Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Chambusiso

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2007
Posts
2,592
Reaction score
4,640
cROPPED.jpg


Mahakama yasisitiza wagombea binafsi

na Happiness Katabazi | Tanzania Daima

Mahakama ya Rufaa Tanzania, imetupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na serikali, ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi katika chaguzi za Tanzania.

Uamuzi huo ulisomwa jana na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufaa, Ferdinand Wambali, kwa niaba ya jopo la majaji watatu, ambao ni John Mroso, Edward Rutakangwa na Engela Kileo.

Akisoa uamuzi huo, Wambali alisema jopo hilo limekubali pingamizi la upande wa mawakili wa mdaiwa, Richard Rweyongeza na Mpare Mpoki, ambao waliiomba mahakama kutupilia mbali rufaa hiyo.

Katika pingamizi hilo, Rweyongeza aliieleza mahakama ombi la rufaa la serikali limejaa dosari za kisheria, likiwemo kosa la kuandika tarehe tofauti ya tarehe ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu.

Wambali alisema wamefuta kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana baada ya kubaini mawakili wa serikali, Mwaimu na Ndunguru waliwasilisha hoja dhaifu, ambazo zimeshindwa kulishawishi jopo hilo kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Kwa sababu hiyo, jopo hili linakubaliana na pingamizi la upande wa mdaiwa, na linatupilia mbali ombi la mrufani, na linaamuru upande wa mrufani kumlipa mdaiwa gharama za uendeshaji wa kesi, alisema naibu msajili huyo.

Hata hivyo, alisema serikali inaweza kuwasilisha tena rufaa yake mahakamani kwa kufuata sheria kama itaona kuna haja ya kufanya hivyo.

Machi mwaka jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, aliwasilisha rufaa iliyopewa namba 20/2007 akiomba Mahakama ya Rufaa itupilie mbali uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuruhusu mgombea binafsi, kwa kuwa umeonekana kuwa na dosari za kisheria.

Mei 5 mwaka 2006, Mahakama Kuu chini ya jopo la majaji watatu walioongozwa na Jaji Kiongozi mstaafu, Amir Manento, waliruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi katika chaguzi kwa sababu katiba ya nchi inatoa haki hiyo. Majaji wengine walioshiriki kutoa uamuzi huo ni Jaji Kiongozi wa sasa, Salum Massati na Thomas Mihayo.

Jopo hilo lilibainisha kuwa, katiba inatamka wazi kuwa kila mwananchi anayo haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi na haiweki masharti kuwa hilo lifanyike kwa mwananchi kujiunga na chama fulani cha siasa.

Katika hati ya rufaa ya serikali, Mwanasheria Mkuu wa serikali anadai Mahakama Kuu ilikosea kisheria katika kutafsri Ibara ya 21 (1) (c), 39 (1) (c) (b) na 69 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwaka 1993, mbele ya Jaji Khawa Lugakingira (sasa marehemu), Christopher Mtikilia alishinda kesi kama hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma. Hata hivyo, Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi katika chaguzi zilizofuata, na ndipo Mtikila alipoamua kufungua tena kesi hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kushinda.

Mtikila alifungua kesi hizo akiomba mahakama itamke kwamba mabadiliko ya ibara ya 39 na 67 chini ya marekebisho ya 11 ya katiba ya nchi kuwa ni batili na kwamba itamke kuwa ibara ya 21(1) inampa haki ya kikatiba ya kuwa mgombea binafsi katika nafasi ya urais na ubunge.


Katika madai yake, Mtikila alieleza mabadiliko hayo ya katiba yanavunja haki za binadamu ambazo zimeainishwa wazi kwenye ibara 9(a) na (f), 13(2), 20(4) na 23(1) ndani ya katiba kama ilivyoainishwa kwenye tamko la haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia.
---

MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU MGOMBEA BINAFSI TANZANIA
Kwa sasa Tanzania inakabiliwa na wimbi la viongozi hasa wabunge na madiwani kuhama vyama vyao licha ya kuchaguliwa na wananchi kwa njia ya sanduku la kura

Moja ya sababu ambazo zinatajwa na wanaohama ni matatizo yaliyomo katika vyama hivyo au kuunga mkono juhudi za Rais

Napendekeza kabla ya 2020 serikali ibadilishe sheria awepo mgombea binafsi, wananchi wenye uwezo wa kuongoza waweze kuchaguliwa na wananchi bila kuzingatia chama anachotoka ili kuepuka gharama za kurudia uchaguzi wa mara kwa mara kwa kile kinachoitwa hama hama kwenye vyama vya siasa

Itaondoa ukiritimba wa watu kuchaguana kwenye vyama vya siasa kwa kujuana na kupitishwa bila kupingwa

Itaondoa chuki ya kivyama,watu kwa sasa wanabaguana hadharani na kuonyesha chuki kwa wananchi wanaoshabikia chama Fulani

Na mwisho itawapa mwanya vijana wengi kujitokeza kugombea nafasi hizo bila vipingamizi ikizingatia kipindi hiki ambacho ajira ni ndogo sana

Nchi nyingi kwa sasa wameruhusu mgombea binafsi kwa hivyo kwa pamoja naomba tuungane kupigania mgombea binafsi ili tuachane na ushabiki wa vyama vya siasa hata hivyo yawezekana bila kutarajia ukawa mbunge au diwani kupitia mgombea binafsi kama Kijana huyu

View attachment 834491
===
wanajamvi habari za mda huu? mimi naenda moja kwa moja kwenye mada je tunapataje mgombea binafsi maana mimi naona mambo ya vyama ni vurugu tupu mpaka sina hata matumaini yeyote kwa nchi yangu kupata watu wanaoweza kutufikisha mahali pazuri yaani naona watu wamekata tamaa sana.

