McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP) kimesema endapo kitapata ridhaa ya kuongoza nchi, kitaanzisha hatua kali dhidi ya vitendo vya ufisadi, ikiwamo kujenga bwawa maalumu lenye mamba Ikulu kwa ajili ya kuwachukulia hatua mafisadi.
Kauli hiyo imetolewa leo, Jumatano Septemba 17, 2025 na mgombea urais wa chama hicho, Kunje Ngombare Mwiru, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mwiru amesema hatua hiyo ni ya ishara katika kupambana na rushwa, akisisitiza kuwa adhabu kali kwa watuhumiwa wa ufisadi ni jambo linalowezekana ikiwa kutakuwa na dhamira ya kweli ya kisiasa.
"Haiwezekani mtu kala hela za umma, anatembea na kitambi chake mtaani tunamwangalia tu huku hospitali watu wanakufa kwa kukosa dawa, hiyo sio kwa Serikali yangu.
"Pale Ikulu nitachimba bwawa la mamba na wale mafisadi wote watadumbukizwa, huko kuliwa hadi kuisha na nguo zake mtazikuta zimewekwa hapo kama ushahidi wa hilo kujua kuna mtu alidumbukizwa humo.
"Pia, hiki kirungu changu nilichoshika mkononi kitatumika kuwapiga kabla hawajaingia ndani ya bwawa hilo na kama nina ziara nje ya nchi siku hiyo nitaiahirisha hadi nihakikishe nimemshughulikia fisadi huyo," amesema mgombea huyo.
Soma Pia:

- GE2025 - Mgombea Urais wa AAFP, Kunje Ngombale Mwiru: Mafisadi watakumbana na Bwawa la Mamba Ikulu
- GE2025 - Kunje Ngombale: Nikiwa rais nitafuga mamba kwa ajili ya mafisadi
- GE2025 - Kingunge Ngombale–Mwiru: Mkinichagua kuwa rais, Mawaziri wangu hawatalala ni mchakamcha tu