Pre GE2025 Mgombea Mwenza wa Urais CCM, Dkt Emmanuel Nchimbi hana Ushawishi wowote ndani na Nje ya CCM, ni Mzigo mzito kumnadi

Pre GE2025 Mgombea Mwenza wa Urais CCM, Dkt Emmanuel Nchimbi hana Ushawishi wowote ndani na Nje ya CCM, ni Mzigo mzito kumnadi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bado sielewi Vigezo ambavyo vimetumika Kumfanya Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM.

Nchimbi hana na wala hajawahi kuwa na Ushawishi wowote kwenye siasa za ndani na hata kwenye Majukwaa ya hadharani, Hata alipofukuzwa na Magufuli ndani ya ccm kwa kuwa Team Lowassa hakuna aliyemsikitikia, Afadhali hata Sophia Simba wanaccm walimpigania, hii maana yake ni kwamba, Sophia Simba alimzidi mno kwa Umaarufu Nchimbi.

Mtu wa aina hii kumpeleka kwenye majukwaa ya kuomba kura ni sawa na kujibebesha Gunia la Misumali, Hata huu Mkutano wa Mkuu wa CCM ambao umeratibiwa naye kama Katibu Mkuu wa Chama, ndio mkutano mkuu wa ccm uliododa zaidi kuliko mikutano mikuu yote tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
Soma Pia: Breaking News: - Uchaguzi 2025 - CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Naitabiria CHADEMA kampeni nyepesi zaidi kuliko Uchaguzi wowote tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi Nchini Tanzania, kazi ni kwenu Chadema, labda itumike tu mbeleko ya dola, lakini Je dola itakubali kutumika kubeba maji kwenye Tenda? Pipa litajaa?
hapo vyombo dola vitafanya kazi
 
Inaonekana humjui Nchimbi. Uliyemuelezea sio Nchimbi ni mtu mwingine. Nchimbi naemjua ni smart sana.
Ni kweli ni Smart maana alimpandisha cheo RPC Michael Kamuhanda aliyeshiriki mauaji ya Mwangosi
 
Mqenzenu tayari amepewa ulinzi leo rasmi, ukiteuliwa ccm ni uhakika na polisi na jeshi watalisimamia hili litokee
 
Ya kwenu yameishaje huko maana mpo kukumbushiana wema mliofanyiana ili muoneane huruma kumpata chairman na mnalaluana kweli kweli.

Zile story za nyinyi ni watu wa democracy mmeonesha kwa vitendo kuwa democracy sio utaratibu wenu.
 
Bado sielewi Vigezo ambavyo vimetumika Kumfanya Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM.

Nchimbi hana na wala hajawahi kuwa na Ushawishi wowote kwenye siasa za ndani na hata kwenye Majukwaa ya hadharani, Hata alipofukuzwa na Magufuli ndani ya ccm kwa kuwa Team Lowassa hakuna aliyemsikitikia, Afadhali hata Sophia Simba wanaccm walimpigania, hii maana yake ni kwamba, Sophia Simba alimzidi mno kwa Umaarufu Nchimbi.

Mtu wa aina hii kumpeleka kwenye majukwaa ya kuomba kura ni sawa na kujibebesha Gunia la Misumali, Hata huu Mkutano wa Mkuu wa CCM ambao umeratibiwa naye kama Katibu Mkuu wa Chama, ndio mkutano mkuu wa ccm uliododa zaidi kuliko mikutano mikuu yote tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
Soma Pia: Breaking News: - Uchaguzi 2025 - CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Naitabiria CHADEMA kampeni nyepesi zaidi kuliko Uchaguzi wowote tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi Nchini Tanzania, kazi ni kwenu Chadema, labda itumike tu mbeleko ya dola, lakini Je dola itakubali kutumika kubeba maji kwenye Tenda? Pipa litajaa?
Sawa, bc shindeni uchaguzi mkuu na usije na kilio cha kuibiwa kura
 
TOKA MAKTABA

11 March 2017
SOPHIA SIMBA AFUKUZWA UANACHAMA CCM, EMMANUEL NCHIMBI AONYWA...

View: https://m.youtube.com/watch?v=jW6MRogjQzk
Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC, imewafukuza Uanachama Baadhi ya wenyeviti wake wa Mikoa, Wilaya, Wajumbe wawili wa Kamati Kuu na Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri kuu kwa tuhuma za Kukihujumu Chama hicho.
 
Hivi umri wa nchimbi ni sahihi? Kwa sura anaonekana mtu mwenye 60+. Ila mwaka wa "kuzaliwa" ni 1971

Rais Ajaye wa 2030
 
Break news toka kwa mheshimiwa rais, From the horse's mouth

View: https://m.youtube.com/watch?v=V07_6eYkmvM

Wajumbe wa mkutano mkuu waelezewa waliyonongona Kamati Kuu CC kutafuta mgombea mwenza, miezi ya karibuni alonikabili kuniomba apumzike ... hali hiyo ikazungumwa Kamati Kuu na kuafiki maombi ya makamu wa Rais ...tumekubaliana Dr. Philip Mpango lakini nani atatufaa nikawa na majina kadhaa nimanongona na kaka zangu wastaafu Dr. Shein, Kikwete na Karume ... tukakubaliana jina moja na likapelekwa Kamati Kuu bahati nzuri likakubaliwa na jina hilo pendekezwa ni la balozi Dr. Emmanuel Nchimbi awe mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM 2025 ...
 
TOKA MAKTABA

11 March 2017
SOPHIA SIMBA AFUKUZWA UANACHAMA CCM, EMMANUEL NCHIMBI AONYWA...

View: https://m.youtube.com/watch?v=jW6MRogjQzk
Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC, imewafukuza Uanachama Baadhi ya wenyeviti wake wa Mikoa, Wilaya, Wajumbe wawili wa Kamati Kuu na Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri kuu kwa tuhuma za Kukihujumu Chama hicho.

😆😆😆
 
DAVOS summit nani atakwenda kuzungumza mambo mazito, sijamsikia Dr. Emmanuel Nchimbi akitiririka kimataifa katika lugha ya kigeni mambo mazito.

TOKA MAKTABA :
March 2024

NCHIMBI HAILS SAMIA'S LEADERSHIP AT 11TH MEETING OF SISTER REVOLUTIONARY PARTIES

View: https://m.youtube.com/watch?v=RiS-IrnPXXY
The Secretary-General of the Revolutionary Party (CCM), Ambassador Dr. Emmanuel John Nchimbi.
Ambassador Emmanuel Nchimbi stated that all Tanzanians take pride in the great leadership capability demonstrated by the President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Samia Suluhu Hassan, during her three years in office.
 
akitiririka kimataifa katika lugha ya kigeni mambo mazito
TOKA MAKTABA:

Dr. Philip Mpango, the Executive Secretary in the President's Office, Planning Commission for Tanzania, discusses Africa's engagement with both new and traditional donors at a roundtable discussion organised by UONGOZI Institute (Institute of African Leadership for Sustainable Development) on 29 May, 2012.

View: https://m.youtube.com/watch?v=AvuU0dVvB40
 
Back
Top Bottom