Kwani huyu kama kaishiwa kabla ya kujitoa aliwasiliana na viongozi wake???
Kuna mjumbe mmoja amesema anaiona CUF kuwa makini kuliko CHADEMA sababu ni wagombea wa CHADEMA tu wanaonunuliwa na si wa CUF. Hili haliifanyi CUF kuwa makini kuliko CHADEMA, tukumbuke kuwa mwaka 2005 tishio kwa CCM ilikuwa ni CUF ndiO maana waliizushia CUF kuwa na udini na kampeni zote mbaya za CCm, target ilikuwa CUF. Mwaka huu target kubwa ya CCM ni CHADEMA maana ndicho chama tishio kwa CCM uchaguzi katika huu. kila wanachosema CCM wanaiwinda CHADEMA maana ndio tishio kwao.
Lazima watanzania tuache unafiki, hapa tulipofika ni CCM ndo imetufikisha hapa. Na tukumbuke kuwa kushindwa kwa CHADEMA mwaka huu ni kushindwa kwa watanzania wote wapenda maendeleo na wenye uchungu na nchi yao. watashindwa chadema baadhi watafurahi lakini foleni bararabani zitazidi,wanafunzi shule za kata wataendelea kufeli, wanafunzi wa vyuo watakosa fedha za kujikimu, watoto wetu wataendelea kukaa chini(kwa shule ambazo wanakaa chini kwa sasa), huduma za afya zitaendelea kuwa duni,Polisi watendelea kukaa kwenye nyumba za full suti mabati, madini yetu yataendea kuibiwa, wageni wataendelea kujineemesha,wajanja wachache wataendelea kuneemeka, Mafisadi wataendelea kutamba mitaani. NINAAMINI HAYA KWA SABABU CCM WAMEKOSA MBINU MBADALA ZA KUTUTOA KATIKA HALI HII. NA KAMA TUKIWAPA NCHI HII TENA BASI HAYA NDO YATAKUWA MAISHA YETU KWA MIAKA MINGINE MITANO IJAYO,