LGE2024 Mgombea akiwa hana mpinzani mpigie kura ya hapana

LGE2024 Mgombea akiwa hana mpinzani mpigie kura ya hapana

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

RMC

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2013
Posts
1,861
Reaction score
2,664
Watanganyika wenzangu

Sasa hivi kuna malalamiko kuwa wagombea wengi wa CHADEMA na wa vile vyama vya CCM B wameenguliwa kugombea. Katika kurafuta ufumbuzi baadhi wanashauri CHADENA na hivyo vyana wasusie uchaguzi. Japo mimi sio mwanachama wa CHADEMA wala hivyo vyama vya CCM B, lakini si haki kuvilaumu vyama kwani vimetimiza wajibu wao.

Ufumbuzi tunao sisi watanganyika, katika eneo lako siku ya kupiga kura ikifika nenda kituo cha kupigia kura; ukipewa karatasi ya kura na ukaona katika nafasi yeyote iwe ya nwenyekiti au wajumbe wa mtaa kuna mgombea hana mpinzani mpigie kura ya HAPANA hata kama mgombea huyo anafaa. Japo hata hizo kura za HAPANA zinaweza kuchakachuliwa lakini bado zitapekeka ujumbe kuwa watanganyika wameanza kuamka. Kwa sababu hata kama huyo mgombea anafaa inaweza ikaja siku ukawekewa asiyefaa hivyo kuwa na chaguo zaidi ya moja ni vizuri.

Wakati wa kura za maoni baadhi ya wagombea wa CCM walioongoza majina yao hayakurudi maana yake mtaa mzima mtaongozwa na mtu ambaye hakubaliki hata miongoni mwa wanaCCM na hii ni hatari Kubwa kwa demokrasia.

Mimi binafsi siku ya kupiga kura ikifika na Mungu akinijalia uzima na afya nitaenda kupiga kura na nikikuta kuna mgombea hana mpinzani hata kama anafaa vipi nitampigia kura ya HAPANA.

Wito wangu kwenu watanganyika badala ya kususia kupiga kura na kukaa kwenye key board unalaumu CHADEMA, NENDA KAPIGE KURA YA HAPANA KWA MGOMBEA ASIYE NA MPINZANI.
 
Hii inaitwa kura za maruani iliwahi kutoka zanZibar wakati wagombea wa cuf walipoenguliwa kinyume Cha Sheria
 
Nani atahesabu kura za hapana. Chini ya udhalimu wa CCM?
 
Back
Top Bottom