CCM hawapambani na umaskini wa watanzania bali wanapambana na cdm namna ya kuimaliza ili kusiwe na kelele. lakini ingekuwa inajitahidi sawa badala yake ni uporaji na ufisadi kwa kwenda mbele.

mwaka huu tumeshuhudia mpaka ukaguzi wa CAG umeshindikana kusomwa bungeni kisa tumepigwa na wajanja mpaka aibu tri.1.6 haionekani. kwa awamu hii ni aibu sana maana wamejinasibu wanatokomeza ufisadi lakini ndo wamepigwa vibaya sana.

Sisi tunaowajua ccm tulijua mambo ni mbele kwa mbele ndo maana tunawaza sana sana labda mgombea binafsi atakuwa suluhisho.
---
MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU

Tuangalie katiba inasemaje kuhusu mgombea urais na ubunge

Ibara ya
39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-

(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipakodi yoyote ya Serikali.

Ibara ya 67

.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-

(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;

(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote

ya Serikali
===
Mtoto,

Mkuu wangu mimi sii mwanasheria isipokuwa natumia logic ktk tungo ya sheria tunazozungumzia..
hakuna interpretation yangu isipokuwa ni kufahamu kwamba Demokrasia inaanza na vyama sii wingi wa watu kugombea nafasi za uongozi. Chama kimoja kinachosimamisha wagombea mia kam wakati wa Nyerere haikuwa demokrasia ingawa kisheria nayo ingesema sawa na ibara inayoruhusu mtu kugombea na kupiga kura.

Kwa hiyo ukifahamu kwamba demokrasia yetu na inatokana na Vyama, ndio maana tukawa na sheria ya vyama vingi na sio sheria ya muundo wa wagombea wengi ilotangulia...Hivyo, sheria zote zinazoambatana na uchaguzi huzungumzia vyama na wagombea ni kati ya watu wanaogombea kupitia ticket za vyama na wananchi kuchagua viongozi wanaopita kwa ticket ya Chama..unapo cast Ur vote unapomchagua mtu unakichagua chama moja kwa moja..

Hivyo basi hata wagombea binafsi hutakiwa kuandaa chama (mrengo) fulani kiaina hata kama wajiite independent, Utakuta mtu huyo (kiti cha Urais) atasimamisha wabunge wakiwakilisha Independent na kadhalika na hata huyo mpiga kura huchahua mgombea wa Independent kwa sababu lengo kubwa la uchaguzi mkuu ni tofauti za itikadi zinazowakilishwa na kundi moja tofauti na jingine na sii mtu mmoja tofauti na mwingine.. Chama ndio alama ya mrengo chama ndicho kinachokupa sura ya imani utakayofuata na sii mtu au sura ya mtu.

Kifupi mkuu wangu wewe unaweza kuwa Mkristu au Muislaam hivyo tafsiri yake ni kwamba una dini.. unaruhusiwa kuamini, kuabudu na kusali lakini kama huna dini wewe ni Kafiri..Unapofungua kanisa lako tafisri yake itakuwa ngumu sana ikiwa bado unakataa kwamba huna dini..sasa kufungua kwako kanisa au msikiti na kujiita Sheikh una maana gani! unataka kuwaongoza watu wenye imani gani?

Hivyo sheria yetu kifungu 21 kinatafrisika vibaya na wanasheria wetu kwa sababu hawafahamu Demokrasia yetu imetokana na kitu gani......tumetoka wapi ndilo somo -Toka chama kimoja kuwa vyama vingi, ndio kichwa cha habari nzima ya uchaguzi na mfumo wa demokrasia yetu..Hao mahakimu wenyewe wamechukua shahada zao nchi za Kikomunist! Lol!

Bila shaka nimejieleza na umenielewa..

kama alivyosema John Tendwa (msajili wa vyama vingi), sheria yetu inatakiwa marekebisho.
Hapa hakuna tafisri inaonyesha wazi katiba ina mapungufu period hakuna kutafsiri vinginevyto.

