Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge Khamis Mwinjuma (Mwana FA) aliwahi kukiri kuwachukia baadhi ya watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama (Askari wa Jiji)

Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge Khamis Mwinjuma (Mwana FA) aliwahi kukiri kuwachukia baadhi ya watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama (Askari wa Jiji)

Askari wa jiji sio Polisi na vyombo vya usalama kama ulivyo orodhesha, Askari wa jiji ni wale wagambo waliokua wakikamata majungu ya Ubwabwa ya Mama ntilie, kukimbizana na wamachinga na wapiga debe kila kukicha,
walikimbizana Sana na ombaomba katikati ya jiji wengi wao wakiwa walemavu.
Hakuna kijana wa daressalaam aliewapenda Hawa jamaa, kwa miaka Ile alikua Sawa 100%
 
Askari wa jiji sio Polisi na vyombo vya usalama kama ulivyo orodhesha
Hata mwanajeshi pia sio Polisi. Ndio maana wakaitwa ni askari wa jiji. Hawa pia ni sehemu ya watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaotambulika kisheria na wanahitaji kuheshimiwa...
 
Askari wa jiji ni wale wagambo waliokua wakikamata majungu ya Ubwabwa ya Mama ntilie, kukimbizana na wamachinga na wapiga debe kila kukicha,
Askari wa jiji (hao mnaowaita mgambo) walikuwa wakijafanya hayo kwa mama lishe, wamachinga na wapiga debe katika kutekeleza kile kinachoitwa utii wa sheria bila shurti, jambo ambalo linamanufaa kwa umma katika kuwakinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko pamoja na kuweka mazingira bora ya "jamii inayoongozeka katika mstari sahihi"...
 
ilikua ni mifumo kandamizi tu ya maisha, mbona utawala huu hawafanyi waliyokua wakiyafanya, na hatulipuki na hayo maradhi na mama ntilie wanaendesha shughuli zao bila bugdha.
Kwanini walikua wanakimbilia kupora majungu ya Ubwabwa na kuondoka nayo pasipo kujua yanapoenda kumwagwa.
Solution ilikua kuwaboreshea mazingira na si kukataza wasifanye biashara.
 
Hata mwanajeshi pia sio Polisi. Ndio maana wakaitwa ni askari wa jiji. Hawa pia ni sehemu ya watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaotambulika kisheria na wanahitaji kuheshimiwa...
Mgambo wanaheshima kubwa Sana kwa nchi lakini lazima tukubali heshima yao waliishusha wenyewe
Wewe unadhani kwanini magufuli alipoingia madarakani tu akaanza na mgambo wanaonyanyasa wafanya biashara.
 
wakati makamba au abas kandoro wakiwa wakuu wa mkoa wa daressalaam ulikua na umri gani au ulikua mkoa gani, maana tuanzie hapo tusipoteze muda na nguvu.
Kwanini unakwepa kujibu swali langu boss? Waliishusha wenyewe kivipi hao askari wa jiji?
 
Back
Top Bottom