Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
Ingawa hakuna kanuni inayohitaji mgombea Urais (CCM) kuwa mjumbe wa NEC, imekuwa ni utamaduni kwa kigezo hiki kutumika, na itaendelea kuwa hivyo for the next foreseeable future; Hii ndio sababu kubwa kwanini Chaguzi za NEC mara zote huwa na pilika pilika nyingi na ushindani wa hali ya juu; Hapo nyuma niliwahi kuja na mada iliyojadili kwanini bila ujumbe wa NEC, Urais Kupitia CCM haiwezekani, na kila siku zinavyozidi kwenda mbele, hoja hii inazidi kuwa na mashiko;
January na Membe walikuwa ‘Very Smart' kuamua to take the risk na kugombea Ujumbe wa NEC kupitia zile nafasi kumi za kifo i.e. NEC Ngazi ya taifa; Ingawa uamuzi huu ulikuwa too risky, suala ambalo wengi waliikimbia na kuamua kwenda kujaribu bahati zao huko wilayani, inaonyesha Membe na January walifanya a Cost – benefit Analysis na hatimaye kuona kwamba, it is more of a political asset than a liability, either for 2015 or beyond, hasa iwapo Chadema itachukua nchi 2015; Faida kubwa ya kuchukua uamuzi huu ni kwamba - whether you lose or win, tayari jina lako litakuwa sio geni miongoni mwa waamuzi wa nani awe mgombea Urais kupitia CCM 2015, ambao ni Wajumbe Mkutano Mkuu wa Taifa (CCM);
Wajumbe wa sasa watamaliza muda wao mwaka 2017, kwahiyo, ni wajumbe hawa hawa waliowapitisha Membe, January, Lukuvi, Wassira, Shigela, Mathayo, Msome, Nchemba, Mukama na Mukangara, ndio watakaopigia kura jina la mgombea Urais (CCM) 2015; Nje na Member na January, wengine waliobakia ni aidha sio Presidential Material au umri hautawaruhusu; Suala hili la Presidential Material ni relative na tutalijadili baadae;
Je, ni vigezo gani hutumiwa na CCM kumpata mgombea Urais? Najua wengi katika mjadala huu wataleta hoja khanga, kofia, n.k, kwani ukweli ulio wazi ni kwamba Chama kimechafuka; Lakini tukiweka hili pembeni kwa sasa, Vigezo vinavyotumika kuteua jina la mtu kuwa mgombea Urais (CCM) vipo vingi, na vingine ni very arbitrary na pia mchakato wake sio democratic; Lakini huo ni mjadala mwingine, na kwa sasa ningependa kujadili vigezo vifuatavyo:
Ifahamike tu kwamba wagombea wa NEC kupitia wilayani hawana prominence kichama kama wale Kumi waliopita ngazi ya Taifa kwani, tofauti na wa wilayani, wa taifa sasa tayari wanajulikana wapiga kura ambao ni Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa 2012-2017, na ni wapiga kura hawa ndio waliompa Membe na January Kura nyingi za NDIO;
Kwahiyo iwapo Membe na January wataamua kugombea 2015, njia yao ni nyeupe, na sana sana wanachohitaji only ‘fine tuning' za hapa na pale; Iwapo mungu atawajalia Afya na Uzima, kitendo cha hawa wawili kuchukau fomu ya kugombea Urais 2015, automatically kitapelekea majina yao kufikia hatua ya mwisho ya mchakato wa kupata mgombea wa CCM - yani majina yao yatakuwa ni miongoni mwa majina matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa May 2015 kupigiwa kura; Kilichobakia kwa sasa ni kujua jina la tatu litakuwa ni la nani, ingawa huyu wa tatu hatokuwa na nguvu kama Membe au January; Nitafafanua hili lidogo hapo chini;
