Elections 2010 Mgombea CHADEMA Nkenge ajiondoa kugombea Ubunge

Elections 2010 Mgombea CHADEMA Nkenge ajiondoa kugombea Ubunge

Binafsi namfahamu huyu bwana Focus,kwanza ninashangaa ni lini huyu bwana ameanza siasa.Ni mpiga muziki maarufu pale Bukoba mjini.Chonde Chadema watu wa namna hii liwe fundisho kwenye chaguzi zingine.Tujipange tafadhali,saa ya ukombozi ndo inakaribia.


kwa hi unakiri kuwa CHADEMA ni wakurupukaji


jee ni kweli hawa ni wa kuwaachia nchi?

bado ni machelema hawa
 
Its sad. Ni makosa yanayofanywa na vyama vyote vya siasa kutofanya screening before. eti wanawaachia wananchi waamue, anyway its democracy...
 
kwa hi unakiri kuwa CHADEMA ni wakurupukaji


jee ni kweli hawa ni wa kuwaachia nchi?

bado ni machelema hawa

Siyo kwamba ni wakurupukaji bali ndivyo taratibu za kidemokrasia. utafanya nini kama mtu kapitia taratibu zote: kwa mfano, alikuwa mwanachama, akaomba uongozi na wanachama wenzake wakampitisha. Kitu kibaya ni huku watu kuwa wasaliti na kununuliwa kwa vijisenti ili kujitoa katika nafasi kama hiyo. Mtu kama huyo alitakiwa achunguzwe na ikithibitika kuwa alihongwa alitakiwa atiwe hatiani pamoja na aliyemhonga
 
mi nilishasema tangia awali. Chadema hamko serious. Mnabisha. Sasa kweli chama ambacho kinataka kipewe nchi hawawezi hata kujipanga kuchagua wagombea wa ukweli. Watu wanawasikiliza, wanaingia kundini, baada ya kuona incompetence ya mbowe jinsi anavyoendesha chama. Tartiibu wanakula kona. Its unfortunate, lakini as of now--hamko serious.


watanzania tumefika hapa tulipo kwa sababu ya kutaka kufanyiwa kila kitu, nakutegemea kuwa tutashushiwa amana kutoka mbinguni. Likitokea tatizo kidogo watu wanakula kona kama ulivyodai hapo juu badala ya kuchangia kuleta mabadiliko kila mtu katika eno lake. Ni wapi kuna watu cvompetemnt? Ni huko walikosheheni mafisadi, world bank na imf?

mpaka kila mmoja wetu atakapoamua kuplay his/her part kama kenya ndio ukombozi wa kweli utakuja, tutapata katiba mpya, na uhuru wa kweli. Lakini hii stayle ya ccm kila mtu anasubiri maagizo ya viongozi wa ngazi ya taifa ndio maana tunaishia kudai viongozi hawaka incompetent and committed enough katika kuleta mabadiliko .

nani kakuzuia wewe kufanya lolote kuleta mabadiliko katika eneo lako ualoishi, kufanya kazi, kutembelea n.k there is alot that can be done by individual activists katika kuleta mabadiliko. Lakini hii trend ya kuwasubiri mbowe, slaa na zitto ndio wafanye sisi wengine tubaki hapa jf kuwapima hatufanikiwa kamwe!!!!!

kama tumeshindwa kufanya chochote kulata mabadiliko katika eneo unaloishi, kufanyia kazi kutembelea n.k na badala yake tunawasubiri mbowe, slaa na zitto ndio waje kutekeleza mabadiliko ni lazima tutawaona hawako competent kumbe ni sisi wenyewe hatuko committed kuleta mabadiliko ya kweli
 
Hii chadema sasa inakuwa kama pakacha inayovuja. Mbona madudu haya hatusikii kutoka CUF? Yaani wanaonunulika ni Chadema tu? What a coincidency!! Naanza kushawishika kwamba CUF wako imara kuliko hiki chama cha ma-DJ.
 
Hii chadema sasa inakuwa kama pakacha inayovuja. Mbona madudu haya hatusikii kutoka CUF? Yaani wanaonunulika ni Chadema tu? What a coincidency!! Naanza kushawishika kwamba CUF wako imara kuliko hiki chama cha ma-DJ.


huku kuna SUGU, mpiga Disco kachomo, Nkaaya Kachomoa, mmiliki Bilicanas (mzee wa wapuki) na msanii Slaaa


hawa ni wasanii tu
 
Iko mkoa wa Kagera wilaya ya Karagwe. Du!! mzee mwenzangu si uwe unafuatilia jiografia na mabadiliko ya ma wilaya yetu?
 
Hii chadema sasa inakuwa kama pakacha inayovuja. Mbona madudu haya hatusikii kutoka CUF? Yaani wanaonunulika ni Chadema tu? What a coincidency!! Naanza kushawishika kwamba CUF wako imara kuliko hiki chama cha ma-DJ.

kumbe bado upo hai, watu walizusha humu jamvini kuwa umeaga dunia, pole sana .
 
Kuna msululu mkubwa wa wagombea wa Chadema kujiengua hata kama majina yao yameshapitishwa ,kama alivyokengeuka Slaa kuacha ubunge na kukurupukia Uraisi ,ndivyo hivyo wengi wa wachadema watakavyofanya alimuradi kuharibu kura za wanananchi.
 