Lakini hata haya marekebisho hayawezi kuja kirahisi kwani Wagombea binafsi nchini wanataka kuingia katika chaguzi hizi wakiwa mikono mitupu yaani hawana mrengo unaoeleweka, basi iwe hata swala moja tu..mfano, kupigania haki ya mazingira, au against Ufisadi ndio swala lao kubwa itaeleweka kwamba wanasimamia maslahi gani na wananchi watawachagua kwa sababu hiyo!

lakini sio sura mkuu wangu hizi habari za kuiuza sura watu wapige kura ni kufilisiana..
===
Field Marshall ES,

Kuna sheria nyingine si lazima ziainishwe kwa kutungwa na bunge. Kuna sheria nyingine zinatoka moja kwa moja kwenye katiba.

Ndiyo maana nikasema Mtikila ana bonge la kesi, kwa sababu katiba imetoa sifa za mtu kupiga au kupigiwa kura, awe Mtanzania aliyefikisha umri fulani na asiye na matatizo ya akili etc etc. Katiba haikusema kwamba lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa.

Kwa hiyo utaona sheria ya kuruhusu wagombea binafsi Tanzania ipo katika katiba, na hili la kuzuia wagombea binafsi linakwenda against the spirit if not the letter of the constitution.

Sasa kukataza wagombea binafsi either kunakuwa unconstitutional, au kunaleta a constitutional crisis.
===
Uchuro wa watendaji serikali ya Tanzania.

Kazi ya kutafsiri mikataba na kutafsiri sheria kwa vitendo ni ya Mahakama. Hakuna chombo kingine chochote klicho na uwezo wa kutafsiri sheria zaidi ya Mahakama.

Bunge lina uwezo wa kutunga sheria na kwa kiwango fulani kidogo kutafsiri sheria hizo kupitia kamati zake. Kwa sababu bunge limejaa watu wenye agenda za kisiasa Bunge si mahali penye usahihi wa 100% wa kutafsiri sheria.

Majaji hawapigiwi kura, majaji hawana agenda za kisiasa wala hawaogopi matokeo ya maamuzi yao ya kisheria. Jaji ni jaji mpaka astaafu au afe. Nguvu ya Jaji iko ndani ya sheria na kazi yake ya ujaji na si katika chombo fulani au kundi fulani la watu au Wahuni ndani ya serikali.

Nguvu ya mbunge iko kwenye siasa na si kazi aifanyayo ya kutunga sheria. Nguvu ya Mbunge ina ukomo wa Muda wa miaka 5. Mbele ya sheria mbunge ni mtu anayejichanganya kimaslahi. Siku zote mbunge atachagua siasa kuliko kuchagua kutunga sheria aua kuimarisha sheria kwa manufaa ya taifa.

Mahakama ni chombo pekee kisicho cha kisiasia chenye uwezo na mamlaka yakutafsiri sheria bila kuwa kujikanganya kimaslahi kama Bunge.

Taarifa ya serikali imejaa siasa na ulevi wa madaraka kama siyo ununda na umbumbu wa katika nyanja za haki za kikatiba kwa kila mwananchi.

Mtu binafsi kugombea nafasi ya uongozi havunji katiba ya Tanzania kwa sababu katiba inasema kila mtu ana haki ya kushiriki katika siasa kama mtu.

Kwa hiyo vifungu vingine vinavyo mlazimisha Mtanzania kushiriki katika siasa kupitia makundi ya kichama ni vifungu vinavyo kwenda kinyume kabisa na haki ya kisiasa aliyonayo Raia Mwema.

Safari hii serikali wamekuja na Gia kwamba Mahakama haina uwezo wa kutafsiri na kuamuru sheria fulani ndani ya katiba ibadirishwe kwa sababu inapingana na sheria mama ya haki ya Mtanzania katika kushiriki siasa.

Ni serikali hii hii imekiri wazi kwamba haina uwezo wa kuandika mikataba ya maana kati yake na Wachimba Madini Wafua Umeme na wafanyi biashara wengi kutoka nje na ndani kiasi cha kusababisha upotevu wa Mabilioni ya Dola huku watendaji haohao wakitajirika Overnight kwa kujijazia vijisenti kwenye account za nje.

Kwa nini leo hiii wanakuja na Gia kubwa kwamba wana uwezo wa kujua kwamba Mahakama haina nguvu za kuingilia kati vifungu vyenye utata ndani ya katiba?

Hivi Jopo la majaji na wanasiasa hawa wasio na uwezo wa kuandika mikataba yenye kunufaisha taifa nani ana jua sheria zaidi?

Watendaji wengi wa serikali wanajificha nyuma ya serikali kuendeleza sheria za kikandamizaji ili kundi lao la Mharamia ndani ya CCM liendelee kuongoza kwa nguvu ya Rushwa ndani ya vikao vya ndani vya CCM vilivyo jaa manyang'au wenye hamu na kiu kuharibu bila faida kwao wala kwa vizazi vyao.

Mjumbe wa Kikao ndani ya CCM ukipewa Tshs 75,000.00, ukalipiwa Guest house kwa siku 7, ukapewa Ulabu na Huduma ya MaChangu Doa au Vijust ili umchague Fisi kuwa mbunge, wewe unapata nini? Mkeo au Mumeoanapata nini? Binti yako ana pata nini?