Uchaguzi wa NEC mwaka huu ulikuwa ni tukio pekee lililobakia kutupatia picha halisi jinsi gani mbio za Urais zitakavyo unfold kuelekea 2015, na unless litokee tukio kubwa sana na lisilotarajiwa kama vile CCM kumeguka na kuwa vyama viwili tofauti, hayata kuja majina mengine mapya na yenye kuvuma kuliko ya Membe, January, Lowassa, Mwandosya, Kigoda, Mwakyembe, Sumaye, Sitta, Migiro, Nape na Magufuli; Kutokana na sababu mbalimbali ambazo tutazijadili baadae, iwapo hawa wengine pia watajaribu bahati yao, mwisho wa siku, wote hawa katika hatua mbalimbali, watahamia kwenye kambi kuu mbili: (1) Kambi ya Membe au (2) Kambi ya January;
Utabiri wangu kama mlivyoona haupo biased, bali ni objective na unaotumia hoja, na sio uganga; Kwahiyo nategemea kwamba hoja yangu itakuwa challenged objectively na bila matusi. Pia ningependa kwenda mbali zaidi kidogo na utabiri wangu kwamba, kutokana na Chadema kuendelea kushindwa kupanua agenda yake ya kuingia ikulu nje ya UFISADI, na pia kutokana na Chadema kuendelea ku-ignore kushinikiza mabadiliko ya Kanuni ya ushindi wa chaguzi kuu i.e. kanuni ya mshindi ni mshindi iliyopitishwa na Bunge, Uchaguzi wa 2015, CCM kupata 50.01% ya popular vote dhidi ya Chadema ni kazi ndogo sana, bila hata ya uchakachuaji; Na kupata 50.01% ni rahisi kwa CCM hata ikiweka mgombea yoyote yule; Vinginevyo, iwapo things remain constant until 2015, na Membe na January wakagombea, Basi Ifikapo November 2015, Rais wa TANO wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania atakuwa ni aidha Bernard Membe, au January Makamba;
Na yoyote kati ya hawa wawili ataweza tu kumudu nafasi hii as long as he fulfills conditions such as: Upeo wa masuala ya kiuchumi na kisiasa - kitaifa na kimataifa katika nyakazi za leo, Uzalendo, anajali maslahi ya taifa mbele, Mkali, Ana uelewa wa matatizo ya wananchi, na ana ubunifu na pia moyo wa dhati wa kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya wananchi, hasa wa vijijini; Lakini Rais ajaye ataweza kumudu nafasi hii vizuri zaidi iwapo katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho ili kuondokana na migogoro inayoendana na nafasi ya Urais; Suala lingine ambalo ni muhimu sana ni kwamba kutakuwa na ulazima wa Rais mteule (CCM) kupewa ushirikiano na kambi zote zilizopo sasa ndani ya CCM, vinginevyo Rais na nchi itayumba/haitatawalika;
Mwisho kabisa niseme tu kwamba nia yangu hapa sio kupigia debe viongozi hawa wawili kwani mbali ya siasa za NEC nilizojadili na pia conditions nilizojadili hapo juu, bado wana kazi kubwa ya kuaminisha watanzania kwamba atakayepita atakuwa Rais Bora na sio Bora Rais; Na mpaka tufikie hatua hiyo, Chadema wakifanyia kazi mapungufu yao, Rais Bora kwa Tanzania 2015 ni Tundu Lissu, na hii ni changamoto kwa Wagombea wa CCM kwamba muda ukifika, waanze kujieleza kwa wananchi kwamba wanasimamia ISSUES gani, kwani suala la PERSONALITY halitakuwa kigezo tosha cha kumpelekea mgombea Urais ikulu 2015; Inawezekana huko mbeleni wagombea wa CCM wataanza kunadi issues wanazosimamia, lakini mpaka tufike huko, mimi binafsi nadhani iwapo kutakuwa na uchaguzi wa Rais leo, Rais bora wa Tanzania ni TUNDU LISSU;

- Awe na Sifa za Kuwa Mbunge Kufikia Kipindi husika
- Awe Mjumbe wa NEC Kufikia Kipindi Husika
- Jina lake liwe familiar miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa
- Asiwe amethibitika kwamba ni mla rushwa (tetesi hazitoshi)/Awe na Sifa Za Kukemea Rushwa
- Na Awe na Umri utakaovutia Wapiga Kura Vijana