Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Ni nini hasa wasiwasi wa Serikali kukubali yaishe?

Nini maana ya Mihimili mitatu ya Dola kama Mahakama haina sauti ya kusikilizwa?

Nadhani imefika wakati Mahakama nayo isimame kidete kusimamia utekelezaji wa Maamuzi au Hukumu zake badala ya kuziachia njiani zime-hang. Huwezi ukaihukumu Serikali kisha utegemee isimamie hukumu kwa haki.

Something need to be done here.
 
Kama ni kwa hoja serikali imeshshindwa kwa sababu hata bwana waziri hapa anachoonyesha ni kuwa tatizo lao si hoja ya mgombea binafsi, bali uwezo wa mahakama kutoa amri kuhusiana na hoja hiyo. Namshukuru sana bwana waziri kwa kuonyesha kuwa hoja hii imeshinda, sasa wanataka kuipinga kwa vioja. Tusonge mbele

Mimi naona 'sense' ya waziri ni kusema kuwa wamekata rufaa mahakama ya rufaa. Lakini kuhoji uwezo wa mahakama kuu hapo sioni hoja. Yeye angeridhika kuwa kama serikali imekata rufaa inaamini ilichokipinga ni sahihi na kitaamuriwa na mahakama ya rufaa.

Lakini kusema mambo yakiachwa hivyo eti mahakama kuu itaweza kubadili katiba yote si kweli. Interpretaion of the law includes also what the High Court has done since a court of law interprets the law in light of the whole constitution. Alichokisema waziri ndicho kinachoitwa kuingilia uhuru wa mahakama.
 
Huyu judge kwa nini hakuweka muda wa hili jambo kushughulikiwa? CCM hapa wanacheza mchezo tu; wanataka hata wakishindw akusiwe na nafasi ya kufanya maandalizi kuruhusu independent candidates.

Iweje case ambayo hukumu ilitoka miaka kama mitatu au minne, wanakuja kukata rufaa leo?
 
Madela Wa- Madilu,

Umeandika fresh sana, i couldn't have put it any better. Lakini swali langu ni nani anachagua ma-judge? Sio kiongozi wa serikali...aka rais. Sasa huoni tayari influence fulani hapo katika judiciary. Hakuna total separation of power. Ukitaka kujua cheki selection ya supreme court judges marekani inavyokuwa influenced na chama tawala.

Lakini point yako ni sawa kabisa. Huyu judge ametafsiri sheria ya 'haki ya kushiriki katika siasa' kana kwamba ina upeo mkubwa kuliko uhuru wa kutoa hoja peke yake. Sasa kama wanataka, wabadilishe katiba na kuweka hiyo limitation. Ama sivyo, mahakama haijafanya kosa lolote. Waka-appeal hiyo hukumu...ni haki yao pia.

Pia huyo judge amefanya kazi yake na huyu waziri, kama mkono mwingine wa utawala(serikali), hatakiwi kusema kuwa kakosea. Hiyo itafanya wananchi kuona kama ma-judge hawafanyi kazi zao na kukosa imani nao. Lazima mikono yote mitatu ya utawala, mahakama, serikali na bunge viache kila kimoja kifanye kazi yake. Wanaoweza kutupiana maneno machafu ni bunge na serikali kwa maana wao ni wana-siasa.
 
Serikali ya CCM ina dilly-dally tu, ili ikifika October 2010 suala liwe bado mahakamani na CCm iweze 'kutesa' kwa kishindo ktk uchaguzi. Hiyo sheria ya wagombea binafsi ikiwepo, the big casualty atakuwa CCM, period.

Watanzania tunaendelea tu kukorogwa na watu wachache (ktk CCM) kuonyesha eti wananchi wengi wanaipenda CCM katika ballot box. Sheria tu ndizo zimekaa ovyo ovyo kuinufaisha CCm na chama hichi kinataka hali iendelee kuwa hivyo tu.

Aliyeanzisha hili suala mahakamani, Mchungaji Mtikila alisha nunuliwa na mafisadi, na siku hizi anaongea lugha yao kama anaongea at all. kaitelekeza issue yenyewe baaada ya kununliwa.
 
Uzuri wa system yetu ya uchaguzi, hata kukiwa na independent candidates, bado haitaharibu chochote. Serikali inaundwa na rais na sio uwiano wa kura za vyama. Labda huyo independent candidate ashinde urais, ambacho ni impossible.
 