Ukichukua hiyo 75,000/(365X5) kila siku ni sawa na kulipwa Ths 4.10 na wasiwasi wa kukwaa miwaya?

Hivi watanzania ndani ya CCM bei yenu kwa siku ni ndogo namna hiyo?
Shs 4 mpaka 1000 kwa siku zina kufaa nini?

Hata hiyo Fisi akiwapeni Rushwa ya Tshs 1,825,000.00 ni swa na kujipatia 1000 kwa siku kwa muda wa miaka 5. fedha hiyo ni ndogo sana ukilinganisha na vurumai na dharau kubwa tupewao na Wabunge wahuni na wanyonge waliojaa ndani ya Bunge la Tanzania.

Serikali yetu imejaa wasomi walioacha elimu yao yote mashuleni na kuondoka na kiburi cha shule tu.
Wengine kama yule naibu waziri wa ulinzi mtani wangu mngoni ni Ma Dr Vihiyo wa kununua vyeti.
Serikali yetu imejaa watu waliokua vimbelembele wa kutaka na kulilia umonita darasani na kung'ang'ania kugawa msosi kila siku ili wajijazie bondo la kutosha kwenye shani zao.

Serikali yetu imejaa wasomi vipanga na manunda wa kutaka ujiko kwenye kila kitu.

Labda safari hii watashinda hasa ukizangatia mahela mengi waliyoiba na wanayoendelea kuiba.
Ukiwa na fedha siunapata uwezo kumnunua kila mtu?.

Labda safari hii wanunue majaji wote kwenye jopo, kinyume cha hapo ushindi wa kesi hii muhimu bado ni Mtikilia.

Mh Chilawe bado una kazi ya kutekeleza hukumu hii.

Unataka au huna taka.
===
CCM na serikali yao lazima wapinge hiyo interpretation. Sababu ni simple, strategy imekuwa hivyo tangu tupate uhuru. Otherwise isingekuwa inawezekana kwa mtu mmoja, asiyekuwa na elimu yoyote ya kutosha, lakini anayo kadi ya chama, anakuwa waziri wa wizara saba(7!) tofauti ktk muda wa karibu miaka 30!
Hii haitokei popote duniani zaidi ya Tanzania! Ukitafuta kwa nguvu sana, unaweza kuikuta North Korea, Cuba, Syria, n.k.

Kwa ufupi katiba yote ya JMT inahitaji kubadilishwa, kwani ndiyo imekuwa ikitudumaza kwenye maendeleo tangu tulipoanza. Kwa kutumia udikteta wawe, baba wa taifa alijilimbikizia madaraka yote mikononi mwake, akidhani kuwa atakuwa "effective" ktk kutimiza "ndoto" zake za ujamaa wa kiafrika.

Alisahau au hakujua mambo mengi ambayo ni muhimu na hayabadilishiki, miongoni mwao kuwa hatoishi milele, na pia hao wakoloni wamekamata mpini na yeye na wenzie wamekamata makali. Matokeo yake tunayavuna hadi leo.

Waziri anapopinga interpretation ya High Court, anasisitiza uwiano uliopo uendelee kuwapo ambapo CCM wanamiliki kila kitu, kila mtu, kila sheria, kila uamuzi, kila uchaguzi.
Idumu CCM!! Idumu CCM! Idumu CCM! Wadumu MAFISADI!!!
===
- Ninakumbuka siku moja huyu waziri akiniambia maneno haya haya one on one, kwamba ni bunge tu ndilo lina power kikatiba kubadilisha au kuidhinisha wagombea huru, na alisema kwamba mara baada tu ya ile hukumu ya Mtikila, serikali ilikata rufaa, lakini mpaka leo mahakama imekua ikikwepa hii kesi kwa sababu ya kuogopa aibu, maana walijua wamechemsha na ile hukumu sasa naona amerudia tena maneno yale yale,

- Niliwahi kumuuliza kiongozi mwingine wa juu wa serikali ya sasa kwamba CCM wanaogopa nini na hili la Independent Candidates? Akasema kwamba moja ya sharti kubwa la Afro Shirazi Party, Visiwani on Muungano ilikuwa kwamba Bara watahakikisha kwamba hilo halitakuja kutokea under their watch, yaani CCM, na siku likitokea itakua ndio mwanzo na mwisho wa Muungano, kwa sababu wanaogopa Sultani atarudi kirahisi sana, kama independent Candidate sijui how much true is this, lakini mpaka leo sioni sababu ya msingi kwa CCM kuikataa hii hoja, kwa sababu hata ikikubaliwa wanaweza kuitumia sana kwa their advantage,

- Ingawa binafsi siamini kwamba hii hoja ndio hasa the answer to our national political na legal misery tuliyonayo sasa, dawa ni kurekebisha katiba tuliyonayo maana iliundwa purposerly for one party rule sio vyama vingi, sijui ni lini wa-Tanzania tutakuja kulielewa hili na kulifanyia kazi!.

Respect.

FMES!
===
Kuna mwanasheria maarufu sana wa Uingereza aliyesema " The Law is an Ass".
Kila mtu aweza kumpanda.

