Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Mgombea udiwani wa kata ya ilala Saady Khimji( Home Boy) amesema Chama Cha Mapinduzi, CCM Kinafanya jitihada kubwa ya kuinadi ilani yake kupitia majukwaa na Kampeni mbambali zinazofanywa na Wagombea wa Chama hicho Akizungumza Leo Oktoba 18, 2025 katika Mkutano wa kuwatambulisha na kuwanadi wagombea katika kata ya ilala, Kabla ya kunadi sera zake Khimji ameahidi kuilinda ilani ya CCM na kueleza kuwa yeyote atakayethubutu kumkwamisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, Pamoja na Serikali yake Watapambana naye kabla yake.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi akiwemo Mwenyekiti wa CCM ilala, Ndugu Alhaji Said Side na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu pamoja na wagombea udiwani kutoka kata mbalimbali na wawakilishi wa ubunge wa viti maalum katika kata ya ilala