JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Sakata la ndoa ya mtaalamu wa tiba mbadala, Juma Mwaka maarufu Dk Mwaka na mkewe Queen Masanja, limechukua sura mpya baada ya shauri hilo kutua kwa wanasheria ambao wamepanga kulipeleka mahakamani.
Shauri hilo tayari limepita kwenye Baraza la Usuluhishi chini ya Ustawi wa Jamii na wakati wowote linatarajiwa kupelekwa mahakamani katika Kituo Jumuishi cha masuala ya familia Temeke, Dar es Salaam.
Akizungumza na HabariLEO kwa njia ya simu, Mwanasheria wa Queen, Zakia Msangi alisema shauri hilo liliondolewa katika Baraza la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) na kulipeleka katika taasisi zinazosimamia masuala ya sheria. Msangi alisema mamlaka waliyopewa Bakwata ndio hayo hayo waliyopewa ustawi wa jamii ambao wana jukumu la kuwasikiliza wanandoa na kujaribu kusuluhisha.
Alisema wanandoa hao (Dk Mwaka na Queen) hawakuonesha kurudiana hivyo wamepewa fomu namba tatu kuashiria kwamba usuluhishi umekwama hivyo shauri lipelekwe mahakamani.
Chanzo: HabariLEO