Hofu ya 2010? hapana...ni yupi wa kuwashinda? simwoni hadi sasa...kwa hiyo asipoteze muda na vitendea kazi kwa ajili ya jambo ambalo lipo wazi na halina athari kubwa kwao kwa hali ilivo sasa
 
CCM na serikali yao lazima wapinge hiyo interpretation. Sababu ni simple, strategy imekuwa hivyo tangu tupate uhuru. Otherwise isingekuwa inawezekana kwa mtu mmoja, asiyekuwa na elimu yoyote ya kutosha, lakini anayo kadi ya chama, anakuwa waziri wa wizara saba(7!) tofauti ktk muda wa karibu miaka 30!
Hii haitokei popote duniani zaidi ya Tanzania! Ukitafuta kwa nguvu sana, unaweza kuikuta North Korea, Cuba, Syria, n.k.

Kwa ufupi katiba yote ya JMT inahitaji kubadilishwa, kwani ndiyo imekuwa ikitudumaza kwenye maendeleo tangu tulipoanza. Kwa kutumia udikteta wawe, baba wa taifa alijilimbikizia madaraka yote mikononi mwake, akidhani kuwa atakuwa "effective" ktk kutimiza "ndoto" zake za ujamaa wa kiafrika.

Alisahau au hakujua mambo mengi ambayo ni muhimu na hayabadilishiki, miongoni mwao kuwa hatoishi milele, na pia hao wakoloni wamekamata mpini na yeye na wenzie wamekamata makali. Matokeo yake tunayavuna hadi leo.

Waziri anapopinga interpretation ya High Court, anasisitiza uwiano uliopo uendelee kuwapo ambapo CCM wanamiliki kila kitu, kila mtu, kila sheria, kila uamuzi, kila uchaguzi.
Idumu CCM!! Idumu CCM! Idumu CCM! Wadumu MAFISADI!!!
 
BUBU Ataka Kusema,
Haya wana sheria hebu tupeni mwanga kidogo hii claim ya Minister inakuwaje........Je ni kweli Jaji ali-alter constitution badala ya Kuitafsiri. Wakuu Mushobozi, Mwendapole, Augustus na wanasheria wengine hebu tupeni elimu kidogo.
 
- Ninakumbuka siku moja huyu waziri akiniambia maneno haya haya one on one, kwamba ni bunge tu ndilo lina power kikatiba kubadilisha au kuidhinisha wagombea huru, na alisema kwamba mara baada tu ya ile hukumu ya Mtikila, serikali ilikata rufaa, lakini mpaka leo mahakama imekua ikikwepa hii kesi kwa sababu ya kuogopa aibu, maana walijua wamechemsha na ile hukumu sasa naona amerudia tena maneno yale yale,

- Niliwahi kumuuliza kiongozi mwingine wa juu wa serikali ya sasa kwamba CCM wanaogopa nini na hili la Independent Candidates? Akasema kwamba moja ya sharti kubwa la Afro Shirazi Party, Visiwani on Muungano ilikuwa kwamba Bara watahakikisha kwamba hilo halitakuja kutokea under their watch, yaani CCM, na siku likitokea itakua ndio mwanzo na mwisho wa Muungano, kwa sababu wanaogopa Sultani atarudi kirahisi sana, kama independent Candidate sijui how much true is this, lakini mpaka leo sioni sababu ya msingi kwa CCM kuikataa hii hoja, kwa sababu hata ikikubaliwa wanaweza kuitumia sana kwa their advantage,

- Ingawa binafsi siamini kwamba hii hoja ndio hasa the answer to our national political na legal misery tuliyonayo sasa, dawa ni kurekebisha katiba tuliyonayo maana iliundwa purposerly for one party rule sio vyama vingi, sijui ni lini wa-Tanzania tutakuja kulielewa hili na kulifanyia kazi!.

Respect.

FMES!
 
Wakuu naomba somo hapa..
Mimi navyofahamu sheria ya mgombea ni kama alivyo eleza huyu Waziri kwamba mahakama kazi yao ni kutafsiri Sheria ktk kutoa suluhu lakini sio kubadilisha sheria..Na hakuna tafsiri yoyote inayomruhusu Mgombea binafsi ambaye hana chama ikatafsirika na kukubalika kinyume kama court ilivyoamua ktk kesi ya Mtikila..Huku ni kubadilisha sheria kazi ambayo sii ya mahakama..

Huwezi kuondoa sheria (restriction) zinazomzuia mgombea binafsi ukasema ni interpret ya sheria ya mgombea yupi anayeruhusiwa wakati sheria inajieleza waziwazi kwamba haruhusiwi!.