Lakini sheria haitekelezeki in a vaacum, inatekelezeka katika jamii inayoimiliki sheria hiyo.
Si nia yangu kuiponda sheria lakini kwa society za third world the Law must be an Ass ambayo inapandwa kwa uangalifu ukijua kule unakoelekea usije anguka.

Na ndio maana leo mwafrika aliyekuwa naturalised katika nchi nyingi tu za Ulaya kupata nafasi ya uwakilishi katika mabunge ya huko , au Uwaziri Mkuu, au Urais ni ndoto.

Tu kitazama sheria yetu na udhibiti wa private canditaes inabidi tutazame upande wa pili wa uhuru huo ambao wengi humu JF wanaushabikia lakini mwisho wake hauna tija. Tutazame scenarios vis-a-vis the Tanzanian palying field,

1 Private candidate itabidi awe na mtaji wa kutosha kuelezea sera zake katika jimbo au nchi nzima
(iwe uchaguzi wa ubunge au wa urais).

2 Private candidate huyu lazima awe na mtandao-si lazima uwe wa kisiasa, kueneza uwezo wake.

3 Watanzania walio wengi, wapiga kura ni masikini sana, na wananunulika kama uzoefu wetu ulivoonyesha katika matukio mengi ya uchaguzi wa kisiasa.

Sasa hivi kuna tatizo kubwa la mafisadi kujipenyeza katika uongozi wa vyama mbalimbali na matokeo yake yanaonekana ikiwa ni pamoja na migongano isiyo ya lazima.

Sasa wana JF nauliza , kisheria , utamzuiaje mtu kama Rostam kuwania Urais akitaka kufanya hivyo as a private candidate?

4 Private candidate huyu na mtandao wake lazima arudishe fedha yake atakapopata madaraka
===
Ogah,
Kwamba Mahakama Kuu ilitengua katiba hilo hata hawabishani. Majaji walitegua kipengele vitatu:

Na, jaji Masati, akiandika kwa niaba ya jopo wala hakuficha kwamba, naam, sasa tunatengua katiba:

Vipengele vilivyotenguliwa na mahakama vilichomekwa kinazi kwenye Katiba katikati ya kesi ya kwanza, mwaka 1993, wiki moja kabla ya hukumu ya hayati jaji Lukakingira alipokubali pingamizi la Mtikila dhidi ya sheria inayotakataza ugombea binafsi. Hivyo, hukumu dhidi ya serikali, kwamba sheria ya uchaguzi ni kinyume cha Katiba, ikawa haina nguvu kwa vile serikali ilishajiwahi kuburuza muswada wa kubadili Katiba ili hiyo sheria ya uchaguzi ikubalike.

Mtikila aliporudi safari ya pili akadai kwamba marekebisho ya Katiba yaliyopitishwa kumzuia asigombee binafsi ni batili. Athari ya mabadiliko hayo, akasema, ni kumlazimisha kuingia kwenye chama wakati Katiba ilikuwa inapiga marufuku kulazimishana hivyo, isitoshe Katiba inaruhusu yeyote kushiriki utawala wa nchi ``moja kwa moja.``
Mahakama Kuu ikakubaliana nae kwamba serikali haina nguvu kuchomeka mabadiliko ya Katiba yanayoondoa haki za msingi zilizokuwepo awali. Hivyo mwaka 2006 majaji wakafuta vipengele vipya vilivyochomekwa kwenye Katiba, kwamba ni unconstitutional. Mtikila akawa two for two, kashitaki mara mbili kashinda mara mbili.

Sasa serikali inakwenda Mahakama ya Rufaa kupinga kitendo cha Mahakama Kuu kubadili Katiba. Serikali inadai 1) walipochomeka kipengele cha katiba kuzuia mgombea binafsi walikuwa ndani ya mipaka yao kwa mujibu wa Katiba, 2 ) Bunge ndio lina nguvu ya kubadilisha Katiba, sio Mahakama.
Swali ni, jee, Mahakama ina nguvu kutengua katiba? Kama inayo, serikali inasema mwishowe majaji wanaweza kukadilisha Katiba nzima. (Kumbuka hawabishani kama ilitengua au haikutengua.)

Kawaida Katiba ni ya watu, inatoka kwa watu, kwa ajili ya watu. Kupitia wawakilishi. Inawezekana Mahakama ya Rufaa ikakubaliana na serikali kwamba wao, majaji, hawana nguvu kutangua Katiba.
===
Dilunga,
Asante sana mkuu Dilunga. Hivi viraka vilivyochomekwa ni uzandiki, uhuni, ubabe na kila aina ya uchafu unaoweza kutaja. Sheria mama inasisitiza "uhuru" wa kuhusiana, kuchagua, kuchaguliwa na kushiriki katika mambo yote yanaoihusu jamii. Hili lakusema huwezi kufanya hiki ama kile linatoka wapi? Vinginevyo warudi kwenye meza ya kuchorea (drawing board) waondoe hicho kifungu kinachotoa huo uhuru ndipo wakazie hivyo vifungu vya kiendawazimu.

