Ingawa hakuna kanuni inayohitaji mgombea Urais (CCM) kuwa mjumbe wa NEC, imekuwa ni utamaduni kwa kigezo hiki kutumika, na itaendelea kuwa hivyo for the next foreseeable future; Hii ndio sababu kubwa kwanini Chaguzi za NEC mara zote huwa na pilika pilika nyingi na ushindani wa hali ya juu; Hapo nyuma niliwahi kuja na mada iliyojadili kwanini bila ujumbe wa NEC, Urais Kupitia CCM haiwezekani, na kila siku zinavyozidi kwenda mbele, hoja hii inazidi kuwa na mashiko;
January na Membe walikuwa Very Smart kuamua to take the risk na kugombea Ujumbe wa NEC kupitia zile nafasi kumi za kifo i.e. NEC Ngazi ya taifa; Ingawa uamuzi huu ulikuwa
too risky, suala ambalo wengi waliikimbia na kuamua kwenda kujaribu bahati zao huko wilayani, inaonyesha Membe na January walifanya a Cost benefit Analysis na hatimaye kuona kwamba, it is more of a political asset than a liability, either for 2015 or beyond, hasa iwapo Chadema itachukua nchi 2015; Faida kubwa ya kuchukua uamuzi huu ni kwamba - whether you lose or win, tayari jina lako litakuwa sio geni miongoni mwa waamuzi wa nani awe mgombea Urais kupitia CCM 2015, ambao ni Wajumbe Mkutano Mkuu wa Taifa (CCM);
Wajumbe wa sasa watamaliza muda wao mwaka 2017, kwahiyo, ni wajumbe hawa hawa waliowapitisha Membe, January, Lukuvi, Wassira, Shigela, Mathayo, Msome, Nchemba, Mukama na Mukangara, ndio watakaopigia kura jina la mgombea Urais (CCM) 2015; Nje na Member na January, wengine waliobakia ni aidha sio Presidential Material au umri hautawaruhusu; Suala hili la Presidential Material ni relative na tutalijadili baadae;
Je, ni vigezo gani hutumiwa na CCM kumpata mgombea Urais? Najua wengi katika mjadala huu wataleta hoja khanga, kofia, n.k, kwani ukweli ulio wazi ni kwamba Chama kimechafuka; Lakini tukiweka hili pembeni kwa sasa, Vigezo vinavyotumika kuteua jina la mtu kuwa mgombea Urais (CCM) vipo vingi, na vingine ni very arbitrary na pia mchakato wake sio democratic; Lakini huo ni mjadala mwingine, na kwa sasa ningependa kujadili vigezo vifuatavyo:
- Awe na Sifa za Kuwa Mbunge Kufikia Kipindi husika
- Awe Mjumbe wa NEC Kufikia Kipindi Husika
- Jina lake liwe familiar miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa
- Asiwe amethibitika kwamba ni mla rushwa (tetesi hazitoshi)/Awe na Sifa Za Kukemea Rushwa
- Na Awe na Umri utakaovutia Wapiga Kura Vijana
Kwa mtazamo wangu, mgombea Urais kupitia CCM (2015) atateuliwa kwa kigezo aidha namba nne au namba tano, kulingana na upepo wa siasa utakavyokuwa; Kwa upande mmoja, iwapo Chadema utamweka Kijana kwa mfano
Zitto au
Lissu, CCM itajibu mapigo kwa kumweka Kijana ambae atakuwa ni
January Makamba; Kwa upande mwingine, iwapo agenda ya Vita dhidi ya Ufisadi itazidi kushika kasi chini ya Chadema, hasa iwapo CCM haitatoa kafara angalau watu wawili watatu kuonyeshe progress towards that end, na Chadema kumweka
Dr. Slaa au Hata
Lissu, CCM italazimika kumweka mgombea ambae atatumika kurudisha imani kwa wananchi kwamba Chama kipo tayari kumaliza rushwa nchini, hivyo kumsimamisha
Bernard Membe;;