Taarifa za sasa hivi ni kuwa mgombea ubunge kupitia CHADEMA Bw Focas amejiondoa katika kinyanganyiro hicho hivyo kuwacha wagombea wa CCM na CUFAwali ilidaiwa kuwa focas ambaye anamiliki vifaa vya mziki alidaiwa kupandikizwa na Dk Kamala aliyebwaga na Asumpta mshama katika kura za maoni.sababu za kujiondoa nitaweka hapa muda mfupi ngoja amalize kulonga na medianatumia simu

Huyu mbinafsi sana, jamaa alitegemea mshiko siyo. Nafikiri yeye alifikiri zile Billion 50 za CCM zinakwenda kwa wagombea hivyo alitegemea CHADEMA nao wana vibillion yao vya kugawa kama wezi wa CCM!!
 
Kuna msululu mkubwa wa wagombea wa Chadema kujiengua hata kama majina yao yameshapitishwa ,kama alivyokengeuka Slaa kuacha ubunge na kukurupukia Uraisi ,ndivyo hivyo wengi wa wachadema watakavyofanya alimuradi kuharibu kura za wanananchi.

Crap
 
kuna msululu mkubwa wa wagombea wa chadema kujiengua hata kama majina yao yameshapitishwa ,kama alivyokengeuka slaa kuacha ubunge na kukurupukia uraisi ,ndivyo hivyo wengi wa wachadema watakavyofanya alimuradi kuharibu kura za wanananchi.
crappy comments
 
Iko mkoa wa Kagera wilaya ya Karagwe. Du!! mzee mwenzangu si uwe unafuatilia jiografia na mabadiliko ya ma wilaya yetu?

Mkuu Magafu,
Sahihisho kidogo.
Ni kweli jimbo la Nkenge liko mkoani Kagera, lakini si wilaya ya Karagwe bali wilaya 'mpya' ya Missenyi. Kabla ya kuanzishwa kwa hiyo wilaya mpya, jimbo lilikuwa ndani ya wilaya ya Bukoba vijijini. Ni jimbo lililomegwa kutoka Bukoba vijijini enzi za utawala wa Mzee Ruksa.Mbunge wake wa kwanza alikuwa Mhe.Joseph Rwegasira, kisha Dr.Diodorus Kamala.
(NB.Binafsi natokea jimbo hilo)
 
kumbe bado upo hai, watu walizusha humu jamvini kuwa umeaga dunia, pole sana .

Teh teh teh teh teh, bado ni hai....hafi mtu hapa hadi nyani ameshakomwa giladi!! Si unajuwa tena JF na box!!!!
 
Kwani huyu kama kaishiwa kabla ya kujitoa aliwasiliana na viongozi wake???

Kuna mjumbe mmoja amesema anaiona CUF kuwa makini kuliko CHADEMA sababu ni wagombea wa CHADEMA tu wanaonunuliwa na si wa CUF. Hili haliifanyi CUF kuwa makini kuliko CHADEMA, tukumbuke kuwa mwaka 2005 tishio kwa CCM ilikuwa ni CUF ndiO maana waliizushia CUF kuwa na udini na kampeni zote mbaya za CCm, target ilikuwa CUF. Mwaka huu target kubwa ya CCM ni CHADEMA maana ndicho chama tishio kwa CCM uchaguzi katika huu. kila wanachosema CCM wanaiwinda CHADEMA maana ndio tishio kwao.

Lazima watanzania tuache unafiki, hapa tulipofika ni CCM ndo imetufikisha hapa. Na tukumbuke kuwa kushindwa kwa CHADEMA mwaka huu ni kushindwa kwa watanzania wote wapenda maendeleo na wenye uchungu na nchi yao. watashindwa chadema baadhi watafurahi lakini foleni bararabani zitazidi,wanafunzi shule za kata wataendelea kufeli, wanafunzi wa vyuo watakosa fedha za kujikimu, watoto wetu wataendelea kukaa chini(kwa shule ambazo wanakaa chini kwa sasa), huduma za afya zitaendelea kuwa duni,Polisi watendelea kukaa kwenye nyumba za full suti mabati, madini yetu yataendea kuibiwa, wageni wataendelea kujineemesha,wajanja wachache wataendelea kuneemeka, Mafisadi wataendelea kutamba mitaani. NINAAMINI HAYA KWA SABABU CCM WAMEKOSA MBINU MBADALA ZA KUTUTOA KATIKA HALI HII. NA KAMA TUKIWAPA NCHI HII TENA BASI HAYA NDO YATAKUWA MAISHA YETU KWA MIAKA MINGINE MITANO IJAYO,
 
Unajua watu wangi wanasahau historia ya mapinduzi, serikali ya wakoloni that time was doing the same to TANU, serikali ya makaburu in SA was doing the same to ANC. Mapinduzi si lelemama........

Someone asked a good question but came up with a crapy conclusion..........

Why CHADEMA????? Kwa nini wagombea wa CUF au TLP hawajitoi, well this is not a coincidence is a carefully calculated move ya kuwaonyesha wananchi ni namna gani CHADEMA haina umaarufu and make no mistake mtaanza kusikia majukwaani sasa hivi hata kutoka kwa mwenyekiti wa CCM kuhusu mambo haya.

Funny enough walivyohama akina Shibuda, Ntagazwa, Nyimbo tuliambiwa ni waroho wa madaraka.

And there comes the little nice phrase "HATUDANGANYIKI"
 
Back
Top Bottom