Mkandara, kuwepo kwa sheria hakumaanishi hata kama ni ya kijinga lazima tukubali tu. Hii sheria haikuwepo kama Dilunga alivyoonyesha na kwa uhakika haitakiwi kuwepo maana ni ya kibazazi kulinda maslahi binafsi.

Kwa ufupi mahakama kuu haikukosea ila jaji alipitiwa kusema anatengua kifungu hicho bali alitakiwa kusema anakifuta na kuwarejesha kwenye sheria mama kwenye katiba. "Uhuru wa ku...."

Pia Soma:
1) Serikali yaamriwa kuanzisha mchakato wa mgombea binafsi, ni baada ya Mtikila kushida kesi

2) Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya Africa
 
Wind of changes is blowing everywhere! This is a good start to our Judges,While the king is seated at his table, the spices has send out their perfum to people.

Bravo.
 
Sasa CCM wakae chonjo maana wagombe binafsi watatokea hukohuko CCM baada ya kuachwa kwenye kura za maoni. inawezekana utabiri wa Mwalimu unakaribia kukamilika kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM.
 
Hapo katikati niliwahi kusema kwamba JK alikuwa hapati usingizi kwa neno mgombea binafsi. I hope sasa kwamba ameridhika kwamba maamuzi ni sahihi na Lunyungu nitasimama Kibaha maana nimekaa sana hapa.

CCM naamini wameumia na hawana namna sasa .Wale wote wanao kimbilia Vyama sasa wameanguka chali. Vurugu zote za vyuoni na CCM kwisha kabisa.

Hongera Majaji.
 
Mahakama sasa imeendelea kushinikiza uwepo wa wagombea binafsi!

Kwa wale waelewa wa siasa..Tunaweza kusema kuwa ugombea binafsi ni jambo la kidemokrasia!

Lakini kwa upande mwingine..Haki hii ya ugombea binafsi imekuwa ikikinufaisha iether chama kimoja cha kisiasa ama kingine!

Kwamba mara nyingi si wagombea binafsi ambao wananufaika binafsi bali vyama vilivyoko kwenye kinyang'anyiro!

Tumeshaona mifano halisi kama vile Ralph Nader ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kwa Al Gore kwenye uchaguzi wa USA 2000!

Swali sasa linakuja kwenye siasa zetu Tanzania.

Je, kuna chama kitakachonufaika na uamuzi huu wa mahakama hapo baadae?
 
Tumeshaona mifano halisi kama vile Ralph Nader ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kwa Al Gore kwenye uchaguzi wa USA 2000!

pamoja na kushindwa kwa Al gore mwaka 2000, hii haiondoi umuhimu wa mgombea binafsi, inapotokea vyama vikawa na mizengwe ni rahisi kwa mtu mwenye uwezo kusimama kuomba kura za wananchi akiwa kama mgombea binafsi.

pili hii itasaidia kuvipa vyama discipline, badala ya ukiritimba wa kimaamuzi wa baadhi ya vigogo katika vyama kuwawekea vikwazo washindani wao kisiasa ndani ya vyama hivyo, itabidi wajiulize mara mbili mbili kwa sababu ukimkwaza mtu anakwenda zake kusimama kama mgombea binafsi.

tatu hii inapanua demokrasia katika jamii, haiwezekani mtu asiyekuwa na chama aweze kupiga kura kuchagua wenye vyama halafu eti na yeye akose haki ya kuchaguliwa.hii ilikuwa hai make sense.
 
ni suala zuri na kupanuka kwa demokrasia.

hata Mwanakijiji anaweza kugombea bila ya chama maana Mbowe hatokubali kumwachia kiti.
 
Gamba la Nyoka,

Nakubaliana na wewe lakini kuna watakaoitumia kwa nia mbaya ya ku divide kura ili kumfanya mwingine ashinde!

Lakini si ndio demkrasia hiyo? Hapa bottom line itategemea na uelewa wa wananchi kwenye suala husika.
 
Nadhani hii ni habari njema na ni habari yenye uzito mkubwa sana katika Tanzania yetu.

Wambali alisema wamefuta kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana baada ya kubaini mawakili wa serikali, Mwaimu na Ndunguru waliwasilisha hoja dhaifu, ambazo zimeshindwa kulishawishi jopo hilo kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Naona upande wa serikali expectedly, umepewa rukhusa ya kuweza kukata rufaa... nevertheless, the fact that wanasheria wa serikali walichemka katika procedure basic kama hizo walipowasilisha kesi, ni jambo ambalo linaonesha ukurupukeni wa serikali kupitia mawakili wake na si kinginecho...

SteveD.
 
Kuna watu wengi sana wenye uwezo wa kuiongoza nchi yetu lakini wamechoshwa na siasa za CCM na Upinzani na labda wana haki ya kuwa wagombea binafsi!
 
