Pre GE2025 Mgombea Mwenza wa Urais CCM, Dkt Emmanuel Nchimbi hana Ushawishi wowote ndani na Nje ya CCM, ni Mzigo mzito kumnadi

Pre GE2025 Mgombea Mwenza wa Urais CCM, Dkt Emmanuel Nchimbi hana Ushawishi wowote ndani na Nje ya CCM, ni Mzigo mzito kumnadi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nchimbi anajua mipaka pia Samia anaenda Ngwe ya mwisho.

Tofauti na kwamba hajawahi fikiria kumpa nafasi ya Urais Mzanzibar na ndicho kinawatesa hakuna Cha ushawishi Wala blaa blaa zingine.

Kama tunachagua na kuweka watu kwenye mizani,Kuna Rais gani anaweza mzidi Samia Kwa utekelezaji wa ilani?
Kununua magoli ya Simba na Yanga ndio kazi za Rais hizo?
 
Unpopular opinion: Nchimbi anamzidi vitu vingi sana Samia katika siasa kuanzia ndani ya chama mpaka nje.

Ukiwekwa uchaguzi ndani ya chama kati ya Samia na Nchimbi, Nchimbi anashinda asubuhi tu.

Samia amechagua makamu wa Rais anayemzidi nguvu ya kisiasa sorry to say this.

Ni hatari kwa siasa za nchi ya giza.
Anamzidi wapi,majina ya wana CCM yaliyopo midomoni mwa Watanzani ni January Malamba,Nape,Mwigulu Nchemba kidogo na Makonda sasa huo umaarufu wa nchimbi umetokea angani.
 
Bado sielewi Vigezo ambavyo vimetumika Kumfanya Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM.

Nchimbi hana na wala hajawahi kuwa na Ushawishi wowote kwenye siasa za ndani na hata kwenye Majukwaa ya hadharani, Hata alipofukuzwa na Magufuli ndani ya ccm kwa kuwa Team Lowassa hakuna aliyemsikitikia, Afadhali hata Sophia Simba wanaccm walimpigania, hii maana yake ni kwamba, Sophia Simba alimzidi mno kwa Umaarufu Nchimbi.

Mtu wa aina hii kumpeleka kwenye majukwaa ya kuomba kura ni sawa na kujibebesha Gunia la Misumali, Hata huu Mkutano wa Mkuu wa CCM ambao umeratibiwa naye kama Katibu Mkuu wa Chama, ndio mkutano mkuu wa ccm uliododa zaidi kuliko mikutano mikuu yote tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
Soma Pia: Breaking News: - Uchaguzi 2025 - CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025


Naitabiria CHADEMA kampeni nyepesi zaidi kuliko Uchaguzi wowote tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi Nchini Tanzania, kazi ni kwenu Chadema, labda itumike tu mbeleko ya dola, lakini Je dola itakubali kutumika kubeba maji kwa kutumia Tenga? Je Pipa litajaa?
Dkt Nchimbi ambacho alishatukera wana CCM ni kusherehekea kifo cha Dkt Magufuli na kuendeleza vijembe. Sijui huu udhaifu ataumalizaje, japo kwa nafasi yake kama Katibu mkuu alitakiwa kuomba msamaha na kuponya mioyo ya kundi la Dkt Magufuli. Ila ninvyoona hawezi kuomba msamaha na mwisho itakuwa mwisho wake mpaka atapopatika rais ambaye ni pro Dkt Magufuli
 
Back
Top Bottom