ambao utaiwezesha Tanzania kupokea mkopo kutoka Korea wa kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 2.5 kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia (2024- 2028).
Rais Samia pia alipendekeza ushirikiano wa sekta nyingine mpya zikiwemo maendeleo ya nishati ya gesi asilia; sekta ya Ubunifu ikiwemo sanaa na filamu; na kufunguliwa kwa soko la ajira la nchini Korea kwa vijana wa Tanzania kupitia mpango wa Employment Permit System (EPS).
Sasa Rais wa Korea amekalia kuti kavu. Wananchi wake wanaandamana ili ajiuzulu.
Juzi rais wa Korea alivunja Bunge na kuondoa utawala wa Kiraia na kuongoza kijeshi.
Sasa mambo yamemgeukia. Amrudisha utawala wa kiraia Wananchi hawataki. Wanataka ajiuzulu.
Uchu wa madaraka umemponza.
Je, akiondolewa madarakani Tanzania tutafanyaje?
Hela tutaipata kweli? Tumuombee rais wetu Samia dili lisibume.