Kama mambo yasipobadilika kama wananchi wanavyoambiwa wasubiri yatabadilika..Kama vile kuwatia nguvuni mafisadi..Then usishangae wengi wetu wakimu endorse mgombea binafsi atakaye fuata matakwa ya wananchi!
 
stage ya pili tunataka mawaziri wasiwe wabunge. Maana yake mtu mmoja, mfano waziri kutoka CCM, yeye ni waziri, yeye ni member wa nec, yeye ni mbunge, yeye ni mkurugenzi wa makampuni na mashirika ya umma kadhaa, yeye ni kiongozi wa familia.

demokrasia inapanuka, na ipanuke katika mengi
 
stage ya pili tunataka mawaziri wasiwe wabunge.
manake mtu mmoja, mfano waziri kutoka ccm, yeye ni waziri, yeye ni member wa nec, yeye ni mbunge, yeye ni mkurugenzi wa makampuni na mashirika ya umma kadhaa, yeye ni kiongozi wa familia. ..........
demokrasia inapanuka, na ipanuke katika mengi

Hapo kwenye highlight naweza kukubaliana na wewe kwasababu moja kubwa..

Wabunge wanapopewa uwaziri mara nyingi tumekuwa na frikra kuwa sasa kwa sababu katokea jimbo fulani. Basi atafanya majukumu yake kwa kubase zaidi kwenye jimbo lake na ndio maana tuna tabia ya kuwafagilia hata kama ni mafisadi!

Juzi tu hata Pinda alipoteuliwa kwenye nafasi ya uwaziri mkuu..Maneno yakaanza kuwa eti sasa RUKWA ITAKUMBUKWA!

Yani Rukwa ilisahauliwa kwasababu eti haikuwahi kutoa waziri mkuu?
Hizi ni issue za kuzitupia macho!
 
stage ya pili tunataka mawaziri wasiwe wabunge.
manake mtu mmoja, mfano waziri kutoka ccm, yeye ni waziri, yeye ni member wa nec, yeye ni mbunge, yeye ni mkurugenzi wa makampuni na mashirika ya umma kadhaa, yeye ni kiongozi wa familia. ..........
demokrasia inapanuka, na ipanuke katika mengi

Na hapo ndio umemaliza mchezo mkuu Gaijin!
 
High Court has no powers to rule on independent candidates, says minister​

ALVAR MWAKYUSA

THIS DAY

Dar es Salaam

THE government has explained why it is intending to appeal against a High Court ruling in favour of private candidates.

The Minister for Justice and Constitutional Affairs, Mathias Chikawe, told THISDAY in Dar es Salaam earlier this week that the intention to appeal is based on the belief that the High Court over-stepped its authority in giving the ruling.

We will be appealing against the powers of the court in this matter. We are questioning whether the High Court has the mandate to alter sections of the national constitution, Chikawe said.

If this trend is left to continue, the court could alter the whole of the constitution, the minister asserted, while at the same time striving to emphasize that the government is not against independent candidates.

According to Chikawe, courts of law are supposed to interpret the laws of the land in resolving cases � but not to alter the laws.

The High Court recently ruled in favour of the removal of restrictions preventing people not affiliated with any political parties from running for the presidency or parliamentary seats during general elections.

The court directed the Attorney Generals Chambers to put in place a legislative mechanism to regulate the activities of non-party candidates in next years elections.

Efforts to get a comment from Attorney General Johnson Mwanyika were not successful as he was said to have travelled out of the country, while his deputy was said to be in Zanzibar on official business.

In its ruling, the High Court declared as unconstitutional the 1994 Election Law stipulating that anyone wanting to contest political posts must be members of a registered political party.

The court said some articles in that law were unnecessary and unreasonable, only serving to restrict the fundamental rights of the citizenry to vie for elective political posts either as party members or as private candidates.

It was the second time the High Court has ruled in favour of independent candidates. In 1994, the late Justice Rugakingira declared that it should be lawful for independent candidates, along with candidates sponsored by political parties, to contest presidential, parliamentary and local council elections held in the country.
 
Uchuro wa watendaji serikali ya Tanzania.

Kazi ya kutafsiri mikataba na kutafsiri sheria kwa vitendo ni ya Mahakama. Hakuna chombo kingine chochote klicho na uwezo wa kutafsiri sheria zaidi ya Mahakama.

Bunge lina uwezo wa kutunga sheria na kwa kiwango fulani kidogo kutafsiri sheria hizo kupitia kamati zake. Kwa sababu bunge limejaa watu wenye agenda za kisiasa Bunge si mahali penye usahihi wa 100% wa kutafsiri sheria.

Majaji hawapigiwi kura, majaji hawana agenda za kisiasa wala hawaogopi matokeo ya maamuzi yao ya kisheria. Jaji ni jaji mpaka astaafu au afe. Nguvu ya Jaji iko ndani ya sheria na kazi yake ya ujaji na si katika chombo fulani au kundi fulani la watu au Wahuni ndani ya serikali.