Mimi nadhani tunachukulia swala hili kwa ushabiki na sii kufuata sheria.. hata mimi ningependa kuona wagombea binafsi lakini swali linarudi palepale.. Ikiwa leo tunashindwa kuvichagua vyama kama CUF na Chadema kwa sababu havina team tosha ya uongozi huyu mtu mmoja atakuwa amebadilisha kitu gani?..Je, akishinda ataweza vipi kuunda serikali!.. maanake inabidi tubadilishe pia sheria za bunge na Mawaziri..Hao mawaziri watatoka chama gani?.

Mbali na yote haya Court ilifanya makosa..labda mnipe somo wakuu zangu hizi tafsiri za sheria kutengua iliyopo ktk msahafu zinashindwa kuzielewa.
 
Ndio maana nikaomba wanasheria waje hapa kutuelimisha....na pengine mwenye ruling atuwekee hapa tuone Mahakama kama ili-alter sheria au ilitafsiri........
 
.....Haya wana sheria hebu tupeni mwanga kidogo hii claim ya Minister inakuwaje........Je ni kweli Jaji ali-alter constitution badala ya Kuitafsiri........Wakuu Mushobozi, Mwendapole, Augustus na wanasheria wengine hebu tupeni elimu kidogo.......

Mimi namsubiri 'Philadelphia Lawyer' wetu humu ndani aje aibomoe bomoe hoja ya waziri...
 
Mimi namsubiri 'Philadelphia Lawyer' wetu humu ndani aje aibomoe bomoe hoja ya waziri...

.....jamaa ana kesi nyingi bana na bado hajazimaliza(uchungzi haujakamilika).....sasa hii sijui ataanzia wapi.........kwi kwi kwi
 
.....jamaa ana kesi nyingi bana na bado hajazimaliza(uchungzi haujakamilika).....sasa hii sijui ataanzia wapi.........kwi kwi kwi

- Subira huwa inavuta heri jamani...it doea not hurt kuendelea kusubiri matokeo ya uchunguzi, bwa! ha! ha! acheni haraka vijana!

Respect.

FMEs!
 
Kuna mwanasheria maarufu sana wa Uingereza aliyesema " The Law is an Ass".
Kila mtu aweza kumpanda.

Lakini sheria haitekelezeki in a vaacum, inatekelezeka katika jamii inayoimiliki sheria hiyo.
Si nia yangu kuiponda sheria lakini kwa society za third world the Law must be an Ass ambayo inapandwa kwa uangalifu ukijua kule unakoelekea usije anguka.

Na ndio maana leo mwafrika aliyekuwa naturalised katika nchi nyingi tu za Ulaya kupata nafasi ya uwakilishi katika mabunge ya huko , au Uwaziri Mkuu, au Urais ni ndoto.

Tu kitazama sheria yetu na udhibiti wa private canditaes inabidi tutazame upande wa pili wa uhuru huo ambao wengi humu JF wanaushabikia lakini mwisho wake hauna tija. Tutazame scenarios vis-a-vis the Tanzanian palying field,

1 Private candidate itabidi awe na mtaji wa kutosha kuelezea sera zake katika jimbo au nchi nzima
(iwe uchaguzi wa ubunge au wa urais).

2 Private candidate huyu lazima awe na mtandao-si lazima uwe wa kisiasa, kueneza uwezo wake.

3 Watanzania walio wengi, wapiga kura ni masikini sana, na wananunulika kama uzoefu wetu ulivoonyesha katika matukio mengi ya uchaguzi wa kisiasa.

Sasa hivi kuna tatizo kubwa la mafisadi kujipenyeza katika uongozi wa vyama mbalimbali na matokeo yake yanaonekana ikiwa ni pamoja na migongano isiyo ya lazima.

Sasa wana JF nauliza , kisheria , utamzuiaje mtu kama Rostam kuwania Urais akitaka kufanya hivyo as a private candidate?

4 Private candidate huyu na mtandao wake lazima arudishe fedha yake atakapopata madaraka
 
Lole Gwasika,
Kuna mwanasheria maarufu sana wa Uingereza aliyesema " The Law is an Ass".
Kila mtu aweza kumpanda.
Duh Mazee, hapa kidogo umenitisha..Kumbe sheria ni hivyo eeeh! au jamaa ni shoga anasherehekea kivyake!
 
Back
Top Bottom