GE2025 Mgombea Udiwani CHAUMMA Kata ya Liganga atimkia CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mgombea Udiwani Kata ya Liganga, Fulco Komba aliyekuwa akigombea kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuvutiwa na sera zake za maendeleo.
Tukio hilo lilijiri jana Septemba 30, 2025 katika mkutano wa kampeni wa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama, uliofanyika Kijiji cha Liganga, wakati akinadi Ilani ya CCM ya 2025-2030.

Aidha, kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mahmoud Juma, naye alitangaza kuhamia CCM akisema ameridhishwa na utekelezaji wa ilani hiyo.

Kwa sasa, Mhagama anaendelea na kampeni zake za kijiji kwa Kijiji katika Jimbo la Peramiho, akiomba wananchi waendelee kuiamini CCM kwa kuwapa kura za ndiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

1759309314002.png

1759308993523.png
 
Ni abrakadabra na vituko vya siasa tu. Ni mpuuzi, angesubiri uchaguzi upite ndio atimkie huko
 
Mgombea Udiwani Kata ya Liganga, Fulco Komba aliyekuwa akigombea kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuvutiwa na sera zake za maendeleo.
Tukio hilo lilijiri jana Septemba 30, 2025 katika mkutano wa kampeni wa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama, uliofanyika Kijiji cha Liganga, wakati akinadi Ilani ya CCM ya 2025-2030.

Aidha, kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mahmoud Juma, naye alitangaza kuhamia CCM akisema ameridhishwa na utekelezaji wa ilani hiyo.

Kwa sasa, Mhagama anaendelea na kampeni zake za kijiji kwa Kijiji katika Jimbo la Peramiho, akiomba wananchi waendelee kuiamini CCM kwa kuwapa kura za ndiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Hata kama angetimkia Chauma sawa pia
 
Back
Top Bottom