Nguvu ya mbunge iko kwenye siasa na si kazi aifanyayo ya kutunga sheria. Nguvu ya Mbunge ina ukomo wa Muda wa miaka 5. Mbele ya sheria mbunge ni mtu anayejichanganya kimaslahi. Siku zote mbunge atachagua siasa kuliko kuchagua kutunga sheria aua kuimarisha sheria kwa manufaa ya taifa.

Mahakama ni chombo pekee kisicho cha kisiasia chenye uwezo na mamlaka yakutafsiri sheria bila kuwa kujikanganya kimaslahi kama Bunge.

Taarifa ya serikali imejaa siasa na ulevi wa madaraka kama siyo ununda na umbumbu wa katika nyanja za haki za kikatiba kwa kila mwananchi.

Mtu binafsi kugombea nafasi ya uongozi havunji katiba ya Tanzania kwa sababu katiba inasema kila mtu ana haki ya kushiriki katika siasa kama mtu.

Kwa hiyo vifungu vingine vinavyo mlazimisha Mtanzania kushiriki katika siasa kupitia makundi ya kichama ni vifungu vinavyo kwenda kinyume kabisa na haki ya kisiasa aliyonayo Raia Mwema.

Safari hii serikali wamekuja na Gia kwamba Mahakama haina uwezo wa kutafsiri na kuamuru sheria fulani ndani ya katiba ibadirishwe kwa sababu inapingana na sheria mama ya haki ya Mtanzania katika kushiriki siasa.

Ni serikali hii hii imekiri wazi kwamba haina uwezo wa kuandika mikataba ya maana kati yake na Wachimba Madini Wafua Umeme na wafanyi biashara wengi kutoka nje na ndani kiasi cha kusababisha upotevu wa Mabilioni ya Dola huku watendaji haohao wakitajirika Overnight kwa kujijazia vijisenti kwenye account za nje.

Kwa nini leo hiii wanakuja na Gia kubwa kwamba wana uwezo wa kujua kwamba Mahakama haina nguvu za kuingilia kati vifungu vyenye utata ndani ya katiba?

Hivi Jopo la majaji na wanasiasa hawa wasio na uwezo wa kuandika mikataba yenye kunufaisha taifa nani ana jua sheria zaidi?

Watendaji wengi wa serikali wanajificha nyuma ya serikali kuendeleza sheria za kikandamizaji ili kundi lao la Mharamia ndani ya CCM liendelee kuongoza kwa nguvu ya Rushwa ndani ya vikao vya ndani vya CCM vilivyo jaa manyang'au wenye hamu na kiu kuharibu bila faida kwao wala kwa vizazi vyao.

Mjumbe wa Kikao ndani ya CCM ukipewa Tshs 75,000.00, ukalipiwa Guest house kwa siku 7, ukapewa Ulabu na Huduma ya MaChangu Doa au Vijust ili umchague Fisi kuwa mbunge, wewe unapata nini? Mkeo au Mumeoanapata nini? Binti yako ana pata nini?

Ukichukua hiyo 75,000/(365X5) kila siku ni sawa na kulipwa Ths 4.10 na wasiwasi wa kukwaa miwaya?

Hivi watanzania ndani ya CCM bei yenu kwa siku ni ndogo namna hiyo?
Shs 4 mpaka 1000 kwa siku zina kufaa nini?

Hata hiyo Fisi akiwapeni Rushwa ya Tshs 1,825,000.00 ni swa na kujipatia 1000 kwa siku kwa muda wa miaka 5. fedha hiyo ni ndogo sana ukilinganisha na vurumai na dharau kubwa tupewao na Wabunge wahuni na wanyonge waliojaa ndani ya Bunge la Tanzania.

Serikali yetu imejaa wasomi walioacha elimu yao yote mashuleni na kuondoka na kiburi cha shule tu.
Wengine kama yule naibu waziri wa ulinzi mtani wangu mngoni ni Ma Dr Vihiyo wa kununua vyeti.
Serikali yetu imejaa watu waliokua vimbelembele wa kutaka na kulilia umonita darasani na kung'ang'ania kugawa msosi kila siku ili wajijazie bondo la kutosha kwenye shani zao.

Serikali yetu imejaa wasomi vipanga na manunda wa kutaka ujiko kwenye kila kitu.

Labda safari hii watashinda hasa ukizangatia mahela mengi waliyoiba na wanayoendelea kuiba.
Ukiwa na fedha siunapata uwezo kumnunua kila mtu?.

Labda safari hii wanunue majaji wote kwenye jopo, kinyume cha hapo ushindi wa kesi hii muhimu bado ni Mtikilia.

Mh Chilawe bado una kazi ya kutekeleza hukumu hii.

Unataka au huna taka.
 
Last edited:
Kama ni kwa hoja serikali imeshindwa kwa sababu hata bwana Waziri hapa anachoonyesha ni kuwa tatizo lao si hoja ya mgombea binafsi, bali uwezo wa mahakama kutoa amri kuhusiana na hoja hiyo.

Namshukuru sana bwana waziri kwa kuonyesha kuwa hoja hii imeshinda, sasa wanataka kuipinga kwa vioja. Tusonge mbele
 
Back
